Tafuta

Vatican News
2020.04.22 Janga la virusi vya corona vinahatarisha baa la njaa katika maeneo yaliyokuwa tayari yamekumbwa na uhaba huo duninani kote kwa mujibu ripoti ya pamoja ya mashirika ya Kimataifa. 2020.04.22 Janga la virusi vya corona vinahatarisha baa la njaa katika maeneo yaliyokuwa tayari yamekumbwa na uhaba huo duninani kote kwa mujibu ripoti ya pamoja ya mashirika ya Kimataifa.  (WFP/Gabriela Vivacqua)

Mtazamo katika Dunia#covid-19:Janga la corona kuhatarisha ongezeko la njaa!

Kwa mujibu wa Mashirika Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP,la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA,la kuhudumia watoto UNICEF,la chakula na kilimo FAO, Umoja wa Nchi za Ulaya EU,naUSAID yamesema Janga la virusi vya corona linahatarisha kuongezeka idadi ya watu walio katika hatari la baa la njaa.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Janga la virusi vya corona au covid-19 linahatarisha kuongezeka idadi ya watu walio katika hatari ya baa la  njaa ulimwenguni na kusababisha kile kiitwacho “janga la kibinadamu la ulimwengu”. Hii ni taarifa  kutoka kwa  Mashirika Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP, la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA, la kuhudumia watoto UNICEF, la chakula na kilimo FAO, Umoja wa Nchi za Ualaya EU, na USAID. Hata hivyo  Ugonjwa wa homa ya mapafu tayari umekwisha waua zaidi ya watu 174,000 ulimwenguni.

Kwa mujibu wa Ripoti mpya iliyotolewa tarehe 22 Aprili 2020 na mashirika ya Umoja wa Mataifa, WFP,OCHA,UNICEF,FAO,EU, na USAID iliyopewa jina “Muungano wa kimataifa dhidi ya mgogoro wa chakula” inaonyesha kwamba mwishoni mwa mwaka 2019 watu milioni 135 katika nchi 55 walikabiliwa na kutokuwa na uhakika wa chakula Na zaidi ya hapo katika nchi 55 zenye mgogoro wa chakula zilizoangaziwa kwenye ripoti hii watoto milioni 75 walikuwa na matatizo ya kudumaa na milioni 17 waathirika la kupoteza uzito kutokana na utapiamlo kwa mwaka 2019.

Katika Ripoti hiyo inasema hiki ni kiwango cha juu sana cha kutokuwa na uhakika wa chakula na utapiamlo kilichoorodheshwa na mtandao huo tangu kutolewa kwa ripoti ya kwanza mwaka 2017. Mwaka huohuo wa 2019 ripoti imewaweka watu milioni 183 katika daraja la pili la kutokuwa na uhakika wa chakula ambalo ni sawa na kukabiliwa na njaa kubwa na kuwa katika hatihati ya kutumbukia katika mgogoro wa chakula endapo watakabiliwa na zahma nyingine kubwa kama janga la COVID-19

CAMERUN:ugunduzi wa maaskari kuuwa watu 13 nchini Cameruni: Kwa upande wa utawala wa urais nchini  Camerun Jumanne 21 Aprili wametambua ukweli  kwamba raia 13, pamoja na watoto 10, waliuawa na askari watatu na wasaidizi katika kijiji cha magharibi kaskazini katikati ya mwezi Februari. Hata hivyo mauaji hayo yalikuwa tamezua maandamano makubwa ya kimataifa na Yaounde mpaka sasa walikuwa mekataa jukumu lolote kwa upande wa jeshi lake.

Musumbiji: raia 50 wameuwa tarehe 7 Aprili: Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari mahalia iliyotolewa tarehe 21 Aprili 2020 vimebainisha kuwa zaidi ya raia 50 waliuawa kunako  Aprili 7 katika kijiji cha kaskazini mashariki mwa Msumbiji katika shambulio la vikundi vya jihad.

22 April 2020, 13:17