Tafuta

Vatican News
Katika maadhimisho Siku ya 22 ya lugha ya mama duniani  lengo ni kuwa na  lugha bila mipaka wakimulika lugha zote pamoja na lugha mama na mchango wake katika kuleta umoja. Katika maadhimisho Siku ya 22 ya lugha ya mama duniani lengo ni kuwa na lugha bila mipaka wakimulika lugha zote pamoja na lugha mama na mchango wake katika kuleta umoja. 

Moja ya lugha iliyoenea katika mataifa ya Afrika ni Kiswahili!

Lugha mama zinasaidia kuweka mazungumzo ya pamoja na kuwawezesha kuchanua na kuchangamka katika muktadha mmoja,lugha mama zinachochoea utangamano wa kijamii,ubunifu na kukuza fikra.Ni kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu,Sayansi na Utamaduni(UNESCO)wakati wa kilele cha Siku ya Kimataifa ya Lugha mama inayoadhimishwa kila tarehe 27 Februari ya kila mwaka.

Tarehe 27 Februari ni siku ya kimataifa ya lugha mama, ambalo Umoja wa  Mataifa unahamasisha lugha ya Kiswahili kwa kuthibitisha  kuwa ni miongoni mwa lugha inayozidi kupanuka kimatumizi duniani na kusaidia kueneza utamaduni wake. Katika ujumbe wake kwenye fursa yasiku hii  Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni,  UNESCO  Bi Audrey Azoulay, amesema, “ikiwa na wazungumzaji kati ya milioni 120 hadi 150, lugha ya Kiswahili ni moja ya lugha zinazoshamiri kuvuka mipaka ya kule inamozungumzwa. Lugha ya Kiswahili ina maneno kutoka Kusini mwa Afrika, uarabuni, Ulaya na India.”

Bi. Azoulay amesema ikiwa ni lugha ya taifa na rasmi kwa Tanzania na pia lugha ya taifa Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Kiswahili pia kinazungumzwa Burundi,  kaskazini mwa Msumbiji, Uganda, Rwanda, kusini mwa Somalia na kwa kiasi fulani Malawi, Sudan Kusini na Zambia. Mkurugenzi Mkuu huyo wa UNESCO amesema ni kwa kuzingatia athari chanya za lugha ndiyo maana katika maadhimisho ya 22 ya lugha ya mama duniani hii leo lengo ni lugha bila mipaka wakimulika lugha zote pamoja na lugha mama na mchango wake katika kuleta umoja. “Kwa kuleta wazungumza pamoja, na kuwawezesha kuchanua na kuchangamka katika muktadha mmoja, lugha mama zinachochoea utangamano wa kijamii, ubunifu na kukuza fikra.”

Halikadhalika Bi Azoulay amesema lugha hizo pia zinaimarisha utofauti wa kitamaduni na kuwa chombo cha kujenga amani na zaidi ya hapo, “lugha mama ni muhimu katika jitihada zetu za kufanikisha elimu kwa wote. Ni kwamba tafiti za UNESCO zimegundua kuwa mtu kusoma kwa lugha ambayo si ya kwake kunaingiliana na uwezo wake wa kujifunza na kuongeza ukosefu wa usawa.” Hata hivyo amesema makadirio ya hivi karibuni yanaonyesha kuwa asilimia 40 ya wakazi wa dunia wanajikuta katika hali hiyo. “Mfumo wa elimu wa kutumia lugha mbili au lugha zaidi ya mbili unaopatia msisitizo lugha ya mama ya mwanafunzi, inachochoea siyo tu kujifunza bali pia huchangia kuelewa na majadiliano baina ya watu,” amesema Mkurugenzi Mkuu huyo wa UNESCO.

27 February 2020, 12:31