Ni zaidi ya watu elfu moja wameathirika na virusi vya xorna nchini China. Ni zaidi ya watu elfu moja wameathirika na virusi vya xorna nchini China. 

Papa amesali kwa ajili ya waathirika wa virusi vya corona nchini China!

Mara baada ya tafakari ya Katekesi ya kwa mahujaji na waamini wote amelekeza sala kwa ajili ya ndugu wa China ambao wanateseka na ugonjwa mbaya sana.Vifo kwa ajili ya Covid-19 vimefikia 1113 kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani,na vyote vikiiitazama China,Hong-Kong na mmoja huko Ufilippini.

Na Sr. Angela Rwezaula Vatican

Tarehe 12 Februari 2020 mara baada ya Katekesi ya Papa Francisko amewakumbuka na kusali kwa ajili ya waathirika wa virusi vya Covid-19 nchini China ambapo amabomba waweze kupona kwa haraka. Hata hivyo vifo vimefikia 1113 nchini China na waathirika wengine huko, Hong-Kong  na kifo kimoja huko Ufilippini, vile vile kuna kesi nyingine mpya za maambukizi yanayoendelea.

Shirika la afya duniani WHO limeendesha jukwaa la utafiti na ubunifu ili kuchukua hatua za kimataifa kushughulikia mlipuko wa virusi vya corona yaani COVID-2019 ambapo hadi sasa watu 42,000 wameambukizwa na tayari vifo vimefikia zaidi ya elfu moja. Jukwaa hilo la siku mbili tarehe 11-12 Februari 2020 limefanyika mjini Geniva, Uswisi, kwa kuandaliwa na ushirikiano wa muungano wa taasisi ya GloPID-R ambao ni wafadhili wa tafiti kuhusu utayari wa magonjwa ya kuambukiza.

Katika maelezo ya hotuba yake ya ufunguzi Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya duniani (WHO) Dk Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema,“Ni vigumu kuamini kuwa miezi miwili iliyopita, virusi hivi ambavyo vimeteka vyombo vya habari, masoko ya uchumi na viongozi wa kisiasa, tulikuwa hatufifahamu kabisa.”  Aidha amesema kuwa: “Huu siyo mkutano kuhusu siasa na pesa. Huu ni mkutano kuhusu sayansi. Tunahitaji uelewa wa pamoja, mtazamo na uzoefu, kujibu maswali ambayo hatuna majibu yake, na kutambua maaswali ambayo tunaweza hata tusitambue kuwa tunahitaji kuuliza.” Na kwa kuhitimisha hotuba yake Dk Tedros amesema: “Tunatumai kuwa moja ya matokeo ya mkutano huu itakuwa namna iliyokubaliwa kufanya utafiti ambao watafiti na wafadhili wataungana. Jambo la msingi ni mshikamano, mshikamano, mshikamano”.

Jukwaa hilo litawaleta pamoja wadau muhimu wakiwemo wanasayansi nguli pamoja na taasisi zaa afya ya jamii, mawaziri wa afya na wafadhili wa tafiti wanaofuatilia ugonjwaa wa corona, afya ya Wanyama na afya ya umma pamoja na maendeleo ya chanjo, tiba na utambuzi wa magonjwa, miongoni mwa uvumbuzi mwingine. Washiriki wanajadili maeneo kadhaa ya utafiti ikiwemo kutambua chanzo cha virusi hivi, pia kupeana taarifa za sampuli za kibailojia na mienendo ya viasili nasaba au maumbile.

Wataalamu wameanzia kwenye utafiti uliopo kuhusu milipuko mingine kama ya ugonjwa wa SARS na MERS na kuona mapungufu na vipaumbele vya utafiti ili kusongesha taarifa za kisayansi na matokeo ya kitabibu ambayo yanahitajika sana kupunguza athari za mlipuko wa sasa wa corona. Hata hivyo hitimisho la Jukwaa hilo ni kutoa ajenda ya utafiti wa kimataifa kwa ajili ya  virusi vya corona, kuweka vipaumbele na mfumo ambao unaweza kuongoza ni miradi gani inatakiwa kutekelezwa mwanzo kabla ya mingine.

12 February 2020, 16:49