Tafuta

Vatican News
Katika Siku ya Kimataifa ya watoto wa kike inayoadhimishwa kila tarehe 11 Oktoba,kuna umuhimu wa kutazama malengo ya Azimio la Beijing la miaka 25 iliyopita la  jukwaa la kujikita katika matendo Katika Siku ya Kimataifa ya watoto wa kike inayoadhimishwa kila tarehe 11 Oktoba,kuna umuhimu wa kutazama malengo ya Azimio la Beijing la miaka 25 iliyopita la jukwaa la kujikita katika matendo 

Siku ya kimataifa ya watoto wa kike:nguvu ya wasichana haielezeki wala kusimamishwa!

Tarehe 11 Oktoba ni Siku ya Kimataifa ya watoto wa kike ambapo mashirika ya Umoja wa Mataifa yabanaibisha juu ya majanga yanayowakumba wasichana hao kama vile ukosefu wa elimu na ajira,kuwaoza wakiwa chini ya umri wa miaka 18,ubakwaji na huku wengine milioni 15,wenye umri wa miaka 15 na 19 wameathirika na manyanyaso ya kijinsia.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya watoto wa kike ambayo huadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe 11 Oktoba, Shirika la watoto UNICEF linakumbusha kuwa kila mwaka ni watoto wa kike milioni 12 ambao wanaolewa kabla ya kufikisha miaka 18 kwa maana ya ndoa za utotoni. Ni milioni 130 za watoto wa kike kati ya miaka 6 hadi 17 dunia kote ambao hawaendi shule; msichana 1 kati ya 4 wenye umri wa miaka 15 na 19 hana ajira, na wala kupata mafunzo au kozi yoyote ukilinganisha karibu na 1 ya 10 ya vijana wavulana wenye umri sawa na huo. Karibia milioni 15 ya watoto wa kike wenye umri kuanzia 15 na 19 wameathiriwa na manyanyaso ya kijinsia katika maisha yao; kwa ngazi ya ulimwengu, kunako mwaka 2018, asilimia 74% ya kesi mpya za virusi vya ukimwa (Hiv) kati ya vijana wenye umri wa miaka 10 na 19 ulithibitishwa kwa vijana wasichana.

Dunia bado inathamini vijana wa kiume na wanaume

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mashirika haya inasema, duniani leo hii bado kuna kasumba za kuthamini wavulana na wanaume. Mantiki hii husababisha wasichane wachague kile ambacho wao wanataka. Kwa mfao ni lini, na ni nani aweze kuolewa, aidha kama wapate elimu na wamalizie shule, au kama wanapate pia huduma za afya au kutafuta namna ya kuishi. Naye Francesco Samengo Rais wa UNICEF nchini Italia akifafanua kuhusu jambo hili amesema, “Leo hii ni zaidi ya bilioni 1,1 ya watoto wa kike walio chini ya miaka 18 ambao wako tayari kuanza kutengeneza maisha yao ya baadaye. Wako tayari vijana kike ukabiliana na afya yao, elimu na usalama ili wajijengee maisha yao yaliyo bora na kuunda ulimwengu ambao ni wa Amani  na matarajio mema ya wote. Kila mwaka tarehe 11 Oktoba ni siku ya kimataifa kwa ajili ya watoto wote wa Kike, UNICEF na wadau wake wanafanya kazi sana na wasichana kwa ajili kuongeza sauti zao na kutetea haki zao. Kauli mbiu ya mwaka huu inaongozwa na “ nguvu ya wasichana: hailezeki na wala kusimamishwa. Aidha ameongeza kusema“ Tunasherehekea matokeo yaliyopatikana na, na kwa wasichana tangu kupitishwa kwa Azimio la Beijing na Jukwaa la hatua  ya ajenda kamili ya kisiasa miaka 25 iliyopita  ili iweze kuendeleza haki na sio tu za wanawake bali, hata za wasichana.

Harakati za kuzuia ndoa za utotoni

Harakati zinazoongozwa na wasichana zinashughulikia maswala kama vile ndoa za utotoni, usawa wa kielimu, vurugu za kijinsia, mabadiliko ya tabianchi, kujithamini na haki ya wasichana katika kuweza kuingia katika maeneo ya ibada au nafasi za umma wakati wakiwa kwenye siku zao za kila mwezi, hasa katika nchi ambazo kuna vizuizi hivyo.  Wasichana wapo wanajitahidi kuvunja mipaka na vizuizi vinavyowekwa na watu kwa sababu ya kutengwa, hata wale wenye kulenga watoto wenye ulemavu na wale wanaoishi katika jamii zilizotengwa. Kama wajasiriamali, wabunifu na wahamaishaji wa harakati za ulimwengu,wasichana wanaongoza na kukuza ulimwengu unaofaa kwao na kwa vizazi vijavyo. Wasichana wako wanajionesha kuwa hawawezi kusimamishwa, na  hakuna chochote kinachopaswa kuwazuia ushiriki wao wa haki sawa katika nyanja zote za maisha.

Video iliyoandaliwa na the Save  the Children

Na Shirika la Kimaifa la Saidia Watoto (Save the Children ) katika fursa ya Siku ya Kimataifa ya Wasichana, wametoa Video kuhusiana na manyanyaso ya kijinsia duniani. Shirika hili la kimaitaifa, kwa miaka 100 linapambania kuokoa watoto dhidi ya hatari na kuwahakikishia wakati wao endelevu ulio bora. Tangu leo yanaanza pia maadhimisho  karibu ya miaka 25 tangu azimio la Beijing la kuhusu Jukwa la kujikita katika matendo ya dhati. Hata hivyo data zilizotangazwa na Shirika hili linaangazia juu ya hali halisi ya kutisha kuhusiana na ubakaji na vurugu katika maeneo yenye mizozo na juu ya janga la ndoa za utotoni, huku wakisisitizia juu ya nafasi msingi wa elimu ili kupunguza matendo hayo ya ndoa za utotoni. Aidha taarifa yao inasema kuwa tangu leo hii hadi  mwaka 2030 ambao ni siku ya mwisho  wa kufikia Malengo ya Umoja wa mataifa katika na mojawapo likiwa la kusitisha ndoa za utotoni, lakini takwimu bado zinaonesha kwamba milioni 134 za watoto wa kike wataolewa na milioni 28,1 wataozwa mapema kabla ya kufikia umri wa miaka 15. The Save Children inasema, iwapo vijana wasichana duniani kote wangeweza kufikia angalau mwisho wa mafunzo ya sekondari, wangeweza kuzuia milioni 51 ya ndoa za utotoni kufikia mwaka 2030.

11 October 2019, 15:04