Umetiwa sahini hivi karibuni katika makao makuu ya Umoja wa Afrika Jijini Addis Abeba  kuhusu mafunzo ya utaalam baranai afrika! Umetiwa sahini hivi karibuni katika makao makuu ya Umoja wa Afrika Jijini Addis Abeba kuhusu mafunzo ya utaalam baranai afrika! 

Acli kutia sahini na Umoja wa Afrika kwa ajili ya mafunzo ya ufundi barani humo!

Katika jijini la Addis Abeba Ethiopia hivi karibuni imetiwa sahini ya kumbukumbu kwa ajili ya usambazaji wa mafunzo ya ufundi katika nchi mbali mbali barani Afrika ili kujaza pengo kutokana na kukosekana kwa mafunzo ya ufundi na kueneza katika maeneo tofauti ya Afrika.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika makao makuu ya Umoja wa Afrika (AU) jijini Addis Abeba Ethiopia  hivi karibuni imesaniwa  Hat ya kumbukumbu kuhusu usambazaji wa mafunzo ya ufundi katika nchi mbali mbali  barani  Afrika ili kujaza pengo kutokana na kukosekana kwa mafunzo ya ufundi na kuineza  katika maeneo tofauti ya Afrika. Kuna saini mbili: kwa upande mmoja ni ile ya Profesa Sarah Mbi Enow anyang Agbor, Kamishna wa Rasilimali za watu, Sayansi na Teknolojia ya Jumuiya ya Umoja wa Afrika na Roberto Rossini, Rais wa Acli na Balozi wa Italia katika Jumuiya ya Muungano wa Afrika (AU), Giuseppe Berlendi, alihudhuria makubaliano ya sahihi hiyo. Kulingana na Kamishna, elimu ya msingi ni hali ya msingi lakini haitoshi kwa maendeleo kwa sababu lazima ifuate elimu ya utaalam. Tutalazimika kukabiliana na pengo la kijiografia ambalo linahusu pengo la mashambani-mji, ikizingatiwa kuwa ubora zaidi na zaidi umewekwa juu ya yote kuelekea miji mikuu ya 54 au maeneo mingine ya mijini, wamsebainisha.

Kutokana na makubaliano haya Acli, itahusika, katika miezi 24 ijayo, katika usaidizi wa kiufundi kwa ajili ya mifumo tofauti ya mafunzo ya kitaalam ambayo hutofautiana kulingana na eneo, maarifa yake, matumizi, mila na desturi. Chama cha  Italia kitaingilia kati katika nchi mbali mbali kama vile Msumbiji, Tanzania, Somalia na Burundi, lakini pia hata nchi ya Senegal. Mkataba wa uelewa na Jumuiya ya Umoja wa  Afrika unatazamia mipango mbali mbali katika  Chama cha ACLI, Enaip, cha Acli ya Terra na Ipsia. Saini ya mkataba huu ni hatua nyingine msingi iliyofanywa  na Acli4Africa kwa jumuiya na maeneo ya nje ya nchi – kwa mujibu wa  rais wa kitaifa wa ACLI na Enaip, Bwana Roberto Rossini. Na ACLI inatoa ahadi ya  kukuza maendeleo ambayo kwa mujibu wa Mtakatifu Papa Paolo VI, ni jina mpya la amani. Mafunzo ya ufundi inaweza kuwakilisha siku boraza za usoni kwa vijana wengi, kwa sababu inawezekana kuingia kuwasiliana na ulimwengu wa biashara wa eneo hilo, ukizingatia mahitaji yao na kwa hivyo mahitaji ya kazi.

Viongozi ahadi ni deni tutimize kwa huduma ya afya kwa wote: Hata hivyo katika Siku ya huduma za afya kwa wote, tarehe 12 Desemba 2019, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  ametoa wito kwa viongozi wa dunia kutimiza ahadi waliyoitoa mwezi Septemba mwaka huu na kuhakikisha afya kwa wote ni hali halisi kwa kila mtu, kila mahali.  Katika ujumbe wake maalum wa siku ya kimataifa ya afya kwa wote Bwana Antonio Guterres amesema wakati watu wengi wanapata huduma muhimu za afya kuliko hapo awali, bado wengi sana wanazikosa. Ameongeza kuwa haikubaliki na sio haki kwamba nusu ya idadi ya watu ulimwenguni bado wanakosa kupata huduma hizi muhimu na watu milioni 100 hutumbukia katika umaskini uliokithiri kila mwaka kutokana na gharama za huduma za afya.

Amesema huduma za afya kwa mtu hazipaswi kutegemea utajiri wake au iwapo wanaweza kuishi. Aidha ameitaka dunia kutanguliza mahitaji ya wale walio hatarini zaidi na walioachwa nyuma, kupitia kuongeza uwekezaji wa umma katika mnepo wa mifumo ya huduma za msingi za afya, ikiwemo mahitaji ya afya ya akili. Pia ameitaka dunia kutambua  mzigo unaoongezeka unaosababishwa na uchafuzi wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi kwenye mifumo ya afya na huduma za afya. Amesisitiza kuwa huduma za afya kwa wote ni muhimu katika utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu, muongozo wa mustakabali bora kwa watu na sayari hivyo ametaka itimizwe ahadi ya uwekezaji katika ubinadamu, ustawi na mafanikio kwa kila mtu.

16 December 2019, 09:05