Tafuta

Takwimu kuhusu umasikini wa watoto kwa mujibu wa shirika la kimataifa la Saidia Watoto Save the Children) Takwimu kuhusu umasikini wa watoto kwa mujibu wa shirika la kimataifa la Saidia Watoto Save the Children) 

Saidia Watoto:Idadi kubwa ya watoto Italia wanaishi katika umasikini!

Miaka kumi ya mwisho nchini Itali imeongezeka idadi ya watoto wanaoishi katika mazingira ya umasikini wa kutisha na ambao ni zaidi ya milioni moja.Hii ni kwa mujibu wa taarifa kutoka Shirika la Kimataifa la Save the Children ambalo tarehe 20 Oktoba 2019 imetoa Ripoti yake kuhusu hatari ya watoto hao.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Nchi ya Italia ni moja ya nchi katika Ulaya ambayo inaendelea kupoteza urithi wake mkuu ambao ni wa utoto. Ni kipeo kilichoonesha katika Ripoti ya Save the Children kwa kulinganisha hali halisi kati ya watoto wadogo na vijana kwa miaka 10 ya mwisho. Katika ramani hiyo ya nchi kuhusu watoto walioko katika hatari ya umasikini ndani ya familia zao, umefanywa utafiti wa miji kumi nchini Italia katika fursa ya Toleo la kwanza la Kampeni iliyopewa jina “tuangazie wakati ujao” ili kuweza kupambana na umasikini hasa wa kielimu, kwa mujibu wa ripoti hiyo mpya iliyotolewa.

Zaidi ya milioni ya watoto wanaishi katika umasikini wa kukithiri

Hali halisi ya kutisha ambayo imepigwa picha na Shirika la Kimataifa la Saidia Watoto inaonesha kwamba ni  milioni 1,2 ya watoto wanaishi katika umasikini wa kukithiri, na hiyo ina  maana ya kwamba mtoto 1kati ya10, lakini pia wanasema takwimu za idadi hiyo imeongezeka mara mbili kwa miaka kumi ya mwisho. Aidha mtoto 1 kati ya 7 ameacha shule na  walio wengi wanasomea katika majengo yasiyokuwa na usalama; mtoto 1 kati ya 5 hafanyi mazoezi ya michezo au shughuli za nje, mantiki zote hizo zinahatarisha uwezekano wa watoto kukua  akiwa na matumaini kwamba anaweza kuwa na  fursa za mustakabali bora wa maisha endelevu.

Kwa 2018, watoto 450,000 wamepewa vifurushi vya chakula

Umasikini kabisa, inamaanisha kutokuwa na hali ya kutosha ya makazi, kutokuwa na uwezo wa kutengeneza hata chakula cha kawaida chenye protini kwa siku kwa kila mtoto. Na kunako 2018 kulikuwa na watoto 450,000 waliopokea vifurushi vya chakula, hii ni idadi kubwa!  Amesema hayo  Bi Daniela Fatarella makamu mkurugenzi wa  Save the Children nchini Italia. Aidha anasema, kuna ukosefu mkubwa wa usawa kwa ngazi ya kijiografia, na hiyo ni kama kusema kwamba ,nchini italia inafanana na madoa ya Chui, mahali ambapo utaona kuwa sehemu kuanzia Kaskazini, za  Kati au Kusini mwa Italia huonesha tofauti kubwa ya namna ya kuishi.

Save the Children inaomba mpango mkakati kwa ajili ya utoto

Nyuma ya hayo yote anaendelea kusema Bi. Fatarella kuna tukio la umasikini ambalo limezidi kuongezeka hasa katika kipindi chote cha mwaka kuanzia  2008/2011. Kwa maana hiyo ni watoto ambao wanatoka katika familia ambazo zina mapato ya chini, kutokana na hali ambazo amesema  “tunaziita uwiano mdogo wa elimu”. Nchini Italia, anathibitisha kwamba hakuna mpango mkakati wa umoja kwa ajili ya msaada wa watoto na vijana ambao wanapaswa kuanza mapema hata kwenda shule za utotoni na ambazo zinakuwa ni dhamana yao ya ukuaji bora, na hasa  kwa ajili ya watoto wasiojiweza katika familia zao, amesisitiza mkurugenzi msaidizi wa Save the Children.

Kuhusu kampeni ya kukuza uelewa wa elimu

Kuanzia tarehe 21 Oktoba 2019 inafanyika wiki ya kampeni, kwa maana hiyo ni  mamia ya matukio mengi ambayo yameanzishwa nchini Italia kuanzia Kaskazini hadi Kusini yakihusisha hali halisi mahalia, vyama, shule, taasisi binafsi na taasisi za utamaduni ambazo kwa mwaka huu wamechagua kuwa bega kwa bega na  Shirika la Kimataifa la Saidia watoto  (Save the Children) ili kuhamasisha na kufanya mafundisho zaidi juu ya mada ya kupinga kwa dhati umasikini wa kielimu ambao kwa sasa unawakumba watoto na vijana, kadhalika hata kuhusu umuhimu wa kuchochea jamii nzima iliyoelimika katika kurudisha hadhi hii, ambayo inazidi kudidimiza chini nchi ya Italia.

Watoto wachache wanaozaliwa nchini Italia

Nchini Italia wanazaliwa idadi ndogo ya watoto na hii imechangiwa sana na kipeo cha uchumi ambacho kwa dhati kinaleta athari mbaya katika sehemu nyingi  na nyumba nyingi za familia. Na matokeo hayo pia yanajionesha katika uandikishwaji wa watoto katika mwaka wa kwanza wa shule ya msingi, kwa mfano katika mwaka wa shule 2019/2019, waliojiandikisha ni karibia  watoto 473.000, kwa upungufu wa watoto 23.000  ukilinganisha na mwanga uliotangulia kwa asilimia (-4,6%), na wakati katika orodha ya waliojiandikisa katika shule ya Sekondari inaangazia  wanafunzi 20.000.

Ongezeko la watoto wageni waliozaliwa nchini Italia tangu 2008

Hata hivyo kinachotia moyo ni tukio la ongezeka la watoto na vijana wageni waliozalia na wanafikia nchini Italia kwani kwa mwaka 2008 walikuwa ni zaidi ya 700.000 na miaka 10 baadaye wamekuwa zaidi ya milioni moja.  Matumizi kwa ajili ya watoto ni pungufu na hakuna haki, na kadiri miaka inavyozidi kwenda, ndivyo inavyozidi kuonekana hali halisi ya ukosefu wa usawa kijamii, kiuchumi na kijiografia. Katika nchi ambayo inazidi kuwa masikini kutokana na ukosefu wa watoto na ambapo mada ya ushirikishwaji kwa watu wapya au wageni  nchini Italia  inazidi kuwa dhaurua.

Watoto wanaishi katika mazingira ambayo hayana uoto wa asili,au kijani

Aidha ripoti ya Save the Children inaonesha kwamba licha ya umasikini wa zana za kufundishia kwa watoto nchini Italia, pia unasindikizwa  na umasikini wa mazingira mazuri.Na hiyo ni kutokana na kwamba wakati kuna mjadala wa ulimwengu unaowaka kuhusu mabadiliko ya tabianchi katika sayari, watoto na vijana nchini Italia wanazidi kukua katika maeneo ambayo yanakosa uoto wa ukijani, kwa ongezeko la Ekari 30,000 za maeneo yaliyo na simenti tu tangu  mwaka 2012 hadi 2018.  Asilimia 37 za watoto wadogo wanaishi katika maeneo 14 ya miji iliyo mikubwa, na katika mazingira ambayo hayafai kwa ajili ya watoto kama hao, na wakati huo mji 1 kati ya 10 haujishughulishi kuchukua jukumu la kupanda miti kwenye viwanja vya umma kama inavyosisitza sheria ya nchi. Tendo la kuona asilimia 44% za watoto na vijana wa Italia wanaokwenda shuleni kwa gari, haishangazi, hasa ukizingatia kwamba uwiano kati ya kila mtoto mchanga aliyezaliwa nchini Italia na mashine za gari zilizosajiliwa katika mwaka huo huo ni 1 hadi 4.

Ni haki watoto na vijana kuandamana kwa ajili ya mabadiliko ya kisiasa na kiutamaduni 

Katika nchi ambayo imeondoa kuwekeza  katika mji mkuu wake  thamani zaidi kwa wanadamu  hasa  ile ya watoto na vijana, ni kweli kabisa  kwamba vijana  wadogo wanayo sababu ya kutoa sauti ya malalamiko kwa watu wazima ili kuwarudishia wakati wao endelevu, ameeleza Bi Raffaela wa Shirika la Saidia watoto.Aidha amekumbusha kwamba, kuna uhusiano ambao unaunganisha harakati za ulimwengu kama  ule wa siku ya “Ijumaa ya siku zijazo” ambayo ni maelfu ya vikundi vya wasichana na wavulana na kati ya hizo, pia ya watoto wa harakati za  “Juu chini  kwa ajili ya “Saidia watoto, ambao kila siku wanajikita kuboresha ubora wa mazingira yao ya maisha. Ni suala linalolenga kubadilisha sana mtindo wa sasa wa maendeleo, kuwarudishia watoto sayari nzuri na nafasi za kukuza ule uwezo wao na maisha yao ya baadaye. SVile vile iwe ile ayari ambayo haiwakatazi watoto, bali inawafanya wawe mstari wa mbele kuandamana kwa ajili ya mabadiliko ya kina ya kisiasa na kiutamaduni kwa ajili ya kutete na kudai haki za wakati wao endelevu.

21 October 2019, 14:52