Tafuta

Vatican News
Bwana Guterres amesema,tunahitaji kuhakikisha kwamba kila mtu anahesabiwa,hususan watu walio masikini sana na wale walio hatarini. Hakuna mtoto azaliwaye bila kuandikishwa Bwana Guterres amesema,tunahitaji kuhakikisha kwamba kila mtu anahesabiwa,hususan watu walio masikini sana na wale walio hatarini. Hakuna mtoto azaliwaye bila kuandikishwa  (Albert Gonzalez Farran - AFP)

Siku ya Kimataifa ya Takwimu:ni kuwa na takwimu bora,maisha bora!

Katika harakati za maadhimisho ya Siku ya Takwimu duniani tarehe 20 Oktoba ya kila mwaka,Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Guterres amesema takwimu sahihi ni muhimu sasa kuliko wakati mwingine ili kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu SDGs.Hakuna mtoto azaliwe bila kuorodheshwa na hakuna kisa cha ugonjwa wowote kisiripotiwe.

Katika ujumbe wake wa kuadhimisha Siku ya Takwimu duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo tarehe 20 Oktoba ya kila mwaka, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bwana Antonio Guterres, amesema wakati nchi na mashirika yakijizatiti kutekeleza ajenda ya mwaka 2030 kwa ajili ya maendeleo endelevu, takwimu sahihi na zinazozingatia wakati ni muhimu sasa kuliko wakati mwingine wowote. Katika  mantiki ya siku ya takwimu duniani mwaka huu inaadhimishwa kwa kuongozwa  kauli mbiu, “Takwimu bora, maisha bora.” Takwimu sahihi ni muhimu kwa ajili ya kufanya maamuzi bora na wote katika jamii na hii ilitambulika tangu mwaka 2014 wakati Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha masharti ya takwimu rasmi kama njia ya kuhakikisha taarifa kwa umma. 

Bwana Antonio  Guterres amesema, “tunahitaji kuhakikisha kwamba kila mtu anahesabiwa, hususan watu walio masikini sana na wale walio hatarini. Hakuna mtoto ambaye amezaliwa hataandikishwa, hakuna kisa chochote cha ugonjwa licha ya eneo aliko hakitalipotiwa.” Aidha amekongeza kusema “tunahitaji takwimu muhimu na mahalia  ili kuhakikisha kwamba kila mtoto anafikia huduma ya elimu na tunahitaji takwimu za kimataifa za kufuatilia madhara jumla ya athari za mabadiliko ya tabianchi.” Umoja wa Mataifa umesema katika miaka 15 iliyopita, nchi nyingi wamepiga hatua katika kuimarisha uwezo wao wa kitaifa wa takwimu chini ya uongozi wa ofis iza kitaifa za takwimu. Kwa upande wake, Umoja wa Mataifa kupitia kamisheni ya takwimu kwa takriban miaka 70 imeongoza mfumo wa kimataifa wa takwimu na kupitia vigezo na uongozi wake kamisheni hiyo imebuni lugha ambayo inawezesha dunia kuzungumzia takwimu na kubadilishana uzoefu kimataifa. Katibu Mkuu huyo amesema, “kamisheni iko tayari kutekeleza wajibu wake katika kuendeleza na kuimarisha mchakato thabiti kwa ajili ya kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu.”

Hata hivyo, Umoja wa Mataifa umesema ufuatiliaji kwa ajili ya mafanikio ya malengo ya maendeleo endelevu inazua changamoto hata katika nchi zilizoendelea sana. Bwana Guterres amesema, “tunahitaji mabadiliko katika takwimu, tunahitaji kuimarisha uwezo wa ukusanyaji takwimu na kutumia teknolojia za kisasa, tunahitaji mchango na ujuzi wa wasimamizi wa takwimu na watumiaji na wasomi, sekta binafsi za vyama vya kiraia." Katibu Mkuu amesisitiza kwamba katika kuadhimisha siku hii, “ninatoa wito kwa wadau kufanya kazi pamoja kuhakisha kwamba uwekezaji sahihi unafanyika, vifaa vya teknolojia vipo, na sehemu mpya za kupata takwimu zinatumika na mbinu bunifu zinatumika kwa ajili ya kuhakikisha kila nchi inapata mifumo kamilifu ya taarifa wanazozihitaji kwa ajili ya kufikia maendeleo endelevu.”

Bwana Guterres vile vile hivi karibuni ametoa wito kwa viongozi na raia kufanya kazi pamoja kwa ajili ya amani Msumbiji. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema anfuatilia kwa karibu hali nchini Msumbiji kfuatia uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 15 Oktoba 2019 Vile vile Bwana Guterres kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake Ijumaa jioni tarehe 18 Okotba 2019 mesema Msumbiji imetoka mbali katika juhudi zake za kujenga amani ikizingatiwa pia makubaliano ya amani yaliyotiliwa saini hivi majuzi. Taarifa ya Katibu Mkuu imemnukuu akisema kwamba uchaguzi wa hivi karibuni ni hatua muhimu katika mchakato wa demokrasia wa nchi hiyo. Na kufuatana na hilo ametoa wito kwa watu wa Msumbiji, ikiwemo viongozi wa kisiasa katika nafasi mbali mbali na wafuasi wao, kuendelea kufanya kazi pamoja kwa ajili ya kuendeleza amani na utulivu wakati huu muhimu katika historia ya nchi hiyo.

21 October 2019, 13:53