WHO inasema hakuna udhuru wowote kwa ukatili dhidi ya Watoto.Tuna ushahidi wa nyenzo za kuzuia ukatili huo ambapo tunazitaka nchi zote kutekeleza.Kulinda afya na ustawi wa Watoto ni kiini cha kulinda afya yetu ya pamoja na ustawi sasa na siku za mbele. WHO inasema hakuna udhuru wowote kwa ukatili dhidi ya Watoto.Tuna ushahidi wa nyenzo za kuzuia ukatili huo ambapo tunazitaka nchi zote kutekeleza.Kulinda afya na ustawi wa Watoto ni kiini cha kulinda afya yetu ya pamoja na ustawi sasa na siku za mbele. 

UNICEF:Bilioni 1 ya watoto ni wanaathirika wa ukatili wa kimwili,kijinsia,kisaikolojia na kujeruhiwa!

Ripoti mpya iliyotolewa tarehe 18 Juni 2020 na Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya kimataifa ya kuzuia ukatili dhidi ya watoto imeonya kwamba nchi zimeshindwa kuzuia ukatili huo dhidi ya watoto na kutoa wito kwa nchi kuchukua hatua kuzuia athari kubwa zaidi.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican

Kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya kimataifa ya kuzuia ukatili dhidi ya watoto imebainisha kuwa nusu ya watoto wote duniani sawa na takribani watoto bilioni moja kila mwaka wanaathirika na ukatili wa kimwili, kingono au kisaikolojia, kujeruhiwa, kusababishiwa ulemavu na kifo kwa sababu nchi zimeshindwa kuzingatia mikakati iliyowekwa ya kuwalinda watoto. Ripoti hiyo iliyotolewa kwa pamoja na shirika la afya duniani (WHO), la kuhudumia Watoto (UNICEF), la elimu sayansi na utamaduni UNESCO, mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu kuhusu ukatili dhidi ya watoto na Wanaharakati katika mapambano dhidi ya vurugu.

Akizungumzia kuhusu ukatili huo mkurugenzi mkuu wa Shirila la afya duniani  WHO Dk. Tedros Adhaanom Ghebreyesus amesema “Hakuna udhuru wowote kwa ukatili dhidi ya Watoto. Tuna ushahidi wa nyenzo za kuzuia ukatili huo ambapo tunazitaka nchi zote kutekeleza. Kulinda afya na ustawi wa Watoto ni kiini cha kulinda afya yetu ya pamoja na ustawi sasa na siku za mbele.” Ripoti iliyopewa jina “Ripoti ya hali ya kimataifa katika kuzuia ukatili dhidi ya watoto 2020” ni ripoti ya kwanza ya aina yake ikiainisha hatua zilizopigwa katika nchi 115 chini ya mkakati wa INSPIRE ambao unajumuisha mikakati saba kwa ajili ya kuzuia na kukabiliana na ukatili dhidi ya watoto.

Ripoti imebainisha bayana haja ya nchi zote kuongeza juhudi kutekeleza mikakati hiyo. Wakati karibu nchi zote (88%) zina sheria muhimu za kuwalinda Watoto dhidi ya ukatili, chini ya nusu ya nchi hizo asilimia  (47%) zimesema mikakati hiyo inatekelezwa ipasavyo. Ripoti hiyo kwa mara ya kwanza imejumuisha makadirio ya mauaji ya watoto hususan walio chini ya umri wa miaka 18. Makadirio ya siku za nyuma yalitokana na takwimu ambazo zilijumuisha vijana wa miaka 18 hadi 19 na imebaini kwamba mwaka 2017 karibu Watoto 40,000 walikuwa wahanga wa mauaji.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa UNICEF Bi. Henrietta Fore amesema “Ukatili dhidi ya watoto siku zote umekuwa ni changamoto na sasa hali itakuwa mbaya zaidi. Hatua za watu kubaki  majumbani, shule kufungwa na vikwazo vya kutembea vimewaacha Watoto wengi wakiwa wamekwama na watu wanaowatendea ukatili, bila kuwa na maeneo salama ambayo shule hutoa mara nyingi. Ni muhimu kufanya kazi haraka kuchukua hatua kuwalinda watoto wakati huu wa na zaidi ikiwemo kuwa na huduma maalum ya wafanyakazi wa ustawi wa jamii na kuimarisha msaada kwa watoto”.

Kupitia mikakati ya INSPIRE fursa za shule tu kupitia Watoto kusajiliwa ndio zilizoonyesha hatua kubwa huku asilimia 54 ya nchi zikiripoti kwamba idadi kubwa ya Watoto wenye mahitaji walifikiwa kwa njia hiyo. Asilimia 32 hadi 37katika nchi asilimia zinachukulia hatua ya waathirika wa ukatili ambao wanaweza kupata msaada, wakati asilimia 26 ya nchi zimetoa msaada kwa wazazi na walezi. Pia ripoti inasema asilimia 21ya nchi zina mipango ya kubadilisha mila mbaya na asilimia 15 ya nchi zimefanya mabadiliko ili kutoa mazingira salama kwa ajili ya watoto. Ingawa asilimia 83 ya nchi zina takwimu za kitaifa kuhusu ukatili dhidi ya Watoto ni asilimia 21 pekee ya nchi iliyotumia takwimu hizo kuweka msingi na malengo ya kitaifa kuzuia na kukabiliana na ukatili dhidi ya watoto.

Hatua kamili inahitajika kuhakikisha kuwa msaada muhimu wa kifedha na kiufundi unapatikana katika nchi zote. Ufuatiliaji na tathmini ni ufunguo wa kuamua ni kwa kiwango gani juhudi hizi za kuzuia zinafikishwa kwa ufanisi kwa wote wanaouhitaji. Kwa mujibu wa ripoti asilimia 80 ya nchi zina mipango ya kitaifa na sera lakini ni moja ya tano tu ya nchi hizo ndizo zilizo na mipango ambayo imefadhiliwa kikamilifu  zina malengo yanayopimika. Ukosefu wa fedha za ufadhili na uwezo wa wahudumu waliohitimu ni miongoni mwa sababu zinachochangia kwa nini utekelezaji umekuwa chini.

Kujibu  COVID-19 na athari kwa watoto. Wakati wa janga la COVID19 na kufungwa kwa shule, tuliona vurugu za mtandaoni na chuki zikiongezeka pamoja na uonevu. Sasa, kwa kufungua tena shule, watoto wanaelezea wasiwasi wao juu ya kurudi shuleni, ni kwa mujibu wa Bwana Audrey Azoulay, Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO. “Ni jukumu letu pamoja kuhakikisha kuwa shule ni mazingira salama kwa watoto wote. Lazima tufikirie na kutenda kwa pamoja kumaliza uhasama mashuleni na katika jamii zetu kwa ujumla.”

Hatua za kukaa nyumbani, pamoja na kufungwa kwa shule, zimepunguza vyanzo vya kawaida vya msaada kwa familia na watu binafsi, kama marafiki, marafiki wa familia au wataalam. Hii inazidisha uwezo wa waathiriwa kutatua migogoro na kushughulika na utaratibu mpya wa maisha ya kila siku. Kulikuwapo na milio simu iliyopungua  ya  kusaidia wale ambao walikuwa wanapata unyanyasaji wa watoto na vurugu za wenzi katika maisha ya uhusiano. Na wakati jamii zikiwa mtandaoni zimekuwa muhimu kudumisha kujifunz, msaada na mchezo kwa watoto wengi, na wameweza kubaini kuongezeka kwa tabia mbaya mtandaoni pamoja na utapeli wa mtandao, tabia  ya hatari na unyanyasaji wa kijinsia.

Wakati ripoti hii ilikuwa inakaribia kukamilika, hatua za kufungwa na usumbufu wa utoaji wa huduma tayari ya ulinzi wa watoto  ilikuwa mi ngumu, ilizidi kuwa katika mazingira magumu ya watoto katika mitindo tofauti ya vurugu. Amesema hayo Najat Maalla M'jid , Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa juu ya dhuluma dhidi ya watoto.  Ili kujibu mgogoro huu, mfumo wa haki za watoto  na mantendo ya umoja, na kimataifa ni muhimu, inayohitaji uhamasishaji madhubuti wa serikali, wafadhili wa nchi mbili / mashirika ya kimataifa, mashirika ya umma, sekta ya kibinafsi na watoto, ambao kwa maoni yao lazima yasikilizwe na kuzingatiwa kiukweli ili kuhakikisha usalama unaofaa na uwezekano wa kila mtu kufanikiwa na kufikia uwezo wao kamili.

19 June 2020, 12:41