Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anahimiza juhudi za kuzishinda kauli za chuki na janga la COVID-19 kwa pamoja. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anahimiza juhudi za kuzishinda kauli za chuki na janga la COVID-19 kwa pamoja. 

COVID-19#coronavirus:kila mtu alipo asimame dhidi ya chuki,kutendeana utu na kutumia kila fursa kueneza wema!

Katika Ombi la Kimataifa la kushughulikia na kupambana na kauli za chuki wakati wa janga la virusi vya covid-19,Katibu wa Umoja wa Mataifa amesema janga hili haijali sisi ni kina nani,tunaishi wapi,tunaamini nini au kuhusu tofauti nyingine yoyote.Sisi sote lazima kuwa na mshikamano ili kukabiliana na janga hili.Kwa wanahabari kufanya juhudi zaidi kulingana na sheria za kimataifa za haki za binadamu,kuondoa ubaguzi wa rangi na mila potofu.

Mtazamo wa kupinga wageni umeenea mtandaoni na mabarabarani. Nadharia za kupinga Uyahudi zimesambaa na mashambulizi yanayoambatana na COVID-19 dhidi ya Uislam yamefanyika. Wahamiaji na wakimbizi wametajwa kama chanzo cha virusi na kisha kunyimwa huduma za matibabu. Pamoja na wazee kuwa miongoni mwa walio hatarini zaidi dharau zimeibuka zikionyesha kuwa na wao pia ndio wanaokubwa zaidi. Na waandishi wa Habari, wanaodokeza ukweli, wataalam wa afya, wafanyakazi wa misaada na watetezi wa haki za binadamu wanalengwa kwa ajili tu ya kufanya kazi zao. Hayo yamesema na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ombi lake la kimataifa kushughulikia na kupambana na kauli za chuki wakati huu wa COVID-19. Ameongeza kuwa pamoja na jitihada lakini bado janga hili linaendelea kuzusha tsunami ya chuki na chuki dhidi ya wageni, ubebeshaji lawama na vitisho.

“COVID-19 haijali sisi ni kina nani,tunaishi wapi,tunaamini nini au kuhusu tofauti nyingine yoyote. Tunahitaji kila aina ya mshikamano kulikabili janga linalotukabili la corona au COVID-19 kwa pamoja”. Katibu mkuu amesisitiza kwamba inapaswa kuchukua hatua sasa kuimarisha kinga ya jamii dhidi ya virusi vya chuki. Ndiyo maana anatoa ombi hlo tarehe 8 Mei 2020 la juhudi za kila namna kukomesha kauli za chuki duniani.

Aidha akigeukia kwa wenye mamlaka Bwana Guterres ametoa wito  kwa viongozi wa kisiasa kuonyesha mshikamano na watu wote wa jamii zao na kujenga na kuimarisha mshikamano wa kijamii. Ametoa wito kwa taasisi za elimu kuzingatia ufundishaji wa kidijitali wakati ambao mabilioni ya vijana wako mtandaoni na wakati ambao wenye itikadi kali wanatafuta kuwinda mateka na hatimaye kurubuni watu hao. Ametoa wito kwa wanahabari hususan makampuni ya mitandao ya kijamii kufanya juhudi zaidi kulingana na sheria za kimataifa za haki za binadamu, kuondoa ubaguzi wa rangi, mila potofu na na maudhui mengine mabaya.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Guterres amezitaka asasi za kiraia kuimarisha hatua za kuwafikia watu walio katika mazingira hatarishi na wadau wa kidini kutumika kama mifano ya kuheshimiana. Amemtaka kila mtu kila mahali asimame dhidi ya chuki, kutendeana utu na kutumia kila fursa kuenzeza wema. Akiongeza pia amesema mwaka jana alizindua mkakati na mpango wa hatua wa Umoja wa Mataifa dhidi ya kauali za chuki ili kuimarisha juhudi za Umoja wa Mataifa dhidi ya jinamizi hili. Kwa kuhitimisha amesema “Tunapopambana na janga hili tuna wajibu wa kulinda watu, kutokomeza unyanyapaa na kuzuia machafuko”. Na hivyo “Hebu na tuzishinde kauli za chuki na janga la COVID-19 kwa pamoja”.

09 May 2020, 13:58