Tafuta

Janga la njaa linaikabili nchi ya Zimbabwe na sasa kuongezeka kwa janga la virusi corona ipo hatari ya kuangamia kwa mamilioni ya watu.Shirika la Mpango na Chakula duniani linaomba msaada wa haraka kuepuka baa hilo. Janga la njaa linaikabili nchi ya Zimbabwe na sasa kuongezeka kwa janga la virusi corona ipo hatari ya kuangamia kwa mamilioni ya watu.Shirika la Mpango na Chakula duniani linaomba msaada wa haraka kuepuka baa hilo. 

Zimbabwe#coronavirus:milioni 4,3 ya watu leo hii wateseka kwa njaa!

Njaa inahatarisha maisha wa watu na zaidi kwa mlipuko wa janga la virusi vya corona kwa mujibu wa Shirika la Mpango na chakula(WFP).Mwishoni mwa 2019 milioni 3,8 za watu walikuwa na janga la njaa,leo hii wamefikia milioni 4,3,ikiwa na maana ya robo tatu ya watu wote.Kwa muktadha huo msaada wa kimataifa unahitajika wa haraka ili kuepusha mamilioni watu na janga hili la njaa nchini Zimbabwe.

Zimbabwe ambayo tayari ilikuwa na matatizo makubwa ya chakula kutokana na mabadiliko ya tabia nchi na kushuka sana kwa uchumi na sasa ni janga la mlipuko wa virusi vya Corona ambao unatishia kuwadumbukiza mamilioni ya watu wa nchi hiyo katika janga kubwa la njaa, kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani (WFP). Katika taarifa iliyotolewa trehe 9 Aprili 2020 Shirika la Mpango na Chakula la Umoja wa Mataifa ( WFP ) linahitaji kwa haraka msaada wa kimataifa wa dola milioni 130 ili kuweza kulisha taifa la Zimbabwe  hadi mwezi Agosti kwa operesheni za dharura za chakula ili kuzuia mamilioni ya watu walio katika hatari nchini humo kusombwa na janga la njaa zaidi.

Kwa mujibu wa shirika la mpang na chakula WFP tathimini iliyofanyika nchi nzima imeonyesha kwamba idadi ya wanachi wa Zimbabwe ambao hawana uhakika wa chakula imepanda na kufikia watu milioni 4.3 kutoka watu milioni 3.8 mwishoni mwa mwaka 2019. Kwa mujibu wa Eddie Rowe mkurugenzi wa Shirika la Mpango na Chakula aWFP nchini Zimbabwe mesema “wakati tayari Wazimbabwe wengi walikuwa wanahaha kuweka mlo mezani, mlipuko wa COVID-19 unahatarisha hali kuwa mbaya zaidi. Ni lazima tufanye kila tuwezalo ili kuzuia janga hili” amesema.

Hata hivyo msaada uliotolewa na WFP katika miezi ya karibuni umesaidia kupunguza njaa katika wilaya sita kati ya tisa zilizoorodheshwa mwishoni mwa kama jana kwamba ziko katika daraja la nne la dharura ya uhakika wa chakula. Kwa sasa shirika hilo la WFP linasema kiwango cha njaa katika wilaya hizo kimeshuka hata hivyo wilaya 56 kati ya 60 za nchi hiyo hivi sasa zimeelezewa kuwa katika mgogoro mkubwa wa chakula. WFP inazisaidia jamii ambazo ziko katika mgogoro na dharura kubwa ya kutokuwa na uhakika wa chakula. WFP inapanga kuwasaidia watu milioni 4.1 mwezi huu wa Aprili ingawa uhaba wa fedha umezuia kufikia lengo la kila mwezi tangu mwanzo wa mwaka huu. Mwezi Machi WFP imewafikia Wazimbabwe milioni 3.7 wasiojiweza.

Kwa mujibu wa shirika la Mpango na Chakula la WFP,  jumla ya watu wasio na uhakika wa chakula nchini Zimbabwe sasa ni  I milioni 7.7 ambao ni nusu ya watu wote wa taifa hilo. Dola milioni 130 zinazohitajika haraka na WFP ni sehemu ya msaada wa jumla wa chakula ambao unahitaji dola milioni 472 kulisaidia taifa hilo hadi Desemba. Uzalishaji wa nafaka mwaka 2019 ulikuwa nusu ya ilivyokuwa mwaka 2018 na ni chini ya nusu ya mahitaji ya kitaifa. Wataalam wanatabiri kwamba mavuno ya 2020 yatakuwa ni mabaya zaidi. Asilimia kubwa ya chakula cha Zimbabwe kinazalishwa na wakulima wa kawaida ambao wanategemea mvua pekee.

Kwa mujibu wa Shirika la Mpang na chakula , wanasema mfumko wa bei ya vyakula wamelazimishwa wazimbabwe wengi kupunguza idadi ya milo, kuuza vitu vyao vya thamani na kupata fedha za kununua chakula na kutumbukia katika madeni. Pamoja na hayo limeongezeka sasa janga la COVID-19 ambalo linatishia kufanya hali kuwa mbayaaidi  ya kiuchumi nchini Zimbabwe na kuzusha janga la njaa linalokithiri maisha ya watu wote wa mijini na vijijini.

09 April 2020, 14:59