Tafuta

Vatican News
Watu zaidi ya 41 wamefariki kufuatia na mvua kubwa iliyonyesha nchini Angola kwa wiki  hii Watu zaidi ya 41 wamefariki kufuatia na mvua kubwa iliyonyesha nchini Angola kwa wiki hii  (AFP or licensors)

Angola:watu 41 wamefariki dunia kufuatia na mvua kubwa!

Kwa siku chache za mfululizo wa mvua kubwa imesababisha watu 41 nchini Angola kufariki dunia amabo maeneo mengi nchini humo yamefurika maji kuanzia mwanzoni mwa wiki hii.Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi anathibitisha janga hili kuharibu makazi na nyumba kujaa maji, kuharibu miundombinu, barabara,madaraja na njia za mawasiliano.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Hali mbaya ya hewa kuanzia saa sita usiku hadi saa 10 jioni siku ya Jumatatu imesababisha vifo vya jumla ya watu 41 kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya ndani Bwana Eugenio Laborinho katika mkutano na vyombo vya habari na wanaandishi katika mji mkuu Luanda nchini Angola. Karibia watu 12,000 wamekumbwa na mvua hizi kali ambazo zimesababisha kujaa kwa mito na kuharibu miundombinu ya barabara njia za mawasiliano na  makazi kwa mujibu wa Waziri wa mambo ya ndani.

Kwa namna ya pekee mvua imeharibu nyumba 378 na makanisa 12 na kusababisha madhara makubwa ya zaidi ya nyumba 2,000 kujaa maji na uharibifu wa madaraja 12 kati ya 18 yaliyoko katika wilaya za nchi ya Angola. Hata hivyo pia mvua hizi kubwa zimesababisha kukatika kwa umeme na njia za mawasiliano mawasiliano. Wahusika wamesema kuwa mvua hizi zimenyesha mara baada ya ukame mkubwa sana nchini Angola kaskazini na kusababisha vivyo vya zaidi ya wanyama 30,000.

Hata hivyo katika mji wa Brazzaville hali kama hiyo imejitokeza, na katika  mikoa mbalimbali ya Congo DRC. Kwa mujibu wa taarifa inathibitisha kwamba, watoto 3 wamefariki dunia kufuatia na kuanguka kwa nyumba iliyosababishwa na mvua kubwa na wakati huohuo Mwezi Novemba 2019 huko Kishansa, tukio la mvua kali lilisababisha vifo vya watu karibia hamsini.

Aidha Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini China, limetangaza tarehe 9 Januari 2020 kuwa mnamo tarehe 12 mwezi Desemba mwaka jana 2019, lilitia saini makubaliano ya msaada wa dola milioni mbili na Shirika la maendeleo la China, CIDCA ili kuwasaidia watu walioathirika na kimbunga Idai nchini Zimbabwe. Mchango huo unatoka katika mfuko wa Ushirikiano wa Kusini wa Serikali ya China, SSCAF.

Kimbunga Idai ni janga baya zaidi lililoasili kusini mwa Afrika katika takribani miongo miwili. Na kimbunga hicho kiliipiga Zimbabwe tarehe 15 mwezi Machi 2019 kikasababisha uharibifu mkubwa wa makazi na maisha na kuwaathiri watu 270,000 wakiwemo watoto 129,600 walioachwa katika mahitaji ya msaada wa kuokoa maisha.

Naye Mwakilishi wa UNICEF nchini China, Cynthia McCaffrey amesema, “mchango wa Serikali ya China utaisaidia UNICEF kuweza kusaidia katika dharura nyingine ya kibinadamu. Tutafanya kazi pamoja kufikia watoto walioathirika pamoja na familia zao, tukiwa na maji, vifaa vya kujisafi, afya, lishe na huduma za ulinzi wa jamii.” Mapema mwaka huu, UNICEF na Serikali ya China walishirikiana chini ya mpango wa SSCAF kutoa msaada wa kibinadamu kwa watu walioathirika na kimbunga nchini Msumbuji na Malawi ambako inakadiriwa watu milioni mbili wako katika uhitaji mkubwa wa misaada ya kibinadamu wakiwemo watoto milioni moja.

10 January 2020, 10:26