Tafuta

Vatican News
UNESCO inasema, katika kipindi cha mwaka 2006 hadi mwaka 2018 kuna waandishi wa habari 1, 109 wameuwawa kikatili sehemu mbali mbali za dunia. UNESCO inasema, katika kipindi cha mwaka 2006 hadi mwaka 2018 kuna waandishi wa habari 1, 109 wameuwawa kikatili sehemu mbali mbali za dunia.  (AFP or licensors)

Waandishi wa Habari 1, 109 wameuwawa kati ya Mwaka 2006-2018: UNESCO

Tangu mwaka 2006 hadi mwaka 2018 kuna waandishi wa habari 1, 109 kutoka sehemu mbali mbali za dunia, wameuwawa kikatili na hakuna watu waliokamatwa na kufikishwa mbele ya sheria. Nchi za Kiarabu zinaongoza kwa asilimia 30%, nchi kutoka Amerika ya Kusini na Caribbean kwa asilimia 26%. Katika orodha hii, Bara la Asia na Nchi za Ukanda wa Pacific zinaongoza kwa asilimia 24%.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Siku ya Kimataifa ya Kukomesha Kutokujali kwa Uhalifu dhidi ya Waandishi wa Habari, duniani inasherehekewa kila mwaka ifikapo tarehe 2 Novemba. Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO linabainisha kwamba, tangu mwaka 2006 hadi mwaka 2018 kuna waandishi wa habari 1, 109 kutoka sehemu mbali mbali za dunia, wameuwawa kikatili na hakuna watu waliokamatwa na kufikishwa mbele ya sheria kujibu shutuma za mauaji ya watu hawa. Nchi za Kiarabu zinaongoza kwa mauaji ya wadau wa tasnia ya mawasiliano kwa asilimia 30%, zikifuatiwa na nchi kutoka Amerika ya Kusini na Caribbean kwa asilimia 26%.

Katika orodha hii, Bara la Asia na Nchi za Ukanda wa Pacific zinaongoza kwa asilimia 24%. Takwimu za mwaka 2017-2018 zinaonesha kwamba, asilimia 505 ya wadau wa tasnia ya mawasiliano wameuwa nje ya maeneo ya vita na kinzani za kijamii. UNESCO inaitaka Jumuiya ya Kimataifa kuwaheshimu na kuwalinda waandishi wa habari sehemu mbali mbali za dunia, ili waweze kuendelea na shughuli zao kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi! Huu ni mwaliko pia wa kukuza na kudumisha ushirikiano miongoni mwa Jumuiya ya Kimataifa ili kulinda utu, heshima na maisha ya waandishi wa habari duniani. Itakumbukwa kwamba, Siku hii ya Kimataifa kwa mwaka 2015 iliadhimishwa Jijini Arusha, nchini Tanzania.

UNESCO: Mauaji
02 November 2019, 13:59