Tafuta

Vatican News
Waziri Mkuu wa china Li Keqiang akiwa amejifunika kujilinda wakati akizungumza na madaktari alipotembelea hospitali ya Jinyintan wanapotibiwa wagonjwa wa virus vya corona Waziri Mkuu wa china Li Keqiang akiwa amejifunika kujilinda wakati akizungumza na madaktari alipotembelea hospitali ya Jinyintan wanapotibiwa wagonjwa wa virus vya corona 

Mlipuko wa virus unazidi kuenea zaidi ya mipaka ya China!

Harakati na uthibiti vinafanywa kitaifa na kimataifa ili kuendelea kupambana na mlipuko wa virusi vya Corona, na wakati huo China ihairisha kufanya siku kuu yake kubwa kabisa ya kitaifa ili kuendelea kupata muda wa kupambana na mlipuko wa virusi vya Corona.Waziri Mkuu wa china Li Keqiang ametembelea na kuzungumza na madaktari wa hospitali ya Jinyintan wanapotibiwa wagonjwa wa virus vya corona

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana pia  ameonesha kuwa  ukaribu nawagonjwa kwa sababu ya virusi ambavyo vimesambaa nchini China.” Anawaombea marehemu wapokelewe kwa Amani na faraja kwa familia na wale wote wanaofanya jitihada za Jumuiya ya nchi ya China ambao wanaendelea kupambana na mlipuko huo”.

Hata hivyo China imeweka mbele zaidi siku kuu yake kubwa kabisa ya kitaifa ili kuendelea kupata muda wa kupambana na mlipuko wa virusi vya Corona, wakati idadi ya vifo ikiongezeka hadi watu 80 licha ya hatua za kiwango kisicho cha kawaida za kuwafungia watu kwenye miji yao na kuzuia usafiri.

Waziri Mkuu Li Keqiang alitembelea mkoa wa Hubei ambao ndio chimbuko la kirusi hicho, ili kuongoza juhudi za kukabiliana na Corona katika mji wa Wuhan ambao una watu milioni 11. Vifo 24 vimeripotiwa katika mkoa wa Hubei, huku idadi ya watu walioambukizwa ikizidi kupanda hadi 2,700 nchini humo. Hata ugonjwa huo unaripotiwa kusambaa katika nchi kadhaa, Mkuu wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) Dk Tedros Adhanom Ghebreyesus ameelekea Beijing kukutana na maafisa wa serikali kuhusu mzozo huo wa kiafya. Vile vile matukio ya ugonjwa huo yameripotiwa hata Ufaransa, Marekani na Canada, huku nchi nyingine za Asia pia zikigundua virusi hivyo.

27 January 2020, 15:22