Katika harakati za kuzuia kusambaa kwa virusi vya Corona, COVID-19, ni lazima nchi zichukue hatua za kuzuia mtu yeyote kukosa makazi kwa kuhakikisha fursa ya mahali pa kukaa kwa wale wasio na makazi Katika harakati za kuzuia kusambaa kwa virusi vya Corona, COVID-19, ni lazima nchi zichukue hatua za kuzuia mtu yeyote kukosa makazi kwa kuhakikisha fursa ya mahali pa kukaa kwa wale wasio na makazi 

Katika janga la Virusi Serikali zisaidie kutoa makazi kwa wasio kuwa nayo!

Makazi yamekuwa ni silaha ya kwanza katika vita dhidi ya virusi vya Corona,kwa maana hiyo serikali zihakikisha kuwapa mahali pa kukaa wale wasio kuwa na makazi.Nchi ni lazima zitoe msaada wa fedha kwa ajili ya kodi ya pango au kulipia mikopo ya nyumba,zisitishe hatua ya kuwafukuza watu kwa sababu ya malipo,zianzishe njia ya kupunguza kodi ya pango japo kwa wakati wa mlipuko pia kusitisha kwa muda gharama za malipo ya matumizi mengine kama maji,umeme na gesi.

Wakati huu ambapo serikali zikitegemea na kuwasii watu wabaki nyumbani ili kusaidia kukabiliana na kupunguza kusambaa kwa virusi vya Corona, COVID-19, ni lazima nchi zichukue hatua za kuzuia mtu yeyote kukosa makazi kwa  kuhakikisha fursa ya mahali pa kukaa kwa wale wasio na makazi. Wito huo umetolewa tarehe 18 Machi 2020 na mtaalam huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya makazi bora Leilani Farha ambaye ameongeza kusema kuwa “Makazi yamekuwa n diyo silaha iliyo mstari wa mbele katika vita dhidi ya virusi vya Corona. Nyumba kwa  hivi sasa imekuwa ni muhimili baina ya hali ya maisha au kifo".

Akiendelea kusisituza ameongeza kueleleza kwamba kuna mambo yanayompa wasiwasi mkubwa:“Nina hofu kubwa kuhusu makundi mawili ya watu, wale wanaoishi katika makazi ya dharura, wasio na makazi na makazi yasiyo rasmi na pili wale ambao wanakabiliwa na kupoteza ajira na hali mbaya ya kiuchumi hali ambayo itasababisha changamoto ya kulipa mikopo ya nyumba, kodi ya pango na kukabiliwa na kufukuzwa katika makazi yao.” Kwa mujibu wa mtaalam huyo takriban watu bilioni 1.8 duniani kote wanaishi bila makazi na kwenye makazi duni, na mara nyingi katika hali ya msongamano, huku wakikosa huduma za msingi kama maji na usafi na hivyo kuwafanya kuwa katika hatari ya kukabiliwa na virusi hivi vipya hasa kwa kuwa mara nyingi wanakabiliwa na changamoto nyingi za kiafya.

Kufuatana na hili amasema mtaalam huyu: “Nitazitaka nchi kuchukua hatua zaidi kuhakikisha haki ya makazi kwa wote ili kuwalinda na janga  hili la Corona. Kuna baadhi ya nchi wanachukua hatua nzuri ikiwemo kusitisha kuwafukuza watu wasiolipa kodi ya pango au kuchelewa kulipia mikopo ya nyumba hasa kule walikoathirika na virusi vya Corona, ambako majira ya baridi kali bado yanaendelea na kwa wale wanaoishi katika makazi yasiyo rasmi. Pia kuna wale wanaotoa huduma kama za maji safi na usafi kwa wasio na makazi tunaomba hili liendelee kwa wote.

Akiendelea kusisitiza zaidi  pia ameongeza kusema kuwa wakati hatua muhimu zinahitajika kukabiliana na hatari ya makundi haya ya watu  na kushughulikia kiwango cha maambukizi lazima  kuhakikisha ulinzi kwa wasio na makazi au wanaoishi katika makazi duni “nchi lazima zisitishe kesi zote za kuwafukuzia makwao watu, ziwape makazi ya muda na huduma za msingi wale waliathirika na virusi vya Corona na kuwatenga, kuhakikisha hatua za kudhibiti kama vile watu kutotembea hovyo hazisababishi adhabu kwa yeyote kutokana na hali ya makazi yake. Pia nchi zitoe fursa sawa ya upimaji na huduma za afya na pia kutoa nyumba kama inahitajika wakati wah aliya tahadhari na dharura ikiwemo kutumia nyumba zilizo wazi au kutelekezwa kwa ajili ya muda mfupi.”

Na kwa wale wanaokabiliwa na kupoteza ajira na kukabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi kutokana na mlipuko huu wa Corona mtaalm huyo ana wito  kuwa “ Nchi ni lazima zitoe msaada wa fedha kwa ajili ya kodi ya pango au kulipia mikopo ya nyumba, zisitishe hatua ya kuwafukuza watu kwa sababu ya malipo, zianzishe njia ya kupunguza kodi ya pango japo kwa wakati wa mlipuko na pia kusitisha kwa muda gharama za malipo ya matumizi mengine kama maji, umeme na gesi.

Hata hivyo amesema hadi sasa “Kuna hatua zimekwisha chukuliwa na fungu la fedha kutengwa ili kukabiliana na athari za kiuchumi zitakazosababishwa na Corona ikiwemo mdororo wa kiuchumi kama vile kupunguza kiwango cha riba. Kadhalika  amesema kuna hatari ya hatua hizo kutumika vibaya na kuitumia fursa za janga hili kutawala soko la nyumba bila kujali viwango vya haki za binadamu  kama ilivyofanyika wakati wa mdororo wa kiuchumi wa kimataifa mwaka 2008. Hivyo nchi lazima zizuie hulka hiyo ya taasisi na wawekezaji katika upande wa nyumba za makazi”. Hatimaye amesisitiza kuwa : “Kwa kuhakikisha fursa ya nyumba bora na usafi siyo tu nchi zitawalinda watu wake na kuokoa maisha ya wasiyo na makazi, bali pia zitasaidia kuilinda dunia dhidi ya COVID-19.

19 March 2020, 13:12