Vatican News
2020.05.05 Janga la  virusi ya corona au covid-19 kuyumbisha ulimwengu mzima 2020.05.05 Janga la virusi ya corona au covid-19 kuyumbisha ulimwengu mzima  (©Romolo Tavani - stock.adobe.com)

Duniani#coronavirusi:harakati za viongozi duniani kuchangia chanjo ya covid-19!

Hadi sasa watu milioni 3 na nusu wameambukizwa virusi vya corona na zaidi ya watu laki mbili na nusu wamekufa ulimwenguni kote kwa sababu ya covid-19.Viongozi duniani wameahidi kuchangisha Euro bilioni 7.4 kwa ajili ya utafiti wa chanjo.Nchi mbalimbali zimeanza hatua ya pili ya ufunguzi wa shughuli za ndani ya maeneo yao kwa uangalifu mkubwa.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Viongozi wa dunia wameahidi kuchangisha Euro Bilioni 7.4 kwa ajili ya kufanya utafiti na kutengeneza chanjo dhidi ya virusi vya corona. Ahadi hiyo imetolewa kwenye mkutano ulioitishwa na Halmashauri ya Umoja wa Ulaya uliofanyika kwa njia ya video tarehe 4 Mei 2020. Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Bi Ursula von der Leyen amesema mkutano huo ni mwanzo tu wa juhudi ndefu ambayo inatarajiwa kufanyika. Hata hivyo Umoja wa Ulaya umeahidi kuchangia Euro bilioni moja, na wakati nchini Ujerumani itatoa Euro milioni 525 na Ufaransa itatenga Euro milioni 500.

Nchi nyingine ambazo zimeahidi kuchangia ni pamoja na Norway ambayo si mwanachama wa Umoja wa Ulaya japokuwa ni mwenyekiti mwenza wa juhudi hizo! Wenyeviti wenza wa mkutano huo ni Ujerumani, Ufaransa, Uingereza, Italia, Japan na Saudi Arabia ambayo kwa sasa ni mwenyekiti wa kundi la nchi za G20.  Kwa upande wa usambaaji wa virusi vya covid-19, taarifa ni kwamba hadi sasa watu milioni 3 na nusu wameambukizwa virusi vya corona na zaidi ya laki mbili na elfu arobaini wamekufa duniani kote kutokana na COVID -19.

Hatua za kuanza hatua ya pili 2 nchini Italia wameanza bila kuwa na matatizo makubwa, japokuwa wafanyazi wengi wa maaofi wanaendelea na ‘smart working’,kufanyia kazi nyumbani na viwanda vimejizatiti kwa itifaki zilizowekwa za usalama. Hali hii ni sawa sawa na mahali pegine katika nchi za Ulaya. Kwa mfano  nchini Ubelgiji,makampuni au mashirika ambayo hayapokei watu yameanza kazi, n anchini Uhispania wamefungua hata saloon. Kwa upande wa Nigeria na Rwanda pia wamefungua shughuli zao.

Tarehe 5 Mei pia nchini Burkina Faso wameanza shughuli zao za ndani na wakati Ufaransa na Lusemburg wataaanza hatua ya II tarehe 11 Mei. Nchini Japan bado wanaendelea hadi tarehe 31 Mei. Vifo duniani kutokana na virusi vya corona imefikia watu 250,000. Na nchini Marekani ambayo sasa ina waathirika 68,000 waliokufa na inaweza kuzidi vifo 100,000 kufikia Juni, kwa mujibu wa makadirio ya wataalamu wa  uanglizi wa mrondo wa usambaaji na unenezi wa ugonjwa wa virusi. Katika kujibu mashtaka ya Marekani dhidi ya China kuhusu asili ya virusi, Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) liinasema hakuna ushahidi wa madai hayo. Na huko Uholanzi, wameweza kutambua kinga yenye uwezo wa kugeuza virusi imetambuliwa.

Utafiti mpya wa kisayansi nchini Uholanzi unabainisha kugundua kinga ambayo inaweza kuwa na  uwezo wa kubadilisha hatua ya virusi vya Sars-CoV-2 kwenye mwili wa binadamu. Utafiti na utafutaji wa tiba na chanjo dhidi ya virusi vya corona mpya unaendelea ulimwenguni kote na hapa kuna matokeo ambayo wanasema ni mazuri kwa utafiti wao uliochapishwa katika  gazeti la ‘Nature Communications’ au ‘Mawasiliano ya Asili’. Kulingana na utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Utrecht na Rotterdam, imegundulika kuwa kinga ya mwanadamu inawezesha kuyeyusha kasi ya makali ya Sars-CoV-2, yaani virusi ambavyo husababisha ugonjwa wa Covid-19. Kwa sasa ni matokeo ya kwanza yaliyopatikana kwa ngazi ya kuchoma seli, lakini inatoa ishara ya hatua zaidi ya ugunduzi wa dawa inayoweza kupambana na nguvu mpya na kuruhusu idadi ya watu kurudia katika hali yao ya kawaida.

Watafiti wanaelezea kwamba kinga ya mwili inalenga kuviweka pamoja virusi hivi na kwa maana hiyo inaweza kuwa dawa ya nguvu  ya kuzuia na hata matibabu ya ugonjwa dhidi ya ugonjwa wa Covid-19. Kwa mujibu wa Watafiti hao kuhusiana na kinga hizi wanaelezea kuwa kinga za   mwili zinaonesha kuwa ni kundi la kuahidi dawa ya mapambano dhidi ya virusi kwa sababu zinalenga kupambana na makazi ya virusi hivyo kwa watu walioathirika kwenye protini za uso wa virusi. Kinga za mwili zinapunguza makali ya virusi vipya vilivyoathiri protini kwenye uso wa virusi ambavyo usaidia kuingia ndani ya seli ngeni.  Kwa mujibu wa watafiti hao. Hii ina maana kwamba kinga za mwili zenye nguvu ambazo ushambulia kwa kawaida ufikia seli za binadamu, na ambazo zina uwezzo wa kulemaza mwingiliano. Kwa njia hii virusi huwekwa nje ya utaratibu na haviwezi kushambulia mwili wa mwenyeji na kwa hivyo hata  kuzaliana.

Maelezo ya Virusi vya covid-19 ni kama Sars-CoV: Kwa mujibu wa watafiti wanabainisha kuwa, Sars-CoV, iligunduliwa na Daktari mwitaliano Carlo Urbani (aliyekufa kutokana na virusi hivyo), ina asilimia “77,5%  ambavyo ni sawa katika muundo wa asidi ya amino msingi  na Sars-CoV-2 iliyogunduliwa kunako Desemba 2019 na daktari wa China Li Wenliang (aliyekufa  na virusi). Kuhusu ukali wa virusi, Sars-CoV inashika rekodi ya kusikitisha na vifo kwa asilimia 10% kwa idadi ya kesi zilizopatikana,  na wakati huo huo  Sars-CoV-2 hadi sasa imeonyesha ukali huo sawa na asilimia 6.8% ya kesi zilizothibitishwa kwa ngazi ya kimataifa.

05 May 2020, 13:07