Tafuta

Kwa upande wa Serikali ya Uturuki kupitia kwa Rais Recep Tayyip Erdogan imesema itaanzisha operesheni ya kujilinda dhidi ya wapiganaji wa Kikurdi kama walivyokubaliana. Kwa upande wa Serikali ya Uturuki kupitia kwa Rais Recep Tayyip Erdogan imesema itaanzisha operesheni ya kujilinda dhidi ya wapiganaji wa Kikurdi kama walivyokubaliana. 

Hofu ni kubwa kuhusu tishio la kuzuka vita kati ya Uturuki na Siria!

Marekani itaongezea mamia ya wanajeshi kwa mujibu wa Rais Trump,iwapo Uturuki itafanya lolote kuzidi kipimo.Lakini kutoka Ankara jibu ni kwamba maandalizi ya wanajeshi yanaendelea.Naye Kardinali Mario Zenari Balozi wa Vatican nchini Siria anasema matukio haya ya mwisho yanasababisha ukosefu zaidi wa msimamo katika nchi ambayo imekwisha teseka na vita.

Siku moja baada ya Rais wa Marekani kusema kuwa nchi yake inajiandaa kuondoka Kaskazini mwa Siria kupisha jeshi la Uturuki kuanzisha operesheni ya kijeshi, serikali ya Uturuki imesema maandalizi ya kushambulia eneo la kaskazini mwa Siria yalikwisha kamilika. Hata hivyo uamuzi wa Rais Donald Trump umekosolewa na wengi nchini Marekani ikiwa ni pamoja na viongozi  wa chama cha Republican serikalini, huku wakitilia mashaka hatua ya jeshi ya Uturuki dhidi ya wapiganaji wa Kikurdi ambao ni washiriki na Marekani katika vita dhidi ya kundi la serikali ya kiislam.

Viongozi hao kutoka chama cha Republican wanabaini kwamba ikiwa askari wa Marekani wataondoka kwenye mpaka na Uturuki na kuachia jeshi la Uturuki kuendesha operesheni katika eneo hilo la mpakani, kuna hatari la jeshi hilo kushambulia wapiganaji wa Kikurdi wanaoshirikiana na Marekani katika vita dhidi ya Serikali ya Kiislam. Kwa upande wake Serikali ya Uturuki kupitia kwa Rais Recep Tayyip Erdogan imesema itaanzisha operesheni ya kujilinda dhidi ya wapiganaji wa Kikurdi kama walivyo kubaliana na Rais Donald Trump kwa njia ya simu huku wakidai kuwa wapiganaji wa kikurdi ni magaidi. Umoja wa Ulaya umeonya kuwa hatua zinazotaka kuchukuliwa na Uturuki za kukabiliana na Wakurdi zitahatarisha usalama wa raia nchini Siria na Uturuki yenyewe.

Kwa upande wa Kardinali Mario  Zenari, Balozi wa Vatican nchini Siria amesema matukio haya ya mwisho yanazidishwa na  ukosefu wa msimamo katika nchi za kivita. Akihojiana na mwandishi wa habari wa Vatican News amesema, Nchi za Mashariki zimekuwa ni nchi za kivita. Migogoro ya Siria inazidi kuonyesha mshangao mkubwa na wa uchungu kwa miaka sasa tisa na kusababisha mambo kuwa magumu yakuweza kutatua. Aidha Kardinali Zenari amesema kwamba, hakuna ambaye angeweza kuona kile ambacho kimetokea tangu mwaka 2011 had sasa. Ni matarajio yake kuwa wasije shutukia wanajikuta tena mbele ya mivutano na vurugu zenye nguvu ziadi ya awali.

Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Antonio Guterres amesema anafuatilia kwa wasiwasi mkubwa kitisho kinachowakabili raia wa Siria kufuatia na uwezekano wa operesheni ya kijeshi kaskazini mashariki mwa nchi hiyo huku akitoa mwito kwa pande zote kujizuia. Msemaji wake Bwana Stephane Dujarric alipozungumza na waandishi wa habari amesema, Bwana Guterres amezitaka pande hizo kuhakikisha kuwa miundombinu ya raia inalindwa wakati wote huku akirudia matamshi yake kwamba, vita haviwezi kuwa suluhisho la mzozo huo Siria. Huko nchini Siria utawala wa Kikurdi umewataka raia wake kupigania eneo lao dhidi ya kitisho cha uvamizi wa Uturuki ambayo imekwisha taarifu kuwa wako tayari kwa operesheni yake ya kijeshi.

09 October 2019, 14:47