2020.06.05 Mada ya inayoongoza Siku ya Usafi wa Mikono duniani mwaka huu ni okoa maisha:wauguzi na wakunga huduma ya usafi iko mikononi mwenu. 2020.06.05 Mada ya inayoongoza Siku ya Usafi wa Mikono duniani mwaka huu ni okoa maisha:wauguzi na wakunga huduma ya usafi iko mikononi mwenu. 

WHO#coronavirus:Okoa maisha:wauguzi na wakunga huduma ya usafi iko mikononi mwenu!

Kila tarehe 5 Mei ya kila mwaka ni Siku ya usafi wa mikono duniani iliyoanza rasmi mwaka 2009 ambapo shirika la afya duniani (who)liwanaalika watu wote duniani mwaka huu kuongeza juhudi za kuhakikisha usafi wa mikono katika vituo vya afya ili kuwalinda wahudumu wa afya na wagonjwa dhidi ya maambukizi ya covid-19.Uingereza yaongoza kwa vifo zaidi Ulaya na mtazamo wa uchumi katika sekta za usafirishaji hususani mashirika ya ndege ni mgumu sana.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika kilele cha siku hii Shirika la Afya duniani WHO limesema maadhimisho ya mwaka huu yameongozwa na kaulimbiu: “Okoa maisha:wauguzi na wakunga huduma ya usafi iko mikononi mwenu”, ikienda sanjari na mwaka wa wauguzi na wakunga na lengo kuu la kutambua mchango wa wahudumu hao wa afya kama mashujaa walio msitari wa mbele na kuwashukuru na kutaambua jukumu kubwa walilonalo katika kuzuia maambukizi. Bi Elizabeth Iro ambaye ni mkuu wa wauguzi katika shirika la Afya ulimwenguni WHO ameeleza sababu ya kuihusisha siku ya mwaka huu na wauguzi na wakunga.

Katika maelezo yake kiongozi huyo amesema kwamba “Sio tu kwamba tunataka kuchagiza usafi wa mikono, kuzuia maambukizi na hulka ya kuyadhibiti lakini pia tunataka kutambua jukumu muhimu walilonalo wauguzi na wakunga katika kuzuia maambukizi yanayoweza kuepukika”. Ameongeza kuwa wauguzi na wakunga ni muhimu sana kwani kama kundi kubwa kabisa la wahudumu wa afya wanaotoa huduma kwa wagonjwa, wauguzi na wakunga ni muhimu katika kutoa huduma ya usafi. Katika nchi nyingi wanaoongoza katika kudhibiti maambukizi ni wauguzi hivyo wana nafasi kubwa katika kuzuia maambukizi hayo”. Na kuhusu kuzingatia usafi wa mikono Elizabeth amesema usafi wa mikono ni hatua moja muhimu na inayofanyakazi unayoweza kuichukua kupunguza kusambaa kwa vijidudu na kuzuia maambukizi, ikiwemo virusi vya COVID-19.

Kwa mtazamo wa maambukizi duniani kwa sasa kitovu cha maambukizi ya virusi vya corona barani Ulaya kimehamia Uingereza, kuwa nchi ya kwanza ya Ulaya kufikisha idadi ya watu zaidi ya 30,000 waliokufa kutokana na ugonjwa wa  COVID-19. Kiwango cha vifo hivi kimepita kile cha Italia ambako hadi sasa takwimu zinaonyesha kuwa watu zaidi ya 29,000 wamepoteza maisha kutokana na virusi vya corona.Nchini China imetimiza wiki tatu bila kuorodhesha kifo chochote kitokanacho na virusi vya corona.

Huko Marekani, baadhi ya majimbo yameingilia kati kusitisha hatua za kuondoa amri inayowalazimisha  wakazi kubaki nyumbani, ambayo imeathiri sehemu kubwa kiuchumi kwa nchi hiyo. Nchini Colombia, wasi wasi mkubwa ni kwa watu wa  Asilia wa Amazonia wanaopakana na nchi ya  Brazil. Maambukizi haya yameweza kufikia hata jumuiya ambayo tayari  imezingirwa na magumu mengi. Nchini Urusi maambukizi yanaendelea  kuongezeka na kufikia kesi za watu 10,000 kwa masaa 24.

Katibu wa Umoja wa Mataifa UN  Bwana Guterres ameomba serikali zote kuhakikisha matibabu kwa watu walemavu walioshambuliwa na virusi. Na serikali Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imeelezea hofu kubwa kubwa ya virusi vya corona, baada ya kuthibitisha maambukizi ya virusi hivyo kwa wafungwa karibia mia moja katika gereza la kijeshi mjini Kinshasa.

Katika kiwango cha uchumi kushuka, pia wametangaza kwa makumi ya maelfu ya wafanyakazi kwa upand wa mashirika ya Ndege ya  BnB, ya Qatar, ya Umeme Mkuu, RyanAir, Rolls-Royce, kwa kutaja kampuni chache tu zilizo kwenye shida, lakini ni makampuni mengi na viwanda vingi ambavyo bado havijuhi kama wataweza kufungua tena, kwa maana nyingine ni wakati mgumu kwa kila sekta duniani!

06 May 2020, 12:08