Tafuta

aibu Katiku Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuna uthibitisho mkubwa juu ya ushiriki wa wanawake ambao hufanya michakato ya amani na usalama kuwa jumuishi zaidi na yenye ufanisi na ya kudumu. aibu Katiku Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuna uthibitisho mkubwa juu ya ushiriki wa wanawake ambao hufanya michakato ya amani na usalama kuwa jumuishi zaidi na yenye ufanisi na ya kudumu. 

AU:Wanawake wako hai katika harakati za kulinda amani!

Afrika inapaswa kusimamia masuala ya Usawa wa Kijinsia ya Ethiopia.Ni kwa mujibu wa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bi.Amina Mohammed kwenye Uzinduzi wa Mtandao wa Viongozi wa Wanawake wa Afrika.Anatoa pongezi kuhusu Tuzo ya Amani ya Nobel iliyotolewa hivi karibuni kwa Waziri Mkuu Abiy Ahmed kwamba ni kichocheo cha wanawake,sera za kisiasa na kijamii nchini Ethiopia.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Tarehe 21 Oktoba 2019 Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bi. Amina J. Mohammed akiwa ziarani mjini Addis Ababa nchini Ethiopia amelihutubia Baraza la Amani na Usalama la Muungano wa Afrika (AU) na kuupongeza Muungano huo kwa kutekeleza kwa vitendo ahadi yao ya kuhakikisha usawa wa kijinsia na ushiriki wa wanawake. Katika hotuba yake amesema hili ni eneo jingine ambalo wana malengo sawa ya pamoja. Aidha amesema Katibu Mkuu amejitolea sana kusimamia juu ya uongozi wa wanawake na ushiriki wa kisiasa kama sehemu ya maono yake ya kuzuia migogoro. Vile vile amesema kwamba kuna uthibitisho mkubwa juu ya ushiriki wa wanawake ambao hufanya michakato ya amani na usalama kuwa jumuishi zaidi na yenye ufanisi na ya kudumu.

Wanawake wanahusika katika masuala ya kijamii na ni muhimili mkubwa

Bi Amina  akiendelea na hotuba yake ametoa mifano ya namna mbalimbali wanawake wanavyohusika katika masuala ya kijamii na walivyo muhimili mkubwa katika kuleta amani na usalama na kusema kuwa katika maeneo ambayo kumekuwa na migogoro, upatanisishi unaosimamiwa na wanawake umeonesha mafanikio. Zaidi ya hayo, amesema, wao  wanajua  kuwa uongozi wa wanawake katika michakato ya kufanya maamuzi ya kisiasa unaboresha matokeo kwa kila mtu katika jamii.  Katika  ulinzi wa amani, anasema  mahali ambako Umoja wa Mataifa una walinzi wa amani wanawake wanajeshi na wale wanaohudumu kama raia, matokeo ni makubwa. Hata hivyo kwa kutazama hali halisi ya takwimu, Bi Mohamed amesema takwimu zinabaki kuwa zenye kuleta wasiwasi mkubwa kwani wanawake ni asilimia 4 tu ya walinda amani wa vikosi vya Umoja wa Mataifa. Akiorodhesha kuhusu takwimu za athari za mifarakano inavyowaathiri wanawake amesema, mathalani mwaka jana ulishuhudia viwango vya juu vya dhuluma za kisiasa kulenga wanawake. Na hiyo ni kwamba mtu mmoja kati ya wanawake 5 waliofukuzwa, hukumbana na dhuluma ya kijinsia na nchi 9 kati ya 10 zilizo na viwango vya juu vya ndoa za watoto ziko katika hali mbaya.

Matarajio ya ziara katika siku za usoni na harakati za kupinga biashara haramu

Bi Amina akisisitiza zaidi amesema kwamba katika siku zijazo, watasafiri kwenda Djibouti, Somalia, na Eritrea kwa lengo la amani ya Wanawake na Usalama na maendeleo. Huu ni ujumbe wa tatu wa pamoja wa Muungano wa Afrika na Muungano wa Ulaya. Katika miaka iliyopita, wametembelea Congo (DRC), Nigeria, Sudan Kusini, Niger na Chad. Bi Amina katika hotuna yake kwenye  mkutano mwingine kuhusu jukumu la wanawake katika kushughulikia biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu, ameanza kwa kuipongeza nchi ya Ethiopia kwa kuonesha uongozi katika mapambano dhidi ya usafirishaji haramu wa binadamu, ikiwa ni nchi ya kwanza ya kusini mwa jangwa la Sahara kuungana na nchi nyingine 30 kuunga mkono Kampeni ya Umoja wa Mataifa inayofahamika kwa jina “ Blue Heart Campaign”, yaani Kampeni ya Moyo wa Bluu. Aidha amesema nchi pia imekuwa kiongozi katika kukuza ushiriki wa wanawake katika maisha ya umma, pamoja na Baraza la Mawaziri la kisiasa ambalo nusu ni wanawake. Akimpongeza Waziri huyo Bi Amina amesema ki ukweli, Tuzo ya Amani ya Nobel iliyotolewa hivi karibuni  kwa Waziri Mkuu  Bwana Abiy Ahmed ilionyesha jukumu lake katika kuongeza sana kichocheo cha wanawake katika maisha ya kisiasa na ya kijamii nchini  Ethiopia.

22 October 2019, 12:24