Tafuta

Vatican News
UNICEF: Kuna zaidi ya watoto milioni 9.3 hawataweza kuanza masomo Kaskani mwa Afrika na huko Mashariki ya Kati kutokana na vita pamoja na umaskini wa familia zao. UNICEF: Kuna zaidi ya watoto milioni 9.3 hawataweza kuanza masomo Kaskani mwa Afrika na huko Mashariki ya Kati kutokana na vita pamoja na umaskini wa familia zao.  (Nadim Asfour)

UNICEF: Watoto milioni 9 huko Mashariki ya Kati hatawaanza masomo kutokana na vita!

UNICEF: Elimu ni ufunguo wa maisha, lakini kwa bahati mbaya, kuna watoto na vijana wanaoishi huko Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika, wenye umri kati ya miaka 15-17 ambao hawataka bahatika kuanza masomo katika kipindi cha mwaka 2019-2020 kutokana na vita. Inakadiriwa kwamba, zaidi ya watoto milioni 9.3 wataendelea kuathirika kwa kukosa masomo kwa sababu ya vita.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF, linasema elimu ni ufunguo wa maisha, lakini kwa bahati mbaya, kuna watoto na vijana wanaoishi huko Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika, wenye umri kati ya miaka 15-17 ambao hawata bahatika kuanza masomo katika kipindi cha mwaka 2019-2020 kutokana na vita. Inakadiriwa kwamba, zaidi ya watoto milioni 9.3 wataendelea kuathirika kwa kukosa masomo kwa sababu ya vita. Takwimu zinaonesha kwamba, nchini Siria kuna watoto milioni 3 ambao hawajawahi kwenda shule kuanzia mwaka 2014. Miundo mbinu ya elimu ipatayo 2, 160 imeshambuliwa wakati wa vita huko Siria, Iraq pamoja na Yemen. Katika mazingira kama haya, watoto wanakosa haki ya kupata elimu ili kuweza kupambana na hali pamoja na mazingira yao kwa siku za usoni.

Idadi kubwa ya watoto ambao hawataweza kupata nafasi ya kuanza au kuendelea na masomo kwa mwaka mpya wa masomo inachangiwa pia na umaskini wa familia hasa zile zinazoishi katika maeneo ya vijijini. Watoto hawa wanaacha masomo ili kusaidia kuchangia gharama ya maisha katika familia zao. Kwa watoto wa kike wanajikuta wakilazimika kuolewa hata katika umri mdogo, hali ambayo inakwenda kinyume cha haki msingi za binadamu. Uduni wa kiwango cha elimu na maeneo ya kufundishia pia yanachangia sana kwa watoto kutokuwa na kiu ya kutaka kuendelea zaidi na masomo. Kuna wanafunzi ambao wamejikatia tamaa na masomo kama Hisabati na Sayansi ni kati ya mambo yanayochangia pia kwa watoto wengi katika maeneo ya vita na kinzani za kijamii kutokuwa na ari na mwamko wa kupenda shule! UNICEF inakaza kusema, kuna haja ya kuwajengea watoto mazingira bora zaidi ya amani na utulivu, ili kuamsha tena ari na moyo wa kupenda kwenda shule. Idadi ya vijana wasiokuwa na fursa za ajira ni kubwa pia katika maeneo haya, jambo ambalo ni hatari kwa maisha yao kwa siku za usoni.

UNICEF
03 September 2019, 12:10