Maelfu ya watoto nchini Camerun wanaishi kwa hofu na wanataka amani ili wapate kurudi katika meza za shule kwa ajili ya maisha yao ya baadaye Maelfu ya watoto nchini Camerun wanaishi kwa hofu na wanataka amani ili wapate kurudi katika meza za shule kwa ajili ya maisha yao ya baadaye 

Asilimia 90 ya shule nchini Camerun zimefungwa kutokana na vurugu na hali tete ya kisiasa.

Ni zaidi ya watoto 855,000 ambao hawaendi shule Kaskazini Magharibi na Kusini Magharibi mwa nchi ya Camerun kufuatia na ghasia na vurugu ambazo zimeendele kwa kipindi cha miaka mitatu. Shirika la UNICEF limeyasema haya katika taarifa yake iliyotolewa hivi karibuni. Ikumbukwe kwamba, elimu ni ufunguo wa maisha na matumaini kwa vijana wa kizazi kipya!

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 29 Septemba 2019 mara baada ya Sala ya malaika wa Bwana, Baba Mtakatifu Francisko alitoa wito kwa ajili ya kuliombea taifa la Camerun ili kuweza kutafuta suluhisho la haki ya amani ya kudumu. Alisema hayo wakati wanajiandaa kufungua mkurano wa majadailiano ya Kimataifa tarehe 30 Septemba kwa ajili ya kupata mwafaka dhidi ya mgogoro ambao unadumu kwa miaka sas ana kuwa tishio kubwa kwa watu. Katika fursa hiyo Baba Mtakatifu Francisko alisali ili mkutano huo wa kimataifa na viongozi wa kisiasa na kidini waweze kupata mwafaka kwa ajili ya manufaa ya wote nchini huo.

Kwa miaka mitatu ya ghasia ileta athari kwa watoto wa shule

Hata hivyo kufuatia na mwendelezo ghasia na vurugu  kwa miaka mitatu  mfululizo katika maeneo ya kaskazini magharibi na kusini magharibi mwa Camerun zimewafanya zaidi ya watoto 855,000 washindwe kwenda  shuleni, kwa mujibu wa taarifa za shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF. Katika taarifa iliyotolewa kwa pamoja tarehe 5 Novemba 2019 huko  New York, Marekani, Dakar, Senegal na Geneva Uswis imemnukuu Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Bi. Henrietta Fore akisema kuwa bila ya hatua za dharura na kujitolea kutoka pande zote katika mzozo huo kwa  kulinda elimu kwa njia zote, hatma ya watoto hao iko hatarini. Bi Fore amesema maelfu ya watoto nchini Camerun wanaishi kwa hofu na wanataka amani ili wapate kurudi katika meza za shule  kwa ajili ya maisha yao ya baadaye.

Tangu kuanza muhula wa shule asilimia 90 ya shule zimefungwa

UNICEF inasema miezi miwili tangu kuanza kwa mwaka mpya wa shule, karibu asilimia 90 ya shule za msingi za umma ikiwa ni zaidi ya shule 4,100 na asilimia 77 ya sekondari za umma au shule 774 zimebaki zimefungwa katika meneo ya Kaskazini magharibi na kusini magharibi.  Hofu ya kuzuka ghasia imesababisha wazazi wengi kutowapeleka watoto wao shuleni na walimu kutofika kazini. Kati ya watoto hao, takribani watoto 150,000, wamehama makwao hali inayosababisha kuwaongezea mihangaiko. Hata katika sehemu nyingine, shule zimefungwa na UNICEF kwa sasa inaendelea kugawa vitabu na vifaa vingine vya masomo kwa watoto 37,000 ili kuwasaidia katika masomo yao. Halikadhalika, UNICEF itaandaa vipindi vya masomo kwa njia ya radio kwa watoto wanaobaki nyumbani. Masomo hayo yamerekodiwa kwa msaada wa UNICEF na yatawasaidia watoto hao katika somo la hesabu na lugha.

07 November 2019, 14:19