Tafuta

Janga la  virusi vya corona linaweza kusababaisha vifo vya nyongeza ya watoto 51,000 walio chini ya miaka mitano katika nchi za Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini kwa mujibu wa Who na Unicef. Janga la virusi vya corona linaweza kusababaisha vifo vya nyongeza ya watoto 51,000 walio chini ya miaka mitano katika nchi za Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini kwa mujibu wa Who na Unicef. 

UNICEF/WHO:Dharura ya kiafya kwa Watoto katika Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini!

Kufikia mwishoni wa mwaka janga la virusi vya corona linaweza kusababaisha vifo vya nyongeza ya watoto 51,000 walio chini ya miaka mitano,katika eneo la Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini kwa mujibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na lile la Afya WHO.Hii inaweza kuchangiwa zaidi na mama kutowapeleka watoto katika vituo vya afya kwa kuogopa kuambukizwa na virusi.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Katika taarifa iliyotolewa tarehe 15 Juni 2020 na Mashirika ya Umoja wa Mataifa yameonya kwamba hadi mwishoni wa mwaka janga la virusi vya corona linaweza kusababaisha vifo vya nyongeza ya watoto 51,000 walio chini ya miaka mitano, katika eneo la Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini. Shirika la Afya Duniani (WHO) pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF, yamesema kuwa usumbufu wa huduma muhimu wa kiafya na lishe unaotokana na janga hilo, unahatarisha kurudisha nyuma maendeleo ya watoto kwa karibu miongo miwili katika maeneo hayo. Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa huko mjini Amman nchini Jordan, mashirika hayo  ya Umoja wa Mataifa yamezisihi serikali kufanya kazi ya kuongeza uaminifu katika mifumo ya afya ya umma, na kukuza tabia zinazofaa za utunzaji ndani familia.

Takwimu hizi za vifo vya watoto kuanzia chini ya miaka mitano katika kanda kwa miezi sita karibia ni 133,000. Kwa maana hiyo vifo 51,000 vinaweza kutoka katika ujumla wa vifo vya  watoto 184,000  walio chini ya miaka 5. Utafiti huo umefanyika katika Nchi kumi, ambapo  miongoni mwa nchi hizo ni Algeria, Gibuti, Misri, Iraq, Yordani, Marocco, Siria, Sudan, Tunisia na Yemen. Watoto ambao wako chini ya miaka  mitano katika nchi hizi kumi ni karibia watu milioni 41 ambayo inakaribia asilimia 75 ya idadi ya watoto walio chini ya miaka mitano katika kanda  ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini.

Mchanganyiko wa mantiki hizi yangechangia utabiri huu wa kusikitisha. Kwa kukabiliwa na mfadhaiko kupita kiasi, wafanyakazi wengi wa afya walioko mstari wa mbele wamegeuza jitihada zao kutoa jibu la janga hilo katika hali ambayo kuna upungufu wa vifaa vya kinga na vifaa vingine muhimu. Karantini, vizuizi vya kuzunguka na vizuizi vya uchumi vinaweza kuzuia kwa kiasi kikubwa jumuiya zaidi kupata huduma za afya. Ata hivyo pia wali wengi wanaogopa kuambukizwa virusi wakati wako kwenye vituo vya kutoa huduma za afya.

Kutokana na hofu hizo watoto na mama zao wana uwezekano wa kupoteza vitendo vya kinga kama vile chanjo, matibabu ya maambukizo ya watoto wachanga na magonjwa ya watoto, msaada wakati wa ujauzito na kuzaliwa na huduma  ya kuzuia kuongezeka kwa utapiamlo wa kukithiri. Lakini tunahitaji kuepuka hali hii kwa kuruhusu makumi ya maelfu ya watoto kusherehekea siku yao ya kuzaliwa kwa mwaka wa tano wakiwa wamezungukwa na familia na marafiki, Mashirika (WHO/UNICEF)ya Umoja wa Mataifa yamethibitisha.

15 June 2020, 10:11