Tafuta

Serikali ya Tanzania imewasimamisha kazi watumishi saba katika Halmashauri ya Kilombero kwa ubadhilifu wa mali ya umma zaidi ya shilingi bilioni 1.3. Serikali ya Tanzania imewasimamisha kazi watumishi saba katika Halmashauri ya Kilombero kwa ubadhilifu wa mali ya umma zaidi ya shilingi bilioni 1.3. 

Wafanyakazi 7 watafuna Bilioni 1.3: Serikali yawachezesha "vidogoli"

Waziri Mkuu amewasimamisha kazi watumishi saba katika halmashauri mbili za wilaya ya Kilombero na kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha ya umma zaidi ya sh. bilioni 1.3 za makusanyo ya mapato ya ndani. Mbali na kuwasimamisha kazi watumishi hao, pia Waziri Mkuu ameagiza watumishi hao warejeshe fedha hizo ndani ya siku tatu kabla hajamaliza ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro.

Na Ofisi ya Waziri Mkuu, - Morogoro.

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi watumishi saba katika halmashauri mbili za wilaya ya Kilombero na kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha ya umma zaidi ya sh. bilioni 1.3 za makusanyo ya mapato ya ndani. Mbali na kuwasimamisha kazi watumishi hao, pia Waziri Mkuu ameagiza watumishi hao warejeshe fedha hizo ndani ya siku tatu kabla hajamaliza ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro. Watumishi hao ni pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Fransis Ndulane anayedaiwa sh. milioni tano alizoingiziwa katika akaunti yake bila maelezo yeyote. Waziri Mkuu amewasimamisha kazi watumishi hao leo, Jumapili, Septemba 15, 2019 wakati akiongea na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara, akiwa katika siku ya pili za ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro. Amesema “Mkoa mzima wa Morogoro umekuwa na tatizo la upotevu wa mapato, fedha zinakusanywa zinapita mikononi mwa watu hazifiki benki, hii ni shida, hatutavumilia. 

Waziri Mkuu amesema kwa mujibu wa taarifa ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) kipindi cha mwaka 2016 hadi Juni 2019, Katika mji wa Ifakara makusanyo yalikuwa ni bilioni 2.7 ambapo fedha iliopelekwa bank ni shilingi bilioni 1.9   na kwamba kiasi cha shilingi milioni 727 hazijulikani zilipoenda. Amesema katika mitambo kumi ya ukusanyaji wa mapato iliokaguliwa imeonyesha kiasi cha shilingi milioni 348 zilizokusanywa hazikupelekwa bank na hivyo kuishia mikononi mwa watu. Waziri Mkuu amesema katika uchunguzi huo ilibainika kuwa fedha hizo ziliingizwa katika akaunti mbalimbali za watumishi wa halmshauri hizo kutoka kwa mtendaji wa Kata ya Viwanja 60 katika Mji wa Ifakara aitwaye Gregory Midas. Watumishi   hao ni: Reina Mrema ambaye anadaiwa kuchukua kiasi cha shilingi 298, Haile Njitango milioni 7, Linus Mdembo kiasi cha shilingi milioni 2 kwa kushirikiana na mtendaji huyo wa Kata.

Hata hivyo Waziri Mkuu ameagiza Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA katika halmashauri ya Mji wa Ifakara, John Mvanga ambaye ndiye alibaini kuwepo na ubadhilifu wa fedha hizo na baadaye kusimamishwa kazi, arejeshwe kazini mara moja na asibugudhiwe. “Mlimsimamisha kazi kwa sababu mlijua amegundua madudu yenu, lakini haisaidii, arejeshwe kazini naagiza apewe ulizi wa kutosha.”  Kwa upande wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero, Waziri Mkuu amesema zaidi ya sh. milioni 600 hazijulikani zilipo huku kiasi cha shilingi milioni 98.5 zikidaiwa kuingizwa katika akaunti za watumishi wa halamshauri hiyo bila maelezo yeyote. Waziri Mkuu amewataja watumishi hao kuwa ni Devid Onyango aliyechukua kiasi cha milioni 51, Elakada Kanongole milioni 36, Fork Karunde milioni 8 na Charlse Chali milioni 2.5. Amesema kati ya milioni hizo 600 kampuni ya Kilombero Plantation LTD (KPL) ambao wanadaiwa kiasi cha shilingi milioni 531 ambazo hazikuingizwa katika mfumo huo.

 

15 September 2019, 14:35