Tafuta

Vatican News
Katika fursa ya kilele cha Siku ya Uhuru wa vyombo vya Mawasiliano Duniani 2020,inaongozwa na kauli mbiu ni uandishi wa habari bila uoga wala upendeleo. Katika fursa ya kilele cha Siku ya Uhuru wa vyombo vya Mawasiliano Duniani 2020,inaongozwa na kauli mbiu ni uandishi wa habari bila uoga wala upendeleo.  (AFP or licensors)

Siku ya uhuru wa vyombo vya mawasiliano:uandishi wa habari bila uoga wala upendeleo!

Tarehe 3 Mei 2020 ilikuwa ni Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Mawasiliano Duniani.Kabla ya kilele hicho,Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Antonio Guterres alikuwa amebainisha kuwa wanahabari na wafanyakazi katika vyombo vya habari ni muhimu katika kusaidia ulimwenguni kwa wakati huu kupitisha maamuzi sahihi kuhusu ugonjwa wa virusi vya COVID-19.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican

Kila tarehe 3 Mei ya kila mwana ni Siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani. Katika kuelekea kilele cha siku hiyo,  naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Antonio Guterres  siku ya Mei Mosi alisem wanahabari na wafanyakazi katika vyombo vya habari ni muhimu katika kusaidia ulimwenguni kupitisha maamuzi sahihi kuhusu ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19. Kwa njia ya ujumbe wake wa siku hiyo ambayo kwa mwaka huu imeongozwa na kauli mbiu “uandishi wa habari bila uoga wala upendeleo”, Bwana Guterres alisema katika vita dhidi ya virusi vya Corona, maamuzi ya aina hiyo yanaweza kuleta tofauti kubwa kati ya uhai na kifo.

Kutokana na mantiki hiyo  Bwana Guterrese ametoa wito kwa serikali, na wengineo kuwahakikishia wanahabari kuwa wanaweza kufanya kazi yao na hasa wakati huu wa janga la COVID-19 na hata baada ya hapo: “Vyombo vya habari vinatoa tiba: habari na uchambuzi uliothibitishwa, wa kisayansi  na wenye ukweli. Cha ajabu lakini amebainisha kwamba tangu kuanza kwa janga la Covid-19, waandishi wengi wa habari wanakabiliwa na vizuizi vya kuandika habari na hata kuadhibiwa pale wanapofanya kazi zao.”

Kadhalika akiendelea kuchambua hali hii inayowakumba waandishi, Bwana Guterres amesema:“Vizuizi vya muda mfupi katika kukabili mienendo ni muhimu katika kutokomeza COVID-19, lakini havipaswi kutumiwa vibaya kama mbinu ya kuzuia uwezo wa wanahabari kufanya kazi zao.” Vile vile hakucha kuvishukuru vyombo vya habari vinavyoendelea kuandika habari za ukweli na zenye uchambuzi yakinifu, huku wakiwawajibisha viongozi katika kila sekta na kueleza ukweli viongozi. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Guterres amesema anatambua  kwa njia ya pekee wale ambao wanatekeleza majukumu yao ya kuandika habari kuhusu afya ya umma na kutoa wito pia kwa serikali ili kulinda wanahabari na kuimarisha na kuendeleza uhuru wa vyombo vya habari ambao amesema ni muhimu kwa mustakabali wa amani, haki na haki za binadamu kwa wote.

Pamoja na kilele cha siku hii, inathibitisha wazi ni kwa jinsi gani pia waandishi wengi wa habari wameweza kukabiliana na hali halisi hasa katika vigezo vya  sheria za kukaa nyumbani. Lakini licha ya hali hiyo haikuzuia wanahabari wasitafuta mbinu mbadala, ubunifu wa kiteknolojia ambao tayari umekuwapo kuharakisha habari lakini pia namna ya kuweza kufanya kazi bila kutoka mahali ulipo.

Waandishi wengi kwa sasa wamelazimika wafanyie kazi nyumbani kwao na huku wakituma kazi  zao kupitia njia ya barua pepe na mifumo mingine ambayo imetolewa, iwe video, sauti kwa anayekuwa amebaki katika studio. Na katika vipindi ambavyo  kwa kawaida vinakwenda hewani moja kwa moja, kwa walio wengi walibadilisha utaratibu na zaidi hasa kwa vile vipindi ambavyo mara nyingi vinajumuisha mahojiano ya moja kwa moja na watu mbalimbali. Kwa kuzingatia hali hii ya kutochangamana, waandishi wengi wa habari wametumia teknolojia ya tihama na kufanya mahojiano kutumia simu za mikononi, whatsapp lakini kwanza kwa kuwatumia maswali kwa njia ya barua pepe na wao kwa urahisi kujibu kwa njia ya sauti kwenye simu na kuwezesha kwa kiasi kikubwa mawasiliano kuendelea. Teknolojia kwa sasa ni muhimu ambayo inazidi kukua na inawezesha kufika mahali ambapo ilikuwa hajafikirika hapo awali.

04 May 2020, 09:56