Tafuta

Shujaa wangu ni wewe,ni jina la kitabu kipya kilichozinduliwa hivi karibuni kusaidia watoto kuelewa kuhusu ugonjwa wa virusi vya Corona -COVID-19 Shujaa wangu ni wewe,ni jina la kitabu kipya kilichozinduliwa hivi karibuni kusaidia watoto kuelewa kuhusu ugonjwa wa virusi vya Corona -COVID-19 

Covid-19#kimezinduliwa kitabu cha kuelimisha watoto juu ya covid-19!

Ili kuweza kuwasaidia watoto uelewa na ufahamu wa kina kuhusu ugonjwa la virusi vya covid-19,zaidi ya mashirika 50 ya kibinadamu yakiwemo ya Umoja wa Mataifa yameandaa kitabu kipya.Janga la virusi vya corona linaendelea kuathiri nchi nyingi hata bara la Amerika ya Kusini mfano Equador ambapo kikosi cha nguvu kazi kimeweza kuondoa maiti karibu mia 800 kutoka majumbani na wengine 631 kutoka mahospitalini.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Hivi karibuni Mashirika ya Umoja wa Mataifa kama la afya, (WHO), la kuhudumia watoto, (UNICEF), la kuhudumia wakimbizi, (UNHCR) na lile la elimu, sayansi na utamaduni, (UNESCO) na wadau wao likiwemo la  Save the Children na shirikisho la vyama vya msalaba mwenkundu wameandaa kitabu kipya kwa ajili ya kuwasaidia wato wawe na ulewa na ufahamu kwa kina kuhusu ugonjwa virusi vya corona au covid-19. Kwa msaada wa kikaragosi cha kufikirika, kiitwacho Ario, kitabu  hicho kiitwacho “Shujaa wangu ni Wewe, Jinsi gani watoto wanaweza kupambana na COVID-19” kinaeleza ni kwa vipi watoto wanaweza kujilinda wenyewe, familia zao na marafiki dhidi ya virusi vya Corona na ni kwa vipi wanaweza kukabili hisia pindi wanapokumbana na hali halisi inayobadilika haraka na mara kwa mara.

Walengwa ni watoto wenye umri wa kuanzia miaka 6 hadi 11 na ni mradi wa kamati ya mashirika mbalimbali kuhusu afya ya akili na usaidizi wa kisaikolojia katika mazingira ya dharura. Mwanzoni mwa maandalizi ya kitabu hicho, zaidi ya watu 17000 wakiwemo watoto, wazazi, walezi na walimu kutoka kona mbalimbali duniani walielezea jinsi gani wanakabiliana na janga la covid-19. Michango  yao ilikuwa muhimu kwa mwandishi wa kitabu na mchoraji Helen Patuck na timu nzima katika kuhakikisha simulizi na ujumbe vinaendana na watoto wa hali tofauti na maeneo mbalimbali duniani. Akizungumzia kitabu hicho, Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dk. Tedros Ghebreyesus, amesema, “majanga ya awali ya kibinadamu yametuonesha ni jinsi gani muhimu kushugulikia hofu na wasiwasi wa vijana pindi maisha waliyoyazoea yanapobadilika. Tunatumaini kitabu hiki chenye picha kinachosafirisha watoto maeneo mbalimbali duniani kitasaidia waelewe kile wanachoweza kufanya na kuwa na mtazamo chanya na kuwa salama wakati wa mlipuko wa covid-19.”

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF Bi. Henrietta Fore, amesema kuwa ulimwenguni  kote, maisha ya watoto yamebadilika, wengi wao katika nchi zenye karantini na hivyo, “kitabu hiki kitasaidia watoto kuelewa na kukabiliana na hali ya sasa na kujifunza ni kwa vipi wanaweza kuchukua hatua ndogo tu na kuwa mashujaa katika simulizi zao.” Ili kuhakikisha kitabu hicho kinafikia watoto wengi kadri iwezekanavyo, kitatafsiriwa kwa lugha nyingi, ambapo kitabu hicho kilipozinduliwa tarehe 9 Aprili 2020 kilikuwa tayari  katika lugha 6,  huku nyingine 30 zikiwa kwenye maandalizi ya kutafsri. Kuhusiana na upatikanaji wa kitabu hiki. Kitabu hicho kinaweza kusomwa kwa maandishi kwenye mtandao na pia kusikilizwa kwa sauti kwenye intaneti.

Ikumbukwe: Ugonjwa wa virusi vya Corona ulitangazwa dharura ya afya ya binadamu mwezi Januari mwaka huu na hadi sasa umeshasambaa katika nchi 212 ulimwenguni kote na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 115,257  kati ya wagonjwa 1,866,510. Marekani ni nchi iliyoambukizwa zaidi kwani inahesabika vifo karibu 22.020, inafuata vifo nchini Italia 19.899, Uhispania  vifo 16.972, Ufaransa 14.393 na Uingereza 10.612.  UjerumanIn GermaniUjerumani maambukizi karibu 130,000. Kesi ya walipona imefikia asilimia 50% ( Nchini Italia ni asilimia 22%. Ufaransa wanaelekea kuendelea na uthibiti wa kufunga kufikia katikati ya mwezi Mei. Jumatatu 13 Apili 2020 Rais Emmanuel Macron atahutubia Taifa.

Bara la Amerika ya Kusini, nchini Ecuador wameondoa maiti 800 kutoka katika nyumba zao. Polisi inchini Equador kwa wiki tatu za mwisho wameweza kuondoa karibu maiti 800 kutoka katika nyumba binafsi (private) huko Guayaquil, mji ambao ni wa uchumi wa nchi hiyo na ambao ndiyo umekuwa kitovu cha janga la corona katika nchi hiyo, baada janga kuingia hata katika mahospitali na katika huduma za kufanya mazishi. Kikosi cha nguvu kazi cha Polisi na wanajeshi kilichoundwa na serikali katika kuendesha shughuli za janga hili, wameondoa maiti  771 kutoka katika majumba binafsi  na maiti 631 kutoka hospitalini. Ni kikosi hicho hicho nguvu kazi kilichohusika na kuzima maiti hizo. Pamoja na janga jipya la virusi vya corona bado hali halisi ya wahamiaji na wakimbizi inaendelea na ambao wengine wamenusurika na wengine kuathirika katika mwambao wa Pozzalo nchini Italia.

13 April 2020, 14:39