Tafuta

Vatican News
Familia ya Mungu nchini Burundi inaomboleza kifo cha Rais Pierre Nkurunziza aliyefariki dunia hapo tarehe 8 Juni 2020 kwa ugonjwa wa moyo. Familia ya Mungu nchini Burundi inaomboleza kifo cha Rais Pierre Nkurunziza aliyefariki dunia hapo tarehe 8 Juni 2020 kwa ugonjwa wa moyo. 

Burundi inaomboleza kifo cha Rais Pierre Nkurunziza: 1964-2020

Taarifa zinaonesha kwamba, Rais Pierre Nkurunziza amefariki Jumatatu 8 Juni 2020 na Serikali ya Burundi kutangaza rasmi tarehe 9 Juni 2020 kwa njia ya mitandao ya kijamii. Rais Rais Pierre Nkurunziza amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 55. Amebahatika kuongoza Burundi kwa muda wa miaka 14 na siku 287, akiwa anapeperusha bendera ya Chama cha CNDD-FDD. RIP.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Rais Pierre Nkurunziza aliyetarajiwa kumaliza muda wake wa uongozi hapo tarehe 20 Agosti 2020 amefariki dunia kutokana na maradhi ya moyo, huko kwenye Hospitali ya Karuzi, iliyoko Mashariki mwa Burundi. Taarifa zinaonesha kwamba, Rais Pierre Nkurunziza amefariki Jumatatu 8 Juni 2020 na Serikali ya Burundi kutangaza rasmi tarehe 9 Juni 2020 kwa njia ya mitandao ya kijamii. Rais Rais Pierre Nkurunziza amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 55.  Amebahatika kuongoza Burundi kwa muda wa miaka 14 na siku 287, akiwa anapeperusha bendera ya Chama cha CNDD-FDD.

Rais Pierre Nkurunziza ameacha watoto watano na mjane Denise Nkurunziza ambaye anaendelea na matibabu mjini Nairobi, Kenya kutokana na kile kinachodaiwa kwamba, anashambuliwa na ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na Virusi vya Corona, COVID-19. Serikali ya Burundi imetangaza maombolezo ya siku saba kwa kupeperusha bendera nusu mlingoti. Itakumbukwa kwamba, Kulingana na katiba ya Burundi Spika wa Bunge Pascal Nyabenda tangu tarehe 10 Juni 2020 ndiye anayekaimu wadhifa wa Urais nchini Burundi. Jenerali Evariste Ndayishimiye mwenye umri wa miaka 52, ambaye ndiye Rais mteule, anatarajiwa kuapisha na hatimaye, kushika madaraka hapo tarehe 20 Agosti 2020.

Burundi
10 June 2020, 13:40