Tafuta

Vatican News
Ripoti mpya ya Unicef imetolewa kuonesha takwimu za maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU) kwa watoto na vijana wadogo katika kuelekea kilele cha Siku ya kuthibiti ukimwi duniani Mosi Desemba Ripoti mpya ya Unicef imetolewa kuonesha takwimu za maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU) kwa watoto na vijana wadogo katika kuelekea kilele cha Siku ya kuthibiti ukimwi duniani Mosi Desemba 

Kila saa wanakufa watoto na vijana wadogo 13 na zaidi ya 300 wanakufa kila siku!

Kila saa moja wanakufa watoto na vijana wadogo 13 na zaidi ya watoto 300 wanakufa kila siku kutokana na masuala yanayohusu virusi vya ukimwi(VVU).Ni kutoka katika Ripoti ya pili ya Shirika la kusaidia watoto duniani UNICEF wakati wa kuelekea kilele cha Siku ya kupambana na Ukimwi duniani kila tarehe Mosi Desemba ya kila mwaka.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Tarehe 26 Novemba 2019 imetolewa ripoti ya pili kwa ufupi na Shirika la Kusaidia watoto UNICEF kuhusu watoto wanaosihi na VVU. Ripoti hiyo mpya imetolewa ikiwa ni katika fursa ya kuelekea katika kilele cha Siku ya Kuthibiti Ukimwi Duniani inayoadhimishwa  kila tarehe Mosi Desemba. Katika Ripoti hiyo inasema kwamba, watoto ambao wanaishi na virusi wa Ukimwi,(VVU) ni nusu yake tu ambao wanapatiwa tiba ya kuokoa maisha yao. Kunako mwaka 2017 karibia watoto 320 na vijana walikufa kila siku kwa sababu ya virusi hivyo, hiyo  inamaanisha kwamba ni watoto 13 kila saa limoja.

Takwimu muhimu za mwaka 2019

Katika ripoti hii mpya inasema kuwa kunako 2018, karibia watoto 160.000  wenye umri kati ya 0-9 ambao wamekumbwa na virusi vya ukimwi na kupelekea idadi ya watoto katika kikundi hicho cha wanaoshi na virusi vya ukimwi kuwa milioni 1,1; wasichana wadogo 140.000 wamekumbwa na virusi vya ukimwi kwa mwaka 2018, kulingana na  wavulana wadogo 50.000. Watoto 89.000 chini ya umri wa miaka 5 wamekumbwa na vurusi,  wakati mama zao wakiwa wajawazito au wakati wanajifungua watoto wao na watoto 76.000 ni wakati wa kipinid cha kunyonya katika mwaka 2018.

Maendeleo ya utafiti wa dawa ya kuzuia ukimwi

Hata hivyo dunia iko karibu kupata matokeo makubwa ya mapambano dhidi ya virusi vya ukimwi (VVU) na AIDS, lakini hatupaswi kusimama mbele ya maendeleo ya matokeo hayo yaliyotimizwa kwa mujibu wa Bi Henrietta Fore, Mkurugenzi Mkuu wa UNICEF.  Aidha amesema kwamba: “Kuwekeza kwa vipimo na tiba kwa watoto na vijana ni suala la maisha na kifo na kwa ajili yao ni lazima kuwafanya lolote hasa la kuchagua maisha”, Bi Fore amesisitiza. Katika Takwimu vile vile  zinaonesha pengo kubwa kikanda katika tiba kwa ajili ya watoto ambao wanaishi na virusi vya  (VVU).  Sehemu kubwa ni Asia ya kusini kwa asilimia 91%, inafuatia Nchi za Mashariki na Afrika ya Kaskazini kwa asilia  (73%), Afrika Mashariki na Kusini kwa asilimia  (61%), Asia ya Magharibi na Pasifiki (61%), Amerika ya Kusini na Visiwa vya Caribbien asilimia  (46%) Na Afrika Magharibi na ya Kati kwa asilimia (28%).

Idadi ya mama wanaofuata matibabu ya kuzuia kuenza virusi kwa watoto inaongezeka

Kwa mujibu wa ripoti hiyo aidha inafafanua kwamba, mama ambao wanafuatilia matibabu kwa ajili ya kuzuia usambazaji wa virusi kwa watoto wao imeongezeka kwa ngazi ya kidunia na kufikia asilimia 82%,  takwimu zinaongezeka kulinganisha na asilimia 44% ya pungufu ya miaka 10 iliyopita. Licha ya hayo, bado kuna tofauti kati ya kanda  kama vile Afrika Mashariki na kusini kwa  kiwango cha juu zaidi (92%), ikifuatiwa na Amerika ya Kusini na Visiwa vya Carribbien (79%), Afrika Magharibi na Kati (59%), kusini mwa Asia (56%), Asia ya Mashariki na Pasifiki (55%) na Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini (53%). “Bado kuna safari ndefu ya kufanya japokuwa tendo la kuwapatia mama  tiba ya kuzuia kuambukizwa kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto imeweza kusaidia karibia milioni 2 za kesi mpya za virusi vya VVU   na kuzuia vifo zaidi ya milioni moja ya watoto chini ya miaka 5” amesisitiza Bi Fore. Kwa njia hiyo: “Tunahitaji kuona maendeleo kama hayo katika utunzaji wa watoto. Kupunguza pengo hili kati ya watoto na mama zao kunaweza kuongeza kwa kiasi kikubwa matarajio na ubora wa maisha ya watoto walioathiriwa na VVU.”

Na Jumuiya ya Kimataifa iweke kasi kusaidia misaada ya kibinadamu Sudan

Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura, OCHA, Bwana Mark Lowcock amehitimisha ziara yake nchini Sudan huku akitaka jumuiya ya kimataifa iweze kuongeza kasi ya kupeleka misaada ya kibinadamu nchini humo. Bwana Lowcock katika ziara yake ya kwanza tangu kuundwa kwa serikali ya mpito nchini humo mwezi Agosti mwaka huu, ameshuhudia kweli kudorora kwa hali ya kibinadamu hususan kwenye maeneo ya kati na mashariki mwa nchi hiyo na kusema kwamba mamilioni ya maisha ya watu yako hatarini.

Kwa mfano akiwa jimbo la Kassala, mashariki mwa Sudan, amejionea hali halisi ambako, zaidi ya watu 400,000 wanakabiliwa na uhaba wa chakula na ni asilimia 13 tu ya wakazi wa vijijini ndio wanapata huduma ya maji safi na salama, milipuko ya magonjwa nayo ikikwamisha harakati za serikali za kuchukua hatua kusaidia kukwamua jamii. Bwana Lowcock amesema kuwa, “hapa hakuna mzozo. Kuna amani na utulivu na kihistoria mashirika ya misaada ya kibinadamu huwa hayafiki huku. Lakini sasa kuna janga la kiuchumi na kuna tatizo la utapiamlo. Kuna mlipuko wa magonjwa ya kuambukiza, magonjwa yanayoua kama vile kipindupindu, dengue, surua na magonjwa mengine".

Bwana Lowcock amepongeza Sudan

Mkuu huyo wa OCHA pia amekutana na Waziri Mkuu Abdallah Hamdock ambapo amesema, “kuna serikali mpya Sudan na ina ajenda ya maendeleo. Hata hivyo inahitaji msaada zaidi kutoka jamii ya kimataifa. Tunatarajia miezi michache ijayo kushuhudia tatizo la kibinadamu hapa, hata katika maeneo yenye amani”. Bwana Lowcock amepongeza azma ya Sudan ya kuongeza uwezo wa mashirika kufikisha misaada ya kibinadamu kwa wahitaji huku akitambua hatua zilizochukuliwa hadi sasa ikiwemo kupunguza taratibu za kiutawala kuruhusu mashirika hayo. Inasadikia kuwa serikali ya Sudan pia inasaidia juhudi za kuwezesha mashirika ya misaada kupita maeneo ambayo bado yako chini ya vikundi vilivyojihami huku Bwana Lowcock akipongeza pia kipaumbele cha serikali ya Sudan katika ujenzi wa amani na kusuluhisha mizozo nchini humo. Hivi sasa nchini Sudan zaidi ya watu milioni 8.5 wanahitaji misaada ya chakula, lishe, ulinzi na kwamba idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka. Mzozo nchini Sudan umesababisha takribani watu milioni 2 kusalia wakimbizi wa ndani huko  Darfur, Kordofan Kusini na eneo la Blue Nile.

26 November 2019, 15:40