2020.04.26 Viongozi wa kimataifa kuzindua mkakati na kuzungumzia juu ya harakati za utafiti na maendeleo hasa katika utafutaji na upatikanaji wa chanjo itakayofaa kwa virusi vya corona. 2020.04.26 Viongozi wa kimataifa kuzindua mkakati na kuzungumzia juu ya harakati za utafiti na maendeleo hasa katika utafutaji na upatikanaji wa chanjo itakayofaa kwa virusi vya corona. 

Covid-19#Mkakati mpya wazinduliwa kukabiliana na virusi vya corona!

Tarehe 24 Aprili 2020 umezinduliwa mkakati mpya wa kimataifa ili kuhamasisha zaidi maendeleo ya uzalishaji na fursa sawa ya nyenzo mpya za kukabiliana na janga la virusi vya corona au COVID-19 hasa katika harakati za upatikanaji wa chanjo.

Mkakati mpya wa kimataifa umezinduliwa tarehe 24 Aprili 2020 katika harakati za kusongeza mbele juhudi za maendeleo, uzalishaji na fursa sawa ya nyenzo mpya za kukabiliana na janga la virusi vya corona au COVID-19 na Zaidi kwa  upatikanaji wa chanjo ambayo inaweza kusaidia madhara haya. Katika uzinduzi huo umewaunganisha pamoja viongozi wa dunia, sekta binafsi, wadau wa masuala ya kibinadamu na washirika wengine kuchagiza afya, kuhakikisha dunia iko salama na kuendelema mema kwa umma.

Afya ya binadamu ni faida bora ya kimataifa kwa umma

Katika uzinduzi huo uliofanyika kwa njia ya mtandao na ambao umeandaliwa na shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO, Rais wa Ufaransa, tume ya Muungano wa Ulaya, Bill na Melinda Gates na kuhusisha washiriki wengine mbalimbali, naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Antonio Guterres akizungumza kwa njia ya video  amesema “Afya ya binadamu ni faida bora ya kimataifa kwa umma,  leo tunakabiliwa na adui mkubwa wa umma ambaye hajawahi kushuhudiwa katika dunia hii iliyounganika na ambayo hakuna yeyote aliye salama hadi pale sote tutakapokuwa salama. Aidha ameongeza kusema kuwa COVID-19 haiheshimu mipaka, mahali popote ni tishio kwa watu na hivyo Dunia inahitaji maendeleo, uzalishaji na utoaji wa usawa wa chanjo salama na inayofaa ya COVID-19, matibabu na uchunguzi.”

Inahitajika Chanjo na matibabu ambayo ni ya gharama nafuu,salama, yanayofanyakazi

Aidha Katibu Mkuu Guterres  amesisitiza kwamba na “Si chanjo au matibabu kwa nchi moja au ukanda mmoja au nusu ya dunia lakini chanjo na matibabu ambayo ni ya gharama nafuu, salama, yanayofanyakazi, rahisi kuyafanya na yanayopatikana ulimwenguni kote kwa kila mtu kila mahali. Dunia huru bila COVID-19 inahitaji juhudi kubwa za afya za umma kuwahi kutokea katika historia”.

Lazima kushirikiana takwimu na uwezo wa uzalishaji lazima uandaliwe

Bwana Guterres amehimiza kuwa “Lazima kushirikiana takwimu, uwezo wa uzalishaji lazima uandaliwe, rasilimali lazima zikusanywe, jamii lazima zishirikishwe na siasa lazima ziwekwe kando. Najua tunaweza kufanya hili, najua tunaweza kuwapa watu kipaumbele cha kwanza na nyenzo hizo mpya lazima ziwe mfano muhimu na wa wazi jambo jema kwa umma.” Kwa kuongeza amesema kwa muda mrefu sana hatujathamini au kuwekeza katika bidhaa za umma kama mazingira safi, usalama mtandaoni, amani na orodha inaendelea.

Tuko katika vita vya maisha yetu na tuko katika janga hili pamoja

Kwa kuhitimisha amesema “hebu na tuache hili liwe somo moja muhimu la janga hili la COVID-19, haja ya uharaka wa dharura mpya ya kuunga mkono bidhaa za umma na huduma za afya kwa wote. Tuko katika vita vya maisha yetu, na tuko katika janga hili pamoja na tutajikwamua katika janga hili tukiwa na nguvu kwa pamoja.” Katibu Mkuu Bwana Guterres amewashukuru wote walioshiriki mkutano huo na kuonyesha mshikamano wa kimataifa dhidi ya janga la COVID-19 ambalo linaitikisa dunia kwa sasa.

25 April 2020, 10:51