Tafuta

Tarehe 2 Aprili ya kila mwaka umaoja wa mataifa unakumbusha elimu kuhusu USONJI(AUTISM) kauli mbiu ya 2020 ni kuelekea utu uzima. Tarehe 2 Aprili ya kila mwaka umaoja wa mataifa unakumbusha elimu kuhusu USONJI(AUTISM) kauli mbiu ya 2020 ni kuelekea utu uzima. 

Kuelekea utu uzima ndiyo kauli mbiu ya siku ya USONJI duniani 2020!

Katika Kilele cha Siku ya USONJI duniani yaani kwa kingereza ni AUTISM iadhimishwayo na Umoja wa Mataifa inaongozwa na kauli mbiu “Kuekelea utu Uzima” ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema watu wenye usonji wana haki ya kufanya uamuzi,kuwa huru na kujitawala pamoja na haki za elimu na ajira sawa na wengine.

Kupitia ujumbe wake  maalum tarehe 2 Aprili 2020  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Antonio Guterres amesema siku ya uelimishaji kuhusu usonji inaadhimishwa kwa kutambua na kusherehekea haki za watu wenye AUTISM yaani USONJI kwamba “Mwaka huu siku hii inaadhimishwa katikati ya janga la kimataifa la kiafya ambalo hatujawahi kulishuhudia katika maisha yetu, janga ambalo linawaweka watu wenye usonji katika hatari kubwa kutokana na virusi vya Corona na athari zake katika jamii.” Bwana Guterres ameongeza kusema  kuwa “watu wenye usonji wana haki ya kufanya maamuzi, kuwa huru na kujitawala pamoja na haki ya elimu na ajira sawa na wengine. Lakini kuvurugika kwa mfumo na mitandao ya msaada kutokana na virusi vya corona, COVID-19 kumezidisha vikwazo ambavyo watu wenye usonji wanakumbana navyo katika kutekeleza haki zao.”

Haki za kimataifa na za binadamu zile za watu wenye ulemavu

Katika siku ya Kimataifa ya Usonji duniani iadhimishwayo kila tarehe 2 Aprili, Katibu Mkuu amesisitiza ni lazima kuhakikisha kwamba usumbufu wa muda mrefu uliosababishwa na dharura ya janga hili hakuchangii kurudisha nyuma haki za watu wenye usonji ambazo mashirika yanayowawakilisha yamefanya kazi kubwa kuzifikia. Amekumbusha kwamba “haki za kimataifa za binadamu zikiwemo za watu wenye ulemavu haipaswi kukiukwa wakati huu wa COVIDI-19. Serikali zinawajibu wa kuhakikisha hatua zao zinajumuisha watu wenye usonji. Watu wenye usonji hawapaswi kukabiliwa na ubaguzi wakati wanatafuta huduma za afya. Wanastahili kuendelea kuwa na fursa ya mfumo wa msaada unaohitajika ili waweze kubali majumbani kwao na katika jamii zao wakati wa janga, badala ya kukabiliwa na matarajio ya kulazimishwa kubaki kwenye vituo.”

Jukumu la kuhakikisha mahitaji yao

Bwana Guterres ameongeza kuwa kila mmoja ana jukumu la kufanya kuhakikisha mahitaji ya watu wanaoathirika zaidi na COVID-19 yanatimizwa katika kipindi hiki kigumu. Pia amesema kwamba taarifa kuhusu hatua za kujikinga zinapaswa kufikishwa kwa njia ambayo inaweza kuwafikia kwa urahisi. “Pia ni lazima tutambue kwamba wakati shule zinapofundishwa kwa njia ya mtandao, wanafunzi wasio na njia za kujifunza wanaweza kuwa katika wakati mgumu na hiyo ni pamoja na maeneo ya kazi na kufanyia kazi nje ya mazingira ya kazi.”

Haki za wenye usonji zikabiliwe

Katibu Mkuu Bwana Guterres amesema hata katika nyakati hizi zisizotabirika ni lazima tuahidi kuwasiliana na watu wenye ulemavu na mashirika yanayowawakilisha na kuhakikisha kwamba njia zetu ambazo si za asili za kufanya kazi, kusoma na kujihusisha na wengine pamoja na juhudi za kimataifa za kukabiliana na virusi vya corona ni jumuishi na zinapatikana kwa watu wote wakiwemo wenye usonji. Haki za watu wenye usonji ni lazima zizingatiwe katika kuandaa mikakati na hatua zote za kukabiliana na virusi vya COVID-19. Aidha amesema “Katika siku hii ya uelimishaji kuhusu usonji duniani hebu tusimame pamoja , tusaidiane na kuonyesha mshikamano na watu wenye usonji.”

Utambue Usonji ni nini

Ugonjwa wa Usonji kwa kiingereza Autism, ni ugonjwa ambao kwa mujibu wa shirika la afya duniani, WHO  hukumba mtoto mmoja kati ya kila watoto 160 duniani. Usonji ni tatizo la kibaiolojia analopata mtoto anapokuwa tumboni mwa mama yake na dalili huonekana kuanzia umri wa miaka mitatu na kuendelea. Kabla ya hapo wataalam wanasema ni mara chache kuona dalili hizo ambapo zinapojitokeza mtoto hukosa mbinu za uhusiano, anashindwa kuzungumza na wakati mwingine kurukaruka na hata kujing’ata.

Katika mataifa mengine watoto kama hawa hutelekezwa

Watoto kama hawa kutokana na tatizo hilo wengine katika mataifa mengine hutelekezwa na jamii na kunyimwa haki zao za msingi ikiwemo kuishi, kuendelezwa kimasomo, kulindwa na kushirikishwa. Hata hivyo katika siku ya kimataifa ya usonji duniani  ifanyikayo kila tarehe 2 Aprili, Umoja wa Mataifa umetaka elimu zaidi jamii ibadili mitazamo yake kwani watoto wenye usonji wakipatiwa huduma mapema wanaweza kushiriki vyema katika jamii zao kwani wana uelewa wa hali  ya juu. Katika mataifa yaliyoendelea, watoto wengi shuleni au madarasani wanakuwa na mwalimu mwingine wa ziada kwa ajili ya watoto hao, maana mara nyingi mtoto mwenden wake unaweza kuleta usumbufu kwa wengine, na nk watoto wengi sana.

 

02 April 2020, 13:49