Wakati wa sala ya Malaika wa Bwana Papa amegusia kuhusu mwaka 2020 kwa ngazi ya kimataifa kama wa wauguzi na wakunga na kwamba wanafanya kazi zaidi ya taaluma zote! Wakati wa sala ya Malaika wa Bwana Papa amegusia kuhusu mwaka 2020 kwa ngazi ya kimataifa kama wa wauguzi na wakunga na kwamba wanafanya kazi zaidi ya taaluma zote! 

Papa:wauguzi na wakunga wanafanya kazi zaidi ya taaluma zote!

Papa Francisko mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana Tarehe 19 Januari 2020 kwa mahujaji na waamini waliokusanyika katika uwanja wa Mtakatifu Petro Vatican,kati ya mambo mengi aliyosemani kukumbusha mwaka 2020 wa Wauguzi na Wakunga uliotolewa kwa ngazi ya kimataifa.Wauguzi na wakunga wanatimiza kazi ya thamani.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Papa Francisko ameonesha kupendezwa na chaguo la mwaka 2020 kuwa mwaka kwa ngazi ya kimataia kama ‘Mwaka wa wauguzi na wakunga’.  Papa amesema: “Ninafurahi kukumbuka kuwa 2020 kwa ngazi ya kimataifa umechaguliwa kama mwaka wa wauguzi na wakunga”. Wauguzi na wakunga ni wahudumu wa afya wengi ambao labda wanafanya  kazi muhimu sana kati  ya taaluma zote. Tuwaombeee wote ambao wako karibu na wagonja zaidi ili waweza kutenda kazi yao vema yenye thamani kubwa”.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya duniani wakunga milioni 9 bado wanahitajika

Dunia itahitaji ongezeko la wauguzi na wakunga milioni 9 ili kutimiza ahadi ya kutoa fursa ya huduma za afya kwa wote ifikapo mwaka 2030. Haya yamethibitishwa na Shirika  Afya ulimwenguni WHO. Kwa mantiki hiyo WHO na wadau watautumia mwaka huu wa 2020 kupigia upatu uwekezaji katika wahudumu hao muhimu wa afya. Alihimiza  hilo mkurugenzi mkuu wa WHO Dk. Tedross Adhamon Ghebreyesus na kusema  “wauguzi na wakunga ni uti wa mgongo wa kila mfumo wa afya na mwaka 2020 tunatoa wito kwa nchi zote kuwekeza kwa wauguzi na wakunga kama sehemu ya ahadi ya huduma za afya kwa wote.” Dk Teodros alisema kuwa mwaka 2020 ni “Mwaka wa wauguzi na wakunga” na ni maadhimisho ya miaka milenia tangu kuzaliwa kwa Florence Nightngale muasisi wa uuguzi.

Mbali na kutoa huduma yao wanaokoa maisha ya watu katika majanga na dharura za kibinadamu

Mwaka huu ni wa kusherehekea wanataaluma ambao wanatoa huduma mbalimbali muhimu kwa watu kila mahali. Mbali ya kuzuia, kubaini, kupima magonjwa na kutoa huduma ya kitaalam wakati wa kujifungua wauguzi na wakunga pia wanaokoa Maisha ya watu katika majanga na dharura za kibinadamu na vita. Hivi sasa  duniani kote kuna wauguzi milioni 22 na wakunga milioni 2 wakiwa ni nusu ya wafanyakazi wote wa huduma za afya kwa mujibu wa  Shirika la Afya duniani (WHO). Hata hivyo shirika hilo limesema dunia inahitaji wahudumu wafanya kazi  milioni 18 zaidi na takribani nusu yao ni wauguzi na wakunga ili kuweza kutimiza lengo la huduma za afya kwa wote kabla ya kumalizika muongo huu kwenda sanjari na ahadi iliyowekwa na viongoziwa dunia kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa mwezi Septemba mwaka 2019.

Maeneo muhimu ya uwekezaji ni kuajiri wakunga na wauguzi wenye taaluma

Kwa mwaka 2020, Shirika la Afya ulimwenguni  litajikita katika  hatua za kuhakikisha kwamba wauguzi na wakunga wanaweza kufanya kazi kufikia kilele cha uwezo wao. Shirila la Afya WHO linasema maeneo ambayo ni muhimu kwa uwekezaji ni pamoja na kuajiri wauguzi na wakunga wenye utaalam, kuwafanya wauguzi na wakunga kuwa kitovu cha huduma za afya za msingi na kuwasaidia katika kuchagiza afya bora na kuzuia magonjwa.

19 January 2020, 14:07