Tafuta

Bado mivutano inaendelea nchini Malawi tangu kumaliza uchaguzi mkuu wa Rais kunako mwezi Mei mwaka huu Bado mivutano inaendelea nchini Malawi tangu kumaliza uchaguzi mkuu wa Rais kunako mwezi Mei mwaka huu 

Malawi:Bado mivutano inaendelea baada ya uchaguzi!

Kufuatia na mivutano ambayo bado inaendelea baada ya uchaguzi mkuu nchini Malawi kunako mwezi Mei mwaka huu,maaskofu nchini humo wanatoa wito ili kuheshimu sheria na haki ya nchi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Hivi karibuni Baraza la Maaskofu katoliki nchini Malawi wametoa wito kuhusu kuheshimu na kusaidia haki ya nchi katika matarajio ya kutangazwa wazi juu ya uchaguzi wa Rais uliofanyika tarehe 21 Mei 2019. Wametoa wito huo kufuatia na ghasia zinazoendelea nchini humo. Matokeo kwa ujumla ya mwezi Mei mwaka huu kiukweli, hayajakubalika baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilipotangaza ushindi wa  Rais wa sasa  Arthur Peter Mutharika wa Chama cha maendeleo cha Kidemokrasia, na ambacho bado kinaendelea kupingwa. Viongozi hao wawili wa upinzaji, Lazaro Chakwera wa Chama cha Wabunge wa Malawi na Makamu wa Rais wa zamani, Saulos Klaus Chilima wa chama cha Harakati ya Mabadiliko ya Muungano walikataa matokeo hayo na kuitaka Mahakama ya Katiba kuingilia kati. Hofu ya maaskofu, kwa namna hiyo, ni kwamba washiriki wanaohusika wanaweza kuanza kufanya vurugu.

Maaskofu wanasema wote lazima kuwajibika

Maaskofu wanasema “ tunawajibika wote na kuhusika kuhamasisha amani na umoja” huku wakiwaalika raia wa nchi kuheshimu na kuunga mkono utawala wa sheria, ili kila mtu aishi kwa amani. Wakati huo huo, maaskofu wanalaani vikali kila aina ya dhuluma ambayo inaendelea kutokea katika sehemu nyingine za nchi, kwa sababu wanasema vurugu ni mbaya na haikubaliki.  Maaskofu nchini Malawi wansema “Ni dhidi ya haki za binadamu na uhuru ambao tumepigania tulipochagua mfumo wa serikali wa vyama vingi”. Kwa upande wao, maaskofu wanahaidi kufanya kazi kwa ajili ya  haki, amani, maridhiano na umoja wa kitaifa. Lakini hata hivyo  wanaalika tume zote za Kanisa, kwa namna ya pekee  kwa zile za  Mawasiliano ya kijamii na ile ya Haki na Amani, ili kutafuta  njia madhubuti za kuandaa watu ili kukubali hukumu ya Mahakama ya Katiba, ili kutunza, kukuza na kulinda amani na umoja kati ya Wamalawi.

Ujumbe unaishia na sala ya Mtakatifu Francis wa Assisi

Ujumbe wa Baraza la Maaskofu nchini Malawi unaishia kwa kutumia maneno ya sala kwa ajili ya amani iliyotungwa na Mtakatifu Francis wa Assisi isemayo: “Bwana, nifanye niwe chombo cha amani yako”. Na ikumbukwe kwamba  ilikuwa ni  tarehe 26 Kanisa katoliki nchini Malawi lilikuwa limetamka kuhusu Siku ya Maombi kitaifa kwa ajili ya amani, umoja na mapatano, kwa matumaini ya kuanzisha majadiliano kati ya vyama vya kisiasa kwa ajili faida ya kitaifa. Na walikuwa wamesema kwamba : “Sisi Wakatoliki tumeomba na kuendelea kufanya hivyo, tukiwaalika viongozi wa vyama vyote vya siasa ili kukomesha kiburi chao, waangalie taifa linaloungua moto na kutafuta suluhisho la kisiasa”. Haya yalikuwa yamesemwa na Rais wa Baraza la Maaskofu wa Malawi, Askofu Luke Thomas Msusa katika fursa ya Mkutano wao na ilikuwa ni matarajio yake  kwamba majadiliano yataleta matunda kati ya vyama, kwa jina la suluhisho la kisiasa la haraka.

 

13 December 2019, 15:07