Umoja wa mataifa kupitia kamati yake ya maendeleo na fedha umesema kuwa fedha za misaada kutoka nje zinapaswa zielekezwe katika vipaumbele  mendeleo kitaifa Umoja wa mataifa kupitia kamati yake ya maendeleo na fedha umesema kuwa fedha za misaada kutoka nje zinapaswa zielekezwe katika vipaumbele mendeleo kitaifa  

Nchi maskini zaidi hakikisha fedha zinajali vipaumbele!

Tarehe 19 Novemba 2019 Umoja wa Mataifa katika ripoti yake kupitia kamati yake ya maendeleo na biashara,UNCTAD umesema kuwa mataifa maskini zaidi duniani yanapaswa kuhakikisha kuwa fedha za misaada kutoka nje zinaelekezwa katika vipaumbele maendelo ya kitaifa.

Umoja wa Mataifa katika ripoti yake kupitia kamati yake ya maendeleo na biashara, UNCTAD umesema kuwa mataifa maskini zaidi duniani yanapaswa kuhakikisha kuwa fedha za misaada kutoka nje zinaelekezwa katika vipaumbele vya maendelo ya kitaifa. Ni katika ripoti  hiyo inayohusu mataifa yaliyo maskini zaidi (LDCs) iliyotolea tarehe 19 Novemba 2019 ambapo inafafanua kuwa mataifa ni 15 kati ya mataifa 20 yanayohitaji zaidi msaada na hii kwa kiasi kikubwa inatokana na nchi hizo kukosa akiba ya fedha za ndani.

Naye Katibu Mkuu  Kamati ya Maendeleo na Biashara UNCTAD, Dk. Mukhisa Kituyi amesema kuwa ili mataifa hayo yaweze kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs na kuepukana na utegemezi wa misaada, ni lazima yapatiwe msaada wa fedha kutoka nje. Hata hivyo amesema ni lazima nchi hizo zimiliki ajenda yao ya maendeleo na kusimamia vyema uelekezaji wa fedha hizo za nje kwenye vipaumbele vya kitaifa vya maendeleo na jamii ya kimataifa isaidie kufanikisha lengo hilo.

Ripoti hiyo aidha  inasema, hivi sasa kuna muundo mpya wa utoaji wa  misaada ambao hata hivyo haujagusa maeneo ya maendeleo hasa kwenye miundombinu. Mkuu wa kitengo cha mataifa masikini zaidi duniani (LDCs) katika  Kamati ya maendeleo na biashara (UNCTAD) Bwana Rolf Traeger amesema kuwa uhusiano kati ya msaada wa fedha za kigeni na vipaumbele vya maendeleo ya kitaifa unazidi kudhoofika na huku “muundo wa msaada wa maendeleo wa kigeni, (ODA) unaegemea zaidi kwenye sekta za kijamii ambayo inapokea asilimia 45 ya msaada, ikilinganishwa na miundombinu ya kiuchumi inayopokea asilimia 14 na ile ya uzalishaji asilimia 8.”

Na kama hiyo haitoshi, hata hivyo ripoti inaonesha kuwa, mfumo wa sasa wa ufadhili umegubikwa na msururu wa kanuni na ulegezaji wa masharti unaompatia nafuu mkopaji lakini akijikuta analipa zaidi deni kwa hofu ya kuongeza deni la nje. Kwa  mantiki hiyo  Kamati ya maendeleo na bishara ya Umoja wa mataifa (UNCTAD) inataka kitengo cha mataifa maskini zaidi duniani (LDCs) zichukue hatua kuweza kusimamia vyema fedha zake ambapo ripoti inasema kuwa, “kubadili mwelekeo huu ni lazima mataifa hayo yaimarishe usimamizi wa fedha zao za maendeleo. Hii inaweza kufanikiwa kwa kuanzisha au kuimarisha mfumo wa uratibu wa misaada, kama ambavyo inatekelezwa na mataifa hayo kama vile Rwanda na Jamhuri  ya watu wa Lao.”

20 November 2019, 12:23