Tafuta

Mshikamano wa dhati kati ya wadau mbali mbali dhidi ya maambukizi mapya ni muhimu sana kwa wakati huu ili kufikia malengo ya maendeleo endelevu ifikapo mwaka 2030. Mshikamano wa dhati kati ya wadau mbali mbali dhidi ya maambukizi mapya ni muhimu sana kwa wakati huu ili kufikia malengo ya maendeleo endelevu ifikapo mwaka 2030. 

Siku ya Ukimwi Duniani Kwa Mwaka 2019: Mshikamano!

Kuna zaidi ya watu milioni 30 ambao wamefariki dunia kutokana na Ukimwi. Katika mapambano dhidi ya maambulizi mapya ya ugonjwa wa Ukimwi, Baraza la Makanisa Ulimwenguni linasema, asiwepo mtu anayebakizwa nyuma. Zaidi ya watu milioni 40 wanaishi na Virusi vya Ukimwi na kati yao kuna wagonjwa milioni 25 ambao wanapewa dawa za kurefusha maisha; idadi bado ni ndogo.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Siku ya Ukimwi Duniani ilianzishwa na Umoja wa Mataifa kunako mwaka 1988 ili kukabiliana na athari kubwa zilizokuwa zinasababishwa na ugonjwa huu usiokuwa na tiba wala chanjo. Ni ugonjwa ambao haubagui wala hauchagui. Baraza la Makanisa Ulimwengu linasema, Siku ya Ukimwi Duniani inayoadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe 1 Desemba ni sehemu ya kampeni inayoendeshwa na Jumuiya ya Kimataifa sanjari na Siku ya Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Wasichana Duniani yaliyoadhimishwa hapo tarehe 25 Novemba 2019 na kampeni hii inakamilika tarehe 10 Desemba. Hizi ni siku za kuragibisha kampeni kuhusu haki msingi za binadamu kuanzia kwenye ngazi ya chini kabisa, kwa sababu ukosefu wa haki msingi za binadamu katika jamii kunaweza kusababisha madhara makubwa katika afya ya watu.

Takwimu zinaonesha kwamba, kuna zaidi ya watu milioni 30 ambao wamefariki dunia kutokana na ugonjwa wa Ukimwi. Katika mapambano dhidi ya maambulizi mapya ya ugonjwa wa Ukimwi, Baraza la Makanisa Ulimwenguni linasema, asiwepo mtu anayebakizwa nyuma dhidi ya mapambano haya. Inakadiriwa kwamba, zaidi ya watu milioni 40 wanaishi na Virusi vya Ukimwi sehemu mbali mbali za dunia na kati yao kuna wagonjwa milioni 25 ambao wanapewa dawa za kurefusha maisha. Baraza la Makanisa Ulimwenguni linawataka wanajumuiya mbali mbali kuungana mkono na kutembea kwa pamoja dhidi ya maambukizi mapya ya ugonjwa wa Ukimwi duniani. Mwaka 2018, maambukizi mapya yalikuwa ni watu milioni 1. 7 na zaidi ya wagonjwa 770, 000 walifariki dunia kutokana na magonjwa nyemelezi. Wanawake ambao wamenyanyaswa kijinsia wanayo hatari kubwa ya kuambukizwa magonjwa na hasa Virusi vya Ukimwi.

Kwa upande wake, Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana antonio Guterres anasema, Jumuiya ya Kimataifa inapaswa kushikamana kwa dhati ili kutokomeza maambuzi ya Ukimwi ifikapo mwaka 2030 kama ilivyobainishwa na Jumuiya ya Kimataifa katika utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Binadamu Ifikapo mwaka 2030. Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na wadau mbali mbali wanapaswa kuongeza kasi ya mchakato wa huduma za afya ili kudhibiti maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi. Watu wanapaswa kudai haki zao msingi na kuchagiza fursa za kupata huduma bora za kijamii na kiafya pamoja na kuondokana na unyanyapaa na sheria zenye harufu ya kibaguzi dhidi ya waathirika wa Virusi vya Ukimwi. Jambo la kusikitisha na kuona kwamba rasilimali fedha kwa ajili ya mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Ukimwi imepungu sana tangu mwaka 2018, kwani kiasi cha dola za kimarekani bilioni 1 zinakosekana. Kumbe, mshikamano na mafungamano ya kijamii dhidi ya maambukizi mapya ya ugonjwa wa Ukimwi ni kati ya vipaumbele vinavyotolewa na Jumuiya y Kimataifa kwa wakati huu!

Ukimwi 2019

 

02 December 2019, 16:23