Tafuta

Vatican News
Mabadiliko duniani:Uvumbuzi na ubunifu ni njia madhubuti katika kuhakikisha miji endelevu ambapo ni mada iliyochaguliwa kuongoza maadhimisho ya Siku ya miji Muniani 2019. Mabadiliko duniani:Uvumbuzi na ubunifu ni njia madhubuti katika kuhakikisha miji endelevu ambapo ni mada iliyochaguliwa kuongoza maadhimisho ya Siku ya miji Muniani 2019. 

Siku ya Miji duniani 2019:ubunifu na maisha bora kwa kizazi endelevu!

Mabadiliko ya dunia.Uvumbuzi na ubunifu ni njia madhubuti katika kuhakikisha miji endelevu ndiyo kauli mbiu iliyoongoza katika maadhimisho ya Siku ya miji duniani 2019.Ni siku ambayo huadhimishwa kila ifikapo tarehe 31 Oktoba.Umoja wa Mataifa ulitangaza Siku hiyo ili kutoa ujumbe kwa mataifa yote wanachama,manispaa na raia ili kubadili mambo na kuboresha maisha ya miji mikuu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican 

Katika sehemu ya ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika maadhimisho ya siku ya miji duniani ambayo haudhimishwa kila tarehe 31 Oktoba ya kila mwaka,imeongozwa na kauli mbiu:“kubadili dunia:uvumbuzi kwa ajili ya maisha bora kwa vizazi vijavyo.Katika hotuba yake NBwana Guterres amesema, zaidi ya nusu ya idadi ya watu duniani hivi sasa wanaishi mijini na kufikia mwaka 2050 theluthi mbili ya watu watakuwa wanaishi mjini na wakati makazi ya kuendana na ongezeko la watu bado hayajakarabatiwa na miji mipya itahitaji kujengwa.

Uhalisia wa sasa unatoa fursa nyingi za kubuni na kutekeleza suluhisho

Katibu Mkuu Bwana Guterres amesema hali ya sasa na inayotarajiwa hapo baadaye, inatoa fursa nyingi za kubuni na kutekeleza suluhisho ambalo linaweza kukabiliana na janga la mabadiliko ya tabianchi na kuweka njia kwa ajili ya mustakabali endelevu. Ameongeza kusema kwamba, miji inatumia theluthi mbili ya kawi au nishati ya umeme ya dunia na inazalisha asimia 70% ya hewa chafuzi. Kimataifa, uamuzi utakaofanyika katika miundombinu mijini katika miongo ijayo kuhusu mipango miji, matumizi bora ya kawi, uzalishaji umeme na usafiri, ambavyo vitakuwa na athari kwa hali ya uchafuzi, kiukweli ni katika miji ambayo vita dhidi ya mabadiliko ya tabianchi itaibuka ushindi au kupoteza. Vile vile Bwana Guterres amesema, licha ya uchafuzi unaotokea mijini, lakini pia miji inachangia asilimia 80 ya pato la taifa kama vile  vituo vya elimu na ujasiriamali, na mbavyo ni kitovu cha uvumbuzi na ubunifu huku vijana wakichukua uongozi.

Changomoto kubwa ni mabadiliko ya tabianchi, ukosefu wa usawa na uhamiaji

Katika kuadhimisha siku kauli mbiu pia inaungwa mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la makazi la Umoja wa Mataifa, (UN-Habitat) Bi. Maimunah Mohd Sharif katika ujumbe wake ambapo  wakati wa kuadhimisha siku hii amesema, changamoto kubwa za dunia ya sasa kutokana na mabadiliko ya tabianchi ni ukosefu wa usawa, uhamiaji kuelekea mitaa duni huku athari mbaya zikiathiri idadi kubwa ya watu mijini. Kwa mantiki hiyo amesema kwamba: “bila mawazo bunifu tutashuhudia ongezeko la joto, mlundikano wa taka, ongezeko la makazi yasiyo rasmi, ongezeko la msongamano wa magari na kuibuka kwa miji bila mipangilio. Na hiyo ni tofauti na miji jumuishi, salama, endelevu na stahimilivu tunayolenga kuunda kufikia mwaka 2030 kuendana na lengo 11 la malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa, SDGs.” amebainisha. Na kutokana na hilo Bi. Sharif ametoa wito wa kufanya kazi pamoja kkatika uvumbua kwa ajili ya kuleta mabadiliko ulimwenguni kote  leo na  kuhakikisha kwamba hakuna atakaye au sehemu yoyote itakayowachwa nyuma. Bi Sharifu amesema: “hebu tufanye hilo kwa ajili ya vizazi vijavyo ili waweze kurithi dunia bora kuliko ile tuliyoipata kutoka kwa waliotutangulia.”

UNESCO wameandaa mkutano jijini Paris, Ufaransa kwa ajili ya Siku ya Miji duniani

Hata hivyo katika maadhimishi ya Siku ya Miji Duniani Unesco imeandaa mkutano Jijini Paris Ufaransa kwa kuwaunganisha pamoja wawakilishi kutoka manispaa karibu 24 ulimwenguni kote ambao wameafanya kazi katika paneli nne zilizowekwa kufuatia na mada  kama vile ya uendelevu na hatua za hali ya hewa, miji kuzaliwa kwa upya na ujumuishaji wa kijamii, uvumbuzi wa kiteknolojia na changamoto za siku zijazo. Wadau hao katika  tishu hizi kuhusu miji wamejishughulisha na mada hizi kwa kuzingatia kuwa ikiwa miji inawakilisha asilimia 3% tu ya uso wa dunia, wajue kwamba  wao pia wanawajibika kwa matumizi ya nishati na robo tatu ya uzalishaji wa mabaki kwenye sayari.

Umoja wa Mataifa unataka mataifa, manispaa na raia kubadili maisha ya miji mikuu 

Hata hivyo ili kuweza kufanikia mkutano huo, mijadala ya hadhara na ya kutumia sauti ya kusikiliza vimeweza kuwaunganisha pamoja wadau wote ili kupata uzoefu tofauti na ubunifu ambao miji inayoungwa mkono na UNESCO imeweza kujikita katika matendo ya kweli  kwa miaka ya hivi karibuni katika sekta kama vile mapambano dhidi ya ubaguzi, malengo ya maendeleo endelevu, elimu na uhuru wa habari, ulinzi wa urithi wa kitamaduni na mengine mengi. Katika fursa ya siku hiyo, pia UNESCO imeungana na Shirika  la Kilimo duniani (FAO), Shirika la Umoja wa Mataifa la Kusaidia wakimbizi (UNHCR), Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa (UN-Habitat) ili kuweza kukuza kazi ya pamoja juu ya kukaribia malengo ya maendeleo endelevu SDGs yaliyowekwa na Umoja wa Mataifa katika Ajenda ya 2030. Umoja wa Mataifa vile vile  (UN) ulitangaza Siku ya Miji ya Duniani ili  kutuma ujumbe wake kwa mataifa yote wanachama, manispaa na raia kwa ujumla ili kubadili mambo na kuboresha maisha ya miji mikuu.

04 November 2019, 18:17