Tafuta

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema:Tuko katika vita na virusi vya Corona hivyo mitazamo bunifu ni lazima iende sanjari na asili ya janga hili na hatua tunazochukuliwa lazima ziendane na ukubwa wa janga hili. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema:Tuko katika vita na virusi vya Corona hivyo mitazamo bunifu ni lazima iende sanjari na asili ya janga hili na hatua tunazochukuliwa lazima ziendane na ukubwa wa janga hili. 

Mkutano wa G7 utafanyika kwa njia ya video!

Bwana Trump amefuta mkutano wa viongozi wa nchi saba tajiri duniani kinyume chake watazungumza kwa njia ya video kufuatia na mlipuko mbaya wa virusi vya corona.Na Katibu Mkuu wa umoja wa Mataifa anasema virusi vinaweza kudhibitiwa na lazima vidhibitiwe.Kufikia hatua hiyo ni wakati wa kuondokana na mkakati wa nchi binafsi na kuhamia katika mkakati wa kimataifa ili kukabiliana na janga hili ikiwepo kuzisaidia nchi ambazo hazijajiandaa kukabiliana na janga hili.

Rais wa Marekani  Bwana Donald Trump amefuta Mkutano wa viongozi wa mataifa saba tajiri duniani (G7) kinyume chake  wataweza kuzungumza kwa njia ya video kwa kutoa fursa kwa viongozi kushughulikia suala la mlipuko wa  maambukizi ya virusi vya corona (COVID-19) katika nchi zao. Mkutano huo uliokuwa unatarajiwa kuwakutanisha mataifa ya Canada, Ufaransa, Ujerumani, Japan, Italia, Uingereza na Marekani ambapo kwa mtazamo wa haraka ndiyo mataifa ambayo yanakabiliana na janga hili la kutisha duniani kwa kiasi kikubwa. Mkutano huo ulikuwa ufanyika mwezi Juni  mwaka huu katika jimbo la Marekani la Maryland.

Aidha Bwana Trump pia ataweza kukutana na viongozi wa mataifa hayo saba kwa njia ya video kunako mwezi Aprili na Mei baada ya viongozi hao kufanya mkutano kuhusu mlipuko huu wa virusi vya corona wiki hii. Kufuatia na hali halisi inavyoendelea, serikali ya Trump inaamini kuwa suala la maambukizi ya virusi vya corona itaendelea kuwa na athari ulimwenguni hadi wakati wa majira ya joto. Hata hivyo wakati hofu ikiendelea kutanda ulimwenguni kote  kufuatia nakusambaa kwa mlipuko wa virusi vya Corona, (COVID-19) Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Antonio Guterres amesema “sasa kuliko wakati mwingine wowote tunahitaji mshikamano, tumaini na utashi wa kisiasa ili kukabiliana na janga hili kwa pamoja.”.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kwa njia ya mtandao mjini New York Marekani tarehe 19 Machi 2020  Bwana Guterres amesema tofauti na majanga mengine makubwa ya kimataifa ya kiafya katika miaka 75 ya historia ya Umoja wa Mataifa “janga la virusi vya corona linasambaza kwa haraka  kwa binadamu na kuathiri uchumi wa dunia. Familia yetu ya kibinadamu inakabiliwa na shinikizo na ukuta wa kijamii umepasuka, watu wanateseka, wanaumwa na kuogopa.” Ameongeza kusema, kwa kuwa ngazi ya taifa haiwezi peke yake kukabiliana na changamoto hii ya kiwango cha kimataifa inahitaji “sera za pamoja na bunifu kuanzia kwenye mataifa yanayoongoza kiuchumi duniani.”

Bwana Guterres amesema kwamba anatarajia kushiriki mkutano wa dharura wa viongozi wa nchi tajiri 20 au G-20 utakaofanyika wiki ijayo kwa lengo la kuchukua hatua za kukabiliana na changamoto ya janga hili. Kwa kusisitiza zaidi amesema “ujumbe wangu huu uko bayana, tuko katika hali ngumu na sheria zetu za kawaida hazifanyi kazi tena. Tuko katika vita na virusi vya Corona hivyo mitazamo bunifu ni lazima iende sanjari na asili ya janga hili na hatua tunazochukuliwa lazima ziendane na ukubwa wa janga hili.” Katibu Mkuu ameongeza kuwa ingawa COVID-19 inaua watu na kuathiri uchumi kwa kuudhibiti vyema janga hili  tunaweza kujijenga upya kuelekea katika njia ambayo ni endelevu na jumuishi. “Natoa wito kwa viongozi wote wa dunia kuwa pamoja na kuchukua hatua za haraka na za pamoja  ili kukabiliana na hali hii ya kimataifa.”

Bwana Guterres pia  amesema kushughulikia dharura ya kiafya ni kipaumbele chake cha kwanza na anachagiza juhudi zaidi ambazo hazina ubaguzi katika  kusaidia kwenye upimaji, kuwasaidia wahudumu wa afya na kuhakikisha vifaa vya kutosha. “Imethibitika kwamba virusi hivyo vinaweza kudhibitiwa, na ni lazima vidhibitiwe, ni wakati wa kuondokana na mkakati wa nchi mojamoja na kuhamia katika mkakati wa kimataifa katika kukabiliana na janga hili ikiwepo kuzisaidia hata nchi ambazo hazijajiandaa vyema kukabiliana na janga hili”. Ameongeza kuwa “mshikamano wa kimataifa siyo tu ni muhimu kidhamira, lakini pia ni suala lenye maslahi kwa kila mtu”, kwa maana hiyo amesisitixa na kuzitaka serikali ili kutimiza maombi yote ya Shirika la Afya ulimwengubu (WHO) na kwamba sisi sote tutakuwa imara tu kwa pamoja wakati mifumo yetu ya afya ikiwa imezidiwa.

Kama kipaumbele chache cha pili Bwana Guterres ametaja athari za kijamii na kiuchumi na jinsi gani ya kujikwamua  nayo na  amegusia ripoti mpya ya shirika la kazi duniani  (ILO) ambao linakaridia kwamba wafanyakazi wanaweza kupoteza dola trilioni 3.4 za mapato ifikapo mwisho wa mwaka. Lakini amesema dunia haishuhudii kudorora sana katika mnyororo wa usambazaji na mahitaji ambapo ni mshangao kwa jamii. Bwana Gusterres amebainisha kuwa: “La msingi zaidi tunapaswa kujikita na watu, wale wasiojiweza , wenye kipato kidogo, wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo. Hii inaamanisha kusaidia mshahara, bima, hifadhi ya jamii, kuzuia kufilisika na kupoteza ajira.” Amefafanua kwamba “kujikwamua kusije kupitia mgogo wa maskini na hatuwezi kuunda kundi la maikini wapya hivyo ni lazima tuwasaidie walioko katika sekta zisizorasmi na nchi ambazo hazina uwezo wa kukabiliana na janga hili.” Akitoa ombi la msaada wa kifedha kimataifa ameainisha kwamba shirika la fedha duniani IMF, Benki ya Dunia na taasisi zingine za kimataifa za kifedha watakuwa na jukumu muhimu.

Bwana Guterres amechagiza kuondoa vikwazo vya kibiashara na kuanzisha upya mnyororo wa usambazaji. Pia ameelezea athari suala la wanawake na kusema kwamba “wanabeba mzigo mkubwa nyumbani, katika uchumi na kwa watoto ambao amesema zaidi ya milioni 800 hawako madarasani  hivi sasa na wengi wao wakitegemea shule kwa ajili ya kupata mlo.” Katibu mkuu ameongeza kwamba wakati maisha ya watu yakiathiriwa, kutengwa na kupinduliwa chini juu ni lazima kuzuia janga hili lisigeuke zahanati ya afya ya akili. Kuna haja ya kuhakikisha program za msaada kwa wasiojiweza na mahitaji ya kibinadamu yasipuuzwe. Hatimaye Katibu mkuu Bwana Guterres ni kwamba tuna jukumu la kujikwamua vyema katika janga hili. “Ni lazima tuhakikishe kwamba tumejifunza na kwamba janga hili linatupa fursa ya maandalizi ya mifumo ya afya na kwamba uwekezaji katika karne ya 21 kwenye huduma za umma ni muhimu” Akigusia ajenda ya maendeleo endelevu ya 2030 na mkataba wa mabadiliko ya tabianchi wa Paris amesema “ni lazima tutimize ahadi yetu kwa watu na sayari dunia.”

20 March 2020, 10:40