Tafuta

Dharura ya koronavirus hata nchini Itala Kaskazini Dharura ya koronavirus hata nchini Itala Kaskazini  

Korona COVID-19:Sasa ni dharura ulimwenguni:vifo viwili nchini Italia!

Wakati maambuziki ya virusi vya korona COVID -19 inazidi kusambaa kwa kasi,Shirika la la Afya duniani limehimiza jumuiya ya kimataifa kuwekeza katika kutafuta sulihisho la Afya na zaidi katika kuthibiti mlipuko huo.Nchini Italia hadi sasa wamekufa watu wasili na kesi za maambukizi ni karibia 29. Wasiwasi mkubwa umeoneshwa hata Rais wa Baraza la Maaskofu Italia.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Wakati idadi ya maambukizi ya virusi vya Korona COVID-19 yanaendelea kuongezeka kwa kasi, Shirika la afya duniani, (WHO) limehimiza jumuiya ya kimataifa kuwekeza katika ili kupata suluhisho la afya kwa maana inaweza kusaidia katika kudhibiti mlipuko wa ugonjwa huo sasa na wakati huo huo kusaidia katika kujiandaa na dharura hii katika jamii kwa siku za mbeleni. Kwa mjibu ngazi za kimataifa, watu walioambukizwa ni zaidi 76, 000 Nchini China na zaidi ya kesi mpya zimezidi kuelendelea kuongezeka.

Korea Kusini, Japan na Iran

Kwa ujumla taarifa zinasema hadi sasa wamefikia vifo karibia 2345. Na kila kuchao hali ya maambuzi inazidi kuongezeka nchini Korea ya Kusini na kusababisha dharura mpya mahali ambako kesi zilizothibitishwa hadi sasa ni 204. Na maambukizi yameongezeka ya watu 34 waamerika. Hata hivyo dhararua pia  nchini Japan kufuatia na Meli ya Diamond Princess kwa wasafiri waliokuwamo na ambao licha ya kuwekwa karantini ndani humo wasiwasi ni mkubwa wa maambukizi ya wasafiri hao. Iran baada ya vifo vya watu wanne wameonesha pia kuambukiza kwa watu wengine watatu.

Nchini Italia

Hadi sasa wamebainisha vifo viwili. Ni kuhusu mwanamme mmoja mwenye umri wa miaka 78 na mwanamke wa  Lombardia. Hadi sasa kesi za maambukizi ni 29 za watu wa Italia wanaoonesha dalili za coronavirusi. Wasi wasi mkubwa pia umeweza kubainishwa na Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Italia Kardinali Gualtiero Bassetti ambaye yuko kwenye Mkutano “kuhusu Mediteranea mpaka wa Amani. Yeye anasema “tunaona kweli kufuata malekezo na kanuni za usafiri. Itakuwapo sadaka ya kukabiliana nayo. Lakini kama ni kwa ajili ya wema wa afya na wema wa wazalendo wetu sadaka itaweza kukabiliana nayo”.

Hofu ya maambuzi kufuatia na kusafiri kwa watu kwa mujibu wa Who

Kwa mujibu wa Shirika la Afya duniani Mkurugenzi Mkuu Dk. Tedros Adhanom Ghebreyesus anasema ni dharurua kubwa kwa namna ya virusi vinavyoendelea katika mfumo wa Nchi wa kiafya wenye kuathirika. Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dk. Tedros Adhanom Ghebreyesus ameonesha hofu yake  ya sasa juu ya kuenea kwa virusi vya Corona, COVID-19 hasa zaidi kutokuwa na taarifa za wazi kuhusu uhusiano wa kuenea kwa virusi hivyo, kama vile historia ya mtu kusafiri China au kuwa na mawasiliano na mtu aliyethibitishwa kuambukizwa virusi hivyo. Amezungumza hayo na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi tarehe 21 Februari 2020 na ambapo anasema inapoelezwa kuwa taifa lenye wagonjwa wengi zaidi wa virusi vya Corona baada ya China ni Korea Kusini. Dk. Tedros amesema zaidi ya meli ya kifahari ya abiria ya Diamond Princess iliyopita Korea Kusini, taifa hilo sasa lina idadi kubwa ya wagonjwa kando ya China na hivyo wanashirikiana na serikali ya taifa hilo kuelewa mzunguko wa maambukizi uliosababisha ongezeko la maambukizi. Tuna wasiwasi pia juu ya ongezeko la wagonjwa wa Corona nchini Iran ambako sasa kuna wagonjwa 18 huku wengine wanne wamefariki dunia katika siku mbili tu zilizopita.

Lebanon 

Kuhusu mgonjwa aliyebainika Lebanon, afisa wa WHO, Jaouad Mahjour amesema mgonjwa huyo aligundulika kwenye uwanja wa ndege kwa sababu walikuwa wanachunguza wasafiri kutoka Iran iwapo wana dalili za virusi vya Corona na ndipo mgonjwa akagundulika. Nayo ofisi ya Shirika la Afya WHO mjini Cairo, Misri hivi sasa ina mawasiliano na Iran na Lebanon kutathmini hali ilivvyo ili kubaini aina ya msaada unaohitajika iwapo nchi hizo zitahitaji. Kwa  mantiki hiyo Dk. Tedros amesema wanachoamini kuna fursa ya kuchukua hatua, lakini fursa hiyo inazidi kuwa finyu na ndiyo maana, “tunatoa wito kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua”. Akithibitisha taarifa yao kuhusu Jumuiya nzima ya Kimataifa ili kuchukua hatua  haraka, ikiwemo kutoa fedha ambazo sasa hazipo.

22 February 2020, 15:08