Tafuta

Vatican News
Ulimwengu unaendelea kuyumbishwa na virusi vya corona,vita vya hapa na pale,mabadiliko ya tabianchi,njaa,utapiamlo kwa watoto,nzige na mambo mengi.Ni muda wa kutafuta amani. Ulimwengu unaendelea kuyumbishwa na virusi vya corona,vita vya hapa na pale,mabadiliko ya tabianchi,njaa,utapiamlo kwa watoto,nzige na mambo mengi.Ni muda wa kutafuta amani. 

Jicho katika ulimwengu wa kipindi cha virusi vya covid-19!

Mamia ya vijiji wamekumbwa na mafuriko,ikiwemo ardhi ya kilimo kusombwa na maji na makumi elfu na nyumba kuharibiwa nchini India na Bangladesh.Watoto karibu milioni 10 wataathirika na utapiamlo katika kipindi cha covid-19.Waziri wa Yordani ametishia kutafakari uhusiano wa nchi yake na Israeli.RaisTrump ametangaza kujiondoa kutoka Mkataba wa Anga,unaoruhusu uhakiki wa harakati za kijeshi na udhibiti wa silaha za nchi zenye saini ya mkataba.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican

Licha ya  watu ambao tayari wamepata pigo la virusi vya corona lakini bado majanga ya asili nayo yanaingilia kati. Hiii ni kutokana na kwamba Mamia ya vijiji wamekumbwa na mafuriko, ikiwemo ardhi ya kilimo kusombwa na maji na makumi elfu na nyumba kuharibiwa. Ni kutokana na dhoruba kali iitwayo Amphan iliyotoa kipigo kikali nchini India na Bangladesh mahali ambapo wanahesabu vifo vya watu karibia 95.  Dhoruba Amphan ilipogusa ardhi kwenye mwambao wa kaskazini mashariki mwa India, upepo wake ulifikia 200km / h, huku ukitoa mawimbi ya urefu wa mita 5 juu ya pwani na kusababisha vifo na uharibifu mkubwa. Mbali na waathiriwa, kuna uharibifu mkubwa katika maeneo ya pwani, mashambani na barabara zilizojaa mafuriko, miti kuangukia taa za umeme ambapo hakuna umeme, miundo mbinu na mitambo ya nguvu  za umeme vimeharibiwa.

Utapiamlo kuathiri watoto karibu milioni 10 duniani kwa mujibu wa WFP: Kwa mujibu wa Shirika la Mpango na Chakula Duniani WFP limebainisha kuwa huenda watoto wengine milioni 10 wanaweza kuathirika kwa utapiamlo. Janga la virusi vya corona au COVID-19 huenda likawatumbukiza watoto wengine milioni 10 zaidi katika utapiamlo uliokithiri kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirika la mpango wa chakula duniani WFP. Makadirio ya WFP yanasema idadi ya watoto wanaougua utapiamlo uliotokana na lishe duniaNI inaweza kuongezeka kwa asilimia 20 kwa sababu ya mlipuko wa COVID-19. Shirika hilo limeongeza kuwa hatua za kupambana na corona ikiwemo watu kusalia majumbani na kutotembea zimeathri sana maisha ya watu na kuongeza tishio lililokuwepo kama la vita na mifumo duni ya afya, na hivyo kufanya familia nyingi hasa katika nchi masikini kushindwa kumudu lishe bora.

Naye mkurugenzi wa lishe wa WFP Lauren Landis  amesema “COVID-19 na utapiamlo ni mchanganyiko hatari sana, virusi vinaweza kuwa na athari mbaya kwa miili ya watoto ambayo tayari iko dhaifu kutokana na lishe duni. Wakati huu wa janga tunaona familia nyingi zikihaha kuwapa watoto wao lishe bora kutokana na kupoteza kipato na kuathirika kwa masoko ya vyakula, hii inaweza kusababisha mamilioni zaidi ya watoto kutumbukizwa katika utapiamlo na magonjwa. Ulimwenguni  kote watoto milioni 22 wa chini ya umri wa miaka mitano na kinamama wajawazito na wanaonyonyesha wanaitegemea WF kuwapa lishe maalum kwa ajili ya kuzuia na kutibu utapiamlo.

YORDANI: Waziri wa Yordan Bwana Omar Tazzaz ametishia kutafakari kwa upya uhusiano wa nchi yake na Israeli iwapo serikali ya litaendelea na mpango wake wa kuchukua kwa nguvu makazi ya Walowezi wa Kiyahudi katika Ukingo wa Magharibi. Waziri Mkuu wa Jordan Omar al-Razzaz kwa vyombu vya habari amesema kwamba hawatokubali hatua hiyo ya Israeli kuchukua kwa nguvu ardhi za Wapalestina, na Jordan italazimika kutafakari nyanja zote za uhusiano wake na Israeli. Mpango huo unaoungwa mkono serikali mpya ya mseto ya Israeli, iliyoapishwa Jumapili iliyopita, unaruhusu kuanzia Julai mosi kutekeleza mpango wa amani ya Mashariki ya Kati uliopendekezwa na rais wa Marekani Donald Trump wenye lengo la kumaliza mzozo wa Israeli na Palestina. Hata hivyo, Wapalestina wameupinga mpango huo wa Trump na kuungwa mkono na jumuiya ya kimataifa.

MAREKANI: Rais Donald Trump ametangaza kujiondoa kutoka Mkataba wa Anga, uitwao (“Open Skies, yaani “Anga zilizofunguka” ambao unaruhusu kufanya uhakiki wa harakati za kijeshi na udhibiti wa silaha za nchi zenye saini, ikishutumu Urusi kuwa imekiuka. Ni moja ya makubaliano muhimu zaidi ya kudhibiti silaha za nchi mbili zilizosainiwa na Urusi. Rais Trump amesema hayo siku ambayo, kwa mara ya kwanza katika miaka kumi, Marekani ilikuwa  iko tayari kufungua mazungumzo kati ya China na Urusi kuhusu kuweka vikwazo vya nyuklia.  “Nina uhusiano mzuri na Warusi, amesema rais wa Marekani, lakini hawakuheshimu makubaliano hayo”. Rais atawasilisha rasmi uamuzi huo kwa Rais Vladimir Putin Jumaa 22 Mei 2020. Washington inatarajia kumaliza makubaliano hayo ndani ya miezi sita. Na wakati nchi ya Ujerumani imemtaka Trump afikirie tena uamuzi wake.

Bendera kupepea nusu mlingoti kwa ajili ya kukumbuka wahanga wa COVID-19: Vile vile Rais wa Marekani Trump ametoa amri ya bendera kushushwa nusu mlingoti kwa siku tatu mfululizo, ili kuomboleza vifo vya Wamarekani waliokufa kutokana na virusi vya corona. Bwana Trump ameamuru hatua hiyo, baada ya idadi ya vifo vinavyotokana na ugonjwa wa COVID-19 kukaribia 100,000 nchini humo. Aidha Trump amesema bendera zitabakia nusu mlingoti Jumatatu ijayo ambayo ni Siku ya Mashujaa nchini humo, kuwakumbuka wale ambao wamepoteza maisha wakilitumikia jeshi la Marekani. Japokuwa idadi ya vifo vya kila siku nchini humo haikuongezeka, zaidi watu bado wanaendelea kupoteza maisha, na hesabu kamili kufikia vifo 94,500.

LIBIA: Jenerali Khalifa Haftar ametangaza kukerwa kwa hewa iliyokuja na ndege nane zilizotumwa kutoka katika ngome ya Urusi kwenda Siria, ili kulenga maswala ya Uturuki na vikosi vya serikali ya Tripoli katika miji yote ya Libya. Mbele ya kukabiliwa na hatari kubwa, Urusi na Uturuki. wanapendelea kusitisha mapigano mara moja na kuanza kwa upya mchakato wa kisiasa chini ya ushauri wa Umoja wa Mataifa (UN)

CONGO DRC: UNICEF imesema tangu mwanzo wa mwaka zaidi ya watu 250,000 sehemu kubwa ikiwa ni watoto wamekimbia vurugu katika vilaya ya Ituri. Mwishoni mwa mwaka janai karibia watu 200.000 walikimbia kutoka maeneo ya Djugu, Mahagi na Irumu, na kupata mahali pa kukimbila katika jumuiya zilizo wakaribisha na ambazo kwa sasa zimerudikana watu wengi huko Bunia, mji mkuu wa Ituri, na shemu zake zinazoizunguka.

Hali halisi ya kibinadamu huko Djugu kwa namna ya pekee ni mbaya kwa maana asilimia 70% ya wahudumu wa kibinadamu, iliwalazimu kusitisha operesheni zao za utoaji wa huduma kutokana na kuongezeka na hali ya ukosefu wa usalama. Karibia watu 25,000 walioongezeka katika makambi ambayo tayari yamejaa sana, wanazidi kupambania uwezekanao wa kupata maji na huduma za  usafi-kiafya zilizo salama. Hata kabla ya wenginewapya kufika walikuwa wanaweza kupata lita tano za maji kwa  siku, chini ya kiwango kilichokuwa kimependekezwa cha kila siku.

22 May 2020, 12:35