Tafuta

TAREHE 22 APRILI YA KILA MWAKA NI SIKU YA KIMATAIFA YA KUENZI MAMA DUNIA TAREHE 22 APRILI YA KILA MWAKA NI SIKU YA KIMATAIFA YA KUENZI MAMA DUNIA 

22 Aprili ni Siku ya Kimataifa ya kuenzi Mama Dunia!

Tarehe 22 Machi ni Siku ya Kimataifa ya kuienzi na kuithamini dunia iliyoanzishwa kwa mara ya kwanza miaka 50 iliyopita.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira wanabainisha siku hii ni kutaka kuonyesha umuhimu uliopo wa kutegemeana baina ya binadamu,viumbe vingine na dunia.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kila tarehe 22 Aprili ya kila mwaka ni  Siku ya Kimataifa ya kuenzi Dunia ambapo siku hii ilianza kuadhimishwa miaka 50 iliyopita. Siku kama hii ya kuienzi na kuithamini dunia mama ni kutaka kuonyesha umuhimu uliopo wa kutegemeana baina ya binadamu, viumbe vingine na dunia. Uharibifu wa sayari dunia ni mkubwa sana na afya za wakazi wa dunia, na ambapo kuna hatari ikiwa hakuna hatua zozote zinazochukuliwa kwa sasa. Shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia Mazingira mara kwa mara wamekuwa wakihimiza  suala hili kwa mfano katika ripoti ya mwaka jana kufuatia utafiti wa mazingira kwa kipindi cha miaka mitano, uliofanywa na wanasayansi 250 na wataalam kutoka takriban nchi 70, wlikuwa wakidhibitisha kuwa ikiwa hatua za haraka za kulinda mazingira au miji hazitachukuliwa, ifikapo katikati ya karne hii, katika maeneo kama vile ya Asia, Mashariki ya kati na Afrika yatashuhudia watu wake wakifariki dunia mapema na visiwa vingi kutowekwa. Kadhalika katika ripoti yao walionya kuwa vichafuzi katika maji yasiyo ya chumvi vitakuwa sugu dhidi ya dawa za vijiuaviumbe kuwa sababu kuu ya vifo ifikapo mwaka 2050.

Wakati Mama Duniani anatutumia ujumbe wake: Katika tovuti ya Umoja wa Mataifa, Shirila linaloshughulika mazingira linabaini kuwa, Mama Duniani anahimiza wito wa kuchukua hatua, kwani Asili inateseka, moto wa Australia, rekodi za joto na uvamizi mbaya wa nzige nchini Kenya na sasa sasa tunakabiliwa na janga la COVID -19, kiungo cha afya ulimwenguni kinachounganisha na afya ya mfumo wetu wa mazingira. Aidha Mabadiliko ya hali ya hewa, mabadiliko ya mwanadamu katika maumbile na uhalifu unaovuruga bianuwai, kama ukataji miti, mabadiliko ya utumiaji hovyo wa ardhi, kuongezeka kwa kilimo na ufugaji au biashara inayokua ya wanyama pori isiyo ruhusiwa vinaweza kuongeza mawasiliano na maambukizi ya magonjwa ya kuambukiza kutoka kwa wanyama kwenda wanadamu (zoonotic disease) kama ya COVID-19.

Kutoka katika ugonjwa mmoja mpya wa kuambukiza ambao hujitokeza kwa wanadamu kila baada ya miezi 4,  asilimia 75% ya magonjwa haya yanayoibuka hutoka kwa wanyama, kkwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira. Hii inaonyesha uhusiano wa karibu kati ya binadamu, wanyama na afya ya mazingira. Inayoonekana, athari chanya, iwe kupitia uboreshaji wa hewa au kupunguzwa kwa uzalishaji wa gesi chafu kwamba ni ya muda mfupi, kwa sababu inakuja nyuma ya kushuka kwa uchumi mbaya na dhiki za wanadamu.

Umuhimu wa bioanuwai kwa wanadamu: Mlipuko wa virusi vya Corona umeweka mahali pa kubwa afya ya umma na uchumi wa ulimwengu katika hatari, lakini hata katika utofauti wa kibaolojia pia. Licha ya hayo bioanuwai inaweza kuwa sehemu ya suluhisho kwani tangu utofauti wa aina hizi uweopo utafanya ugumu wa vimelea kuenea kwa haraka.

Siku ya kuienzi Dunia Mama: Siku hii  kuienzi Mama Dunia inayokwenda sambamba na  Mwaka mzuri wa Bioanuwai, inajikita katika jukumu lake kama kiashiria cha afya ya Dunia. Kuna aina ya kukua mambo yanayotazama athari za kiafya, katika  upotezaji wa bianuwai na mabadiliko. Mabadiliko ya bianuawai yanaathiri utendaji wa mazingira na usumbufu mkubwa wa mifumo ya mazingira inaweza kusababisha mifumo ya ya bidhaa na huduma. Ushirikiano maalum kati ya afya na bioanuwai ni pamoja na athari ya lishe, utafiti wa afya au dawa za jadi, magonjwa mapya ya kuambukiza na mabadiliko ya ushawishi katika usambazaji wa mimea, vimelea, wanyama, na hata makazi ya watu, wengi wao wameaathiriwa na mabadiliko ya tabianchi.

Kwa mujibu wa shirika  la umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira aidha wanaandika kuwa, licha ya juhudi zinazoendelea, bioanuwai inazorota ulimwenguni kwa viwango visivyo kawaida katika historia ya wanadamu. Inakadiriwa kuwa karibu wanyama milioni moja na ya mimea sasa inatishiwa kutoweka. Pamoja na suta hii kubwa ya picha, na mazingira ya virusi vya corona kipaumbele  cha kwanza  kwa wote ni kuzuia kuenea kwa COVID-19, lakini pia si kwa muda mrefu, ni muhimu kukabiliana na upotezaji wa makazi na ule wa viumbe hai.

Tuko kwenye vita pamoja na Mama yetu Duniani na hili heri kujikumbusha  zaidi kuliko hapo zamani katika Siku hii ya Kimataifa ya  kuenzi Mama Dunia wanabainisha na kwamba kunahitajika mabadiliko ya uchumi endelevu ambao unafanya kazi kwa watu wote na sayari. Lazima katika siku hii kuhimiza maelewano na maumbile na Dunia. Siku ya kuienzi na kuithamini dunia ilianza kuadhimishwa kwa mara ya kwanza miaka 50 iliyopita.

21 April 2020, 14:58