Zimbabwe#coronavirus:Chama cha Kikristo kutoa ombi kwa ajili ya nchi maskini zipokee msaada kujibu janga la sasa!
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican
Baada ya kutangazwa wiki iliyopita kwa upande wa mataifa makuu tajiri duniani (G20) kusimamisha kwa muda ulipwaji wa madeni kwa nchi zinazoendelea, kuanzia Mei Mosi hadi tarehe 31 Desemba 2020, Chama cha Kikristo cha kutoa msaada cha Uingereza kinatoa ombi la haraka kwamba Zimbabwe, hata kama haipo kwenye makubaliano, ipokee misaada inayohitajika ili kujibu janga la Covid-19.
Kusimamishwa kwa deni hilo, ambalo halitafutwa, lakini lazima lilipwe kati ya mwaka 2022 na 2024, pamoja na riba iliyopatikana kwa muda, inatazama nchi 77 ambazo ni sehemu ya mpango wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa (IDA), wakala ya Benki ya Dunia ambayo inasaidia nchi masikini zaidi ulimwenguni, au zile zenye kipato cha chini. Zimbabwe ni sehemu ya nchi inayoshiriki kwa kijujuu tu katika IDA na kwa sababu za kiufundi, ilitengwa kwenye mkataba huo. Ikiwa mpango wa sasa wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) umeundwa tena na msaada wa wadau, basi Zimbabwe inaweza kusimamishwa malipo ya deni kwa upande wa Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Afrika na Benki ya Ulaya kwa uwekezaji, kati ya wadai wengine wa kimataifa.
Chama cha kikristo cha msaada kinaamini kwamba kutengwa kwa nchi hiyo kwenye kifurushi siyo haki, kwa sababu ya hali ngumu ya kiafya iliyosababishwa na Covid-19 na athari zake za kiuchumi kwa watu masikini zaidi na walio katika mazingira magumu zaidi. Kwa maana hiyo wanaomba kwamba Uingereza na serikali nyingine zisaidi sasa kufadhili asasi za kiraia kwa kushirikiana na sekta binafsi, katika kusaidia moja kwa moja masikini, huku wakishughulikia miundombinu, huduma za afya na ulinzi wa vikundi vilivyo hatarini zaidi. Kwa sababu mara tu kesi za Covid-19 zitakapofikia kizingiti fulani, mfumo dhaifu wa afya wa nchi hautaweza kufana hiyo.
Nicholas Shamano, Mhusika wa Cahama cha Kikristo cha msaada nchini Zimbabwe, amesisitiza pia kuwa “kukosekana kwa mpango wa IMF nchini Zimbabwe siyo sababu ya kuwaacha watu wateseke zaidi na janga hili”. Umuhimu wa kibinadamu kwa sasa ni ule wa kuhakikisha kuwa “jamii ya kimataifa inawasaidia Wazimbabwe kupambana na athari mbaya za virusi vya corona na mgogoro wa uchumi duniani”.