Kenya,Musumbiji na Niger wamezuia milipuko ya ugonjwa wa polio ambayo ilishuhudiwa nyakati tofauti katika kipindi cha miezi 24 iliyopita kwa mujibu wq shirika la Afya duniani WHO Kenya,Musumbiji na Niger wamezuia milipuko ya ugonjwa wa polio ambayo ilishuhudiwa nyakati tofauti katika kipindi cha miezi 24 iliyopita kwa mujibu wq shirika la Afya duniani WHO 

WHO:Nchi tatu za Afrika zazuia milipuko ya ugonjwa wa polio!

Kwa mujibu taarifa kutoka shirika la afya duniani WHO lililotangzwa tarehe 23 Desemba 2019 ni kwamba Kenya,Musumbiji na Niger wamezuia milipuko ya ugonjwa wa polio ambayo ilishuhudiwa nyakati tofauti katika kipindi cha miezi 24 iliyopita na kuchangia nchi hizo kutangazwa kuwa zisizokuwa na ugonjwa wa polio.Visa vya virusi vya polio vinavyotokana na chanjo ni vichache lakini huwaathiri ambao hawajachanjwa na waliopata chanjo kidogo.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya duniani WHO katika taarifa yao iliyotolewa Juamatau 23 Desemba 2019 inasema kuwa Kenya, Musumbiji na Niger wamezuia milipuko ya ugonjwa wa polio ambayo ilishuhudiwa nyakati tofauti katika kipindi cha miezi 24 iliyopita na kuchangia nchi hizo kutangazwa kuwa zisizokuwa na ugonjwa wa polio. Kwa mujibu wa shirika hili wanabainisha ugonjwa huo wa polio utokanao kusambaa kwa kinyesi cha waliopatiwa chanjo kwenda kwa wasio na ikinga uligunduliwa katika nchi tatu mwaka 2018 na mapema mwaka 2019 na uliwaathiri  jumala ya watoto 14.

Kumaliza kwa milipuko katika nchi hizi tatu ni uthibitisho kuwa shughuli za kupambana na polio na matumizi ya chanjo ya hali ya juu inaweza kuzima milipuko iliyobaki eneo hilo. Hayo yamesemwa na Dk. Modjirom Ndoutabe mratibu wa kundi la Shirika la Afya duniani (WHO) la kupambana na polio katika eneo la Afrika.

Visa vya virusi vya polio vinavyotokana na chanjo ni vichache lakini huwaathiri watato ambao hawajachanjwa na waliopata chanjo kidogo. Wakati watoto wanapochanjwa, chanjo hiyo hubaki kwenye matumbo yao kwa kipindi kifupi kuwapa kinga wanayohitajia na kisha hutoka kwa njia ya haja kubwa ambapo inaweza kubaki katika mazingira. Ikiwa utoaji chanjo katika jamii na usafi unabaki kuwa duni virusi vilivyo katika mazingira vinaweza kuwaambukiza watu wasiojua. Kumaliza milipuko huo huduma kwenye nchi zilizoathirika, makundi ya uchunguzi na mahabara ni lazima yathitbitishe kuwa hakuna maambukizi ya polio yanayotambuliwa kutoka kwa sampuli zinazokusanywa kutoka kwa watoto waliopooza kwa kipindi cha karibu miezi tisa.

Nchi ambazo bado zinashushua milipuko ya ugonjwa wa polio ni pomoja na Angola, Benin, Cameroon, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Chad, Côte d'Ivoire, Jamhuri ya Demokrasia ya Congo, Ethiopia, Ghana, Nigeria, Togo na Zambia. Kati ya masuala yanayochangia kushuhudiwa milipuko hiyo ni udhaifu katika utoaji chanjo, watu kukataa chanjo, vigumu kuyafikia maeneo mengine, kampeni chache za utoaji chanjo ambazo hufanya vigumu kuwafikia watoto.

 

 

23 December 2019, 16:36