Tafuta

Vatican News
Madaktari wakiwa wanasaidia wagonjwa wa Corona nchini Iran Madaktari wakiwa wanasaidia wagonjwa wa Corona nchini Iran 

COVID-19:Shirika la Afya duniani limetuma timu ya wataalam nchini Iran!

Timu ya wataalamu wa shirika la afya duniani wamefika jijini Tehran kusadia nchi ya Iran.Timu hiyo itafanya kazi kwa karibu na mamlaka za afya na wadau wengine kutathimini juhudi zinazoendelea za hatua za kupambana na ugonjwa wa Corona(Covid-19),kuzuru vituo maalum vya afya,maabara na maeneo ya mipakani ya kuingia na baadaye kutoa muongozo wa kiufundi

Timu ya wataalam wa shirika la afya duniani WHO imewasili mjini Tehran tarehe 2 Machi 2020 ili kuisaidia nchi ya Iran katika juhudi zinazoendelea za kupambana na mlipuko wa virusi vya Corona (COVID-19) nchini humo. Timu hiyo itafanya kazi kwa karibu na mamlaka za afya na wadau wengine kutathimini juhudi zinazoendelea za hatua za kupambana na ugonjwa huo, kuzuru vituo maalum vya afya, maabara na maeneo ya mipakani ya kuingia na baadaye kuweza kutoa muongozo wa kiufundi.

Kwa ujumla lengo la ziara hiyo ni kubaini mwenendo wa maambukizi na hatari kwa umma, kutoa muongozo wa kuimarisha na kuongeza juhudi za kupambana na mlipuko unaoendelea, ikiwemo makubaliano ya hatua za kipaumbele za kudhibiti mlipuko na kutoa muongozo kuhusu kuimarisha udhibiti katika maeneo ambayo bado hayajaathirika na mlipuko huo. Hadi kufikia tarehe 2 Machi kulikuwa na  visa 1501 vya COVID-19 vilivyothibitishwa nchini Iran ikiwemo vifo 66. Kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya afya ya Iran watu 291 tayari wameruhusiwa kutoka hospitali baada ya kupona.

Visa vinavyotokana na historia ya kusafiri kwenda Iran vimeripotiwa kutoka Afghanistan, Canada, Lebanon, Pakistan, Kuwait, Bahrain, Iraq, Oman, Qatar na Emarati. Ndege iliyowabeba timu ya wataalam hao pia ilijumuisha madawa na vifaa tiba, ikiwemo vifaa vya kujikinga kuwasaidia zaidi ya wahudumu wa afya 15,000 pamoja na vifaa vya kutosha vya maabara ambavyo vinaweza kuwapima karibu watu 100,000. WHO imeishukuru serikali ya Emarati kwa kutoa ndege hiyo ambayo imeiwezesha WHO kupeleka timu na vifaa tiba nchini Iran.

Aidha hali ya wasiwasi imetanda barani Ulaya baada ya kurekodi visa vipya vya maambukizi ya Corona, ikiwa ni mara tisa zaidi ya China ambako ni kitovu cha mlipuko wa virusi hivyo. Kwa mujibu wa shirika la WHO, virusi hivyo vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 3,100 huku watu zaidi ya elfu 90 wakiambukizwa duniani kote. Kupungua kwa maambukizi mapya nchini China kumehusishwa na mikakati iliyowekwa na mamlaka nchini humo kudhibiti kusambaa kwa virusi hivyo ikiwemo kuzuia mikusanyiko ya watu na kuweka marufuku ya usafiri. Peng Xiaoxiang ambaye ni mkurugenzi wa hospitali ya muda ya Gymnasium amesema. “Tulitakiwa kujiandaa kwa mlipuko wa Corona lakini sasa tumesimamisha kwa muda oparesheni katika hospitali hii kwa sababu idadi ya wagonjwa imepungua. Hatutaifunga lakini iwapo huduma zetu zitahitajika, basi tuko tayari.”

Wakati maambukizi mapya yanapungua China, hali ni tofauti nchini Marekani kwani taifa hilo sasa linakabiliwa na janga kubwa la kusambaa kwa virusi hivyo. Tayari watu sita wamefariki dunia katika jimbo la Washington. Makamu wa Rais wa Marekani amesema yako matumaini kuwa tiba dhidi ya Corona huenda ikapatikana hivi karibuni. Akizungumzia mlipuko wa virusi vya Corona, Makamu wa Rais Mike Pence amesema yako matumaini kuwa huenda tiba dhidi ya virusi hivyo ikapatikana hivi karibuni. China imechukua hatua kali za kuweka karantini na kuzuwia usafiri kuzuwia kusaamba kwa virusi hiyo, hatua ambayo inaonekana kuzaa matunda.

Wakati Italia imezuia mizima yenye maambukizi watu wake kutoka nje wala kuingia yoyote, mataifa mengine yamejizuia kuwaweka watu wengi  karantini na badala yake wamejaribu kuwazuia mikusanyiko mikubwa, kuchelewesha matukio ya michezo na kupiga marufuku abiria kutoka mataifa yaliyoathirika zaidi. Korea Kusini, Iran na Italia ni mataifa ya karibuni ambayo yamekumbwa na mlipuko wa virusi vya Corona.

03 March 2020, 13:42