Tafuta

Janga la Corona licha ya kushusha uchumi duniani, watu walio katika mazingira magumu zaidi hasa wakulima na wafanyabiashara wadogo watateseka sana. Janga la Corona licha ya kushusha uchumi duniani, watu walio katika mazingira magumu zaidi hasa wakulima na wafanyabiashara wadogo watateseka sana.  

Janga kubwa zaidi ni hatari katika maeneo ya vijijini!

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD),linathibitisha hatari iliyopo inayosababishwa na janga la covid-19 na ambalo pia linatazama uchumi zaidi kwa watu wanaoishi vijijini:kwa jinsi hii tangu 20 Aprili limezinduliwa mkakati wa mfuko wa IFAD kwa lengo hilo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kwa ngazi ya  Kimataifa, kuna majadiliano mengi kuhusu kushuka kwa uchumi kama matokeo ya Covid-19. Kwa namna ya pekee  kengele kubwa ni ile ya uwepo wa watu walio katika mazingira magumu zaidi duniani, hasa kwa wakulima. Tangu tarehe 20 Aprili umezinduliwa  mfuko wa Ifad ambao utafanya kazi kwa ajili ya lengo hilo. Katika mahojiano na  mmoja wa viongozi wa Umoja wa Mataifa, Paolo Silveri amethibitisha kuwa katika dunia asilima 80 ya watu ni maskini na wako hatari ya ukosefu wa chakula na wanaisha maeneo ya vijiji.

Hata kabla ya kuzuka kwa janga la covid-19 zaidi ya watu milioni 820 walikuwa wanateseka na njaa kila siku. Na kwa muktadha wa kiuchumi kufuatia na janga la virusi vya corona, kwa ngazi la kidunia inaweza kusababisha ongezeko la masikini zaidi ya watu milioni 500. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo(IFAD) umekwisha pata kutoka kwa kwa serikali zaidi ya nchi 65 zikiomba msaada. Hatari inatazama ustawi, msimamo wa ulimwengu na maendeleo yote yaliyopatikana katika miaka ya hivi karibuni, ambapo yanaelekea kurudia nyumba katika  umaskini

Kwa sababu ya vizuizi vilivyowekwa vya harakati ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo kuenea wakulima wengi wadogo wanashindwa kufikia masoko kuuza bidhaa zao au kununua vifaa muhimu, kama mbegu au mbolea kwa mujibu wa kiongozi huo. Kufungwa kwa njia kuu za usafirishaji wa kibiashara na marufuku ya kuuza bidhaa nje kumeathiri vibaya mifumo ya chakula cha kilimo. Minyororo ya uzalishaji mzima iko hatari ya kusitishwa. Kati ya jamii zilizo hatarini zaidi ni zile za wafanyakazi wa siku na wale wanaofanya kazi katika biashara ndogo ndogo au biashara isiyo rasmi, na mara nyingi hawa ni wanawake na vijana.

Kwa kuongezea, kutazama wafanyakazi katika miji mahali ambapo shughuli za kiuchumi na kibiashara zimefungwa  zinawakilisha  mzigo zaidi kwa familia za maeneo ya vijijini, ambao pia wataacha kupokea chochote ambacho walikuwa wanapokea na kuhitaji sana. Ili kuzuia uharibifu mkubwa kwa uchumi wa vijijini, ni muhimu kuhakikisha kuwa kilimo, minyororo ya chakula, masoko na biashara vinaendelea kufanya kazi, kwa mujibu wa Bwana  Paolo Silveri, mhusika mkuu wa IFAD katika eneo la Amerika ya Kusini na visiwa vya Carribbien.

20 April 2020, 18:16