2019.03.19 uhamiaji,ukimbii na umaskini Afrika 2019.03.19 uhamiaji,ukimbii na umaskini Afrika  

UN:Watu wengi duniani kulazimika kukimbia makwao kutokana na vurugu!

Kupitia ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya wakimbizi(UNHCR)imetoa wito kwa nchi zote duniani kujitahidi zaidi kuwapa makazi mamilioni ya wakimbizi na watu wengine waliotawanywa na vita,mauaji au vitendo vingine vya kuvuruga amani na utulivu wa umma.

Ripoti mpya ya mwenendo wa kimataifa wa wakimbizi na watu waliotawanywa duniani ambayo imetolewa tarehe 18 Juni 2020 na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR inasema asilimia moja ya watu wote duniani wamelazimika kufungasha virago na kukimbia makwao kwa sababu moja au nyingine. Kupitia ripoti hiyo UNHCR imetoa wito kwa nchi zote duniani kujitahidi zaidi kuwapa makazi mamilioni ya wakimbizi na watu wengine waliotawanywa na vita, mauaji, au vitendo vingine vya kuvuruga amani na utulivu wa umma.

Kwa mujibu wa UNHCR ripoti hii iliyotolewa leo inaonyesha kwamba “kwa mara ya kwanza kutawanywa kwa lazima kuwewaathiri asilimia moja ya watu wote duniani sawa na mtu 1 katika kila watu 97 huku watu wanaoweza kurejea makwao idadi inazidi kuwa ndogo.” Ripoti hiyo ya kila mwaka ya UNHCR ambayo imetolewa siku mbili kabla ya siku ya wakimbizi duniani itakayokuwa Juni 20 inasema mwaka 2019 watu waliolazimika kutawanywa kote duniani ilikuwa milioni 79.5 ikiwa ni idadi kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa.

Ripoti  aidha  inaonyesha kupotea kwa matarajio ya wakimbizi linapokuja suala la matumaini ya kumalizika kwa kwa shida.   Katika miaka ya 1990 kwa wastani wakimbizi milioni 1.5 waliweza kurejea nyumbani kila mwaka lakini katika muongo uliopita idadi hiyo imepungua na kufikia takriban watu 385,000. Akifafanua kuhusu ripoti hiyo Kamishnaa Mkuu wa wakimbizi Bwana  Filippo Grandi amesema “Tunashuhudia mabadiliko ya hali halisi kwa watu wanaotawanywa kwamba leo hii hilo sio tu ni tatizo kubwa lililosambaa bali pia sio tatizo la muda mfupi tena .Watu hawawezi kutarajia kuishi katika hali ya sintofahamu kwa mika mingi bila fursa ya kurejea nyumbani wala matumaini ya kujenga mustakbali wao mahali waliko. Kimsingi tunahitaji mtazamo mpya na wa ukarimu kwa watu ambao wanakimbia,ambao utakuwa na lengo la kutatua migogoro ya muda mrefu ambayo ndiyo chanzo cha muktadha makubwa kwa watu hawa.”

Ripoti inasema ongezeko la watu waliotawanywa kutoka milioni 70.8 mwishoni mwa mwaka 2018 ni matokeo ya sababu kuu mbili. Ni hali mpya ya kuogopesha ya idadi kubwa ya watu waliotawanywa mwaka 2019 hususani nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC, Sahel, Yemen na Siria ambayo sasa iko katika mwaka wa kumi wa vita ambayo pekee ina wakimbizi, waomba hifadhi na wakimbizi wa ndani milioni 13.2 idadi ambayo ni moja ya sita ya idadi yote ya dunia. Pili ni hali ya uwakilishi wa Wavenezuela walio nje ya nchi ambao hawajaorodheshwa rasmi kama wakimbizi au waomba hifadhi lakini wanahitaji mipango ya kuwalinda. Ripoti imeweka bayana kwamba katika idadi yote hiyo watoto wanakadiriwa kuwa kati ya milioni 30 hadi 34 na maelfu kati yao wako peke yao bila wazazi au walezi.

18 June 2020, 14:52