Tafuta

Aliyekuwa rais mstaafu nchini Msumbiji Robert MUGABE amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95 Aliyekuwa rais mstaafu nchini Msumbiji Robert MUGABE amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95 

Rais Mstaafu wa Zimbabwe Robert Mugabe afariki Dunia!

Aliyekuwa Rais Mstaafu nchini Zimbabwe Robert Mugabe amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95,tarehe 6 Septemba 2019 akiwa katika Hospitali moja nchini Singapore.

Na Padre Angelo Shikombe –Vatican News

Rais mstaafu Robert Mugabe aliyekuwa Rais wa Zimbabwe tangu mwaka 1980 hadi 2017 amefariki dunia tarehe 6 Septemba 2019 huko Nchini Singapore akiwa anapatiwa matibabu. Taarifa rasmi zilizotolewa katika mtandao wa “Twitter” na Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amesema, amepokea kwa masikitiko makubwa habari za kifo cha mwazilishi wa Zimbambwe na Rais mstaafu Robert Mugabe. Kifo chake kimetokea karibu miaka miwili tangu aondolewe madarakani kwa kile kinachoelezwa kuwa ni mapinduzi ya kijeshi. Rais huyo wa zamani tangu Aprili mwaka huu, alikuwa anipatiwa matibabu huko Singapore kutokana na ugonjwa ambao haukuwekwa wazi kutokana kuhifadhi faragha ya marehemu kwa mujibu wa taarifa. Aidha,Rais Emmarson Mnangagwa Rais wa Zimbabwe ameandika kuwa Mugabe alikuwa alama ya ukombozi wa Zimbabwe, alitumia muda wa maisha yake yote kuwajengea uwezo watu wa Zimbabwe na hivyo mchango wake katika taifa la Zimbabwe na Afrika kwa ujumla hautaweza kusahaulika.

Magufuli na Kenyatta wamlilia Mugabe

Pia kupitia ukurasa wa “Twitter”, Rais Josefu John Pombe Magufuli, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Rais Mstaafu na Baba wa Taifa la Zimbabwe Mzee Robert Mugabe. Akieleza huzuni yake Rais Magufuli amesema, Afrika imepoteza mmoja wa viongozi jasiri, shupavu, mwanajumuiya wa Afrika aliyekataa ukoloni kwa vitendo. Naye Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametuma salamu za rambirambi akisema, hana maneno ya kutosha kuelezea uzito wa kuachwa na kiongozi shupavu, shujaa na mzalendo wa Afrika ambaye alitekeleza jukumu muhimu katika kutete maslahi ya bara la Afrika. 

Mugabe alizaliwa 1924

Mugabe alizaliwa  tarehe 21 Februari 1924 kwenye koloni la Rhodesia. Alitupwa jela kwa miaka 10 bila ya kufunguliwa mashtaka kwa kuukosa uongozi wa Rhodesia. Na mwaka 1973, akiwa gerezani alichaguliwa kuwa Rais wa chama cha Zimbabwe (ZANU), ambacho alikuwa ni mwanachama mwanzilishi. Baada ya kuachiwa kutoka gerezani, alikimbilia Msumbiji na kuongoza mapambano ya kijeshi ya kudai uhuru. Licha ya kuwa mpiganaji wa vya kushtukiza, alisifika kwa kuwa mzuri kwenye majadiliano. Mpigania uhuru huyo wa zamani, aliendesha vita vya msituni dhidi ya utawala wa wazungu wachache katika kipindi ambacho Zimbabwe ikifahamika kama Rhodesia. Baadaye alipoingia madarakani, akawa mmoja kati ya viongozi wa muda mrefu kabisa barani Afrika. Ameheshimika na watu wengi barani Afrika kwa vita vyake dhidi ya walowezi wa kuzungu. Hata hivyo Rais mstaafu Robert Mugabe atakumbukwa kwa uzalendo wake kwa nchi ya Zimbabwe na bara zima la Afrika.

06 September 2019, 14:58