Tafuta

Huyu ni mwanaharakati kijana wa masuala ya mazingira kutoka nchini Sweden Greta Thunberg  akiwa katika kongamano la vijana jijini New York Marekani kabla ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa Huyu ni mwanaharakati kijana wa masuala ya mazingira kutoka nchini Sweden Greta Thunberg akiwa katika kongamano la vijana jijini New York Marekani kabla ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa 

New York:Vijana wanataka wakuu wa dunia kuchukua hatua ya mabadiliko ya tabianchi!

Tarehe 23 Septemba 2019 vijana wameandamana mjini New York Marekani kabla ya kilele cha Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya Tabianchi.Ujumbe wao kwa viongozi wa dunia ni kwamba hali kwa sasa ni ya dharura.Huo ni mkutano unaotaka kujaribu kuanzisha kampeni ya kimataifa dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.Ni takriban viongozi 60 kutoka dunani ili kuweza kuchukua hatua za kupambana na ongezeko la joto duniani.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kabla ya mkutano wa kilele wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi Jumatatu, 23 Septemba 2019 vijana wameandamana mjini New York. Ujumbe wao kwa viongozi wa dunia ni kwamba hali kwa sasa ni ya dharura. Katika kipindi cha miaka miwili na nusu tangu kuingia madarakani, Rais wa Marekani Donald Trump amefuta sheria kadhaa za kulinda mazingira na kuiondoa nchi yake katika mkataba wa mabadiliko ya tabianchi ulioafikiwa mjini Paris, ambao unalenga kuzuia ongezeko la joto ulimwenguni lisizidi nyuzi joto mbili. Lakini Umoja wa Mataifa Jumatatu 23 Septemba 2019 ndiyo umefungua mkutano huo katika makao yake makuu mjini New York. Ni mkutano ambao utataka kujaribu kuanzisha kampeni ya kimataifa dhidi ya mabadiliko ya tabianchi. Katika vikao viwili, takriban viongozi wa dunia wapatao 60 watatangaza hatua wanazopanga kuchukua kupambana na ongezeko la joto ulimwenguni. Umoja wa Mataifa umeamua kuwanyima nafasi ya kuzungumza viongozi wa mataifa ambao hawafanyi vya kutosha kutimiza malengo yaliyowekwa wakati wa Makubaliano ya Mabadiliko ya Tabianchi ya mjini Paris.

Na wakati huo huo kuna vijana bilioni 1.8 duniani leo, hiyo ni idadi kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa, ambapo ni muhimu wawe na sauti kuhusu mustakabali wa sayari dunia na mustakbali wao. Migomo ya kutohudhuria shule kwa ajili ya hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi ilianzishwa na mwanaharakati kutoka Sweden, Greta Thunberg katika mji mkuu wa Sweden Stockholm na migomo hiyo na mingine kote ulimwenguni ambayo imefuatwa na vijana kote ulimwenguni, na imeonyesha kwamba wanataka hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na wanataka nafasi ya kufanya maamuzi katika mchakato wa maamuzi. Wakati wa kuchukua hatua ni sasa. Kongamano la vijana linalofanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa litawaleta pamoja viongozi muhimu kwa harakati ya vijana kuhusu kongamano la hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na kutoa fursa kwao kushiriki na watu wengi zaidi. Takriban vijana 1,000 kutoka kote ulimwenguni wamehudhuria tukio hilo na wengine wengi wamefuatilia kwenye mtandao. Ni dhahiri kwamba ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kunahitaji ushirikishwaji wa kila mtu, vijana na wazee, walio nazo na walala hoi, kutoka mataifa yaliyoendelea na yale yanayoendelea. Vijana wanahitaji na wanafaa kuwa na nafasi kwa kile ambacho kinahitaji kuwa ni mchakato jumuishi na migomo ya kutohudhuria shule kwa ajili ya hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi zilitokana na ari ya kuwafanya viongozi wa dunia kufahamu na kuchukua hatua juu ya wasiwasi wao. Kama ajenda ya mwaka 2030 ya maendeleo endelevu inavyoainisha kwamba vijana ndio vinara wa maendeleo endelevu, ni wenye mawazo, ni watendaji na wabunifu ambao wanaweza kufanikisha maendeleo endelevu. Wana maslahi katika mustakabali kwani hii ndio sayari dunia watakayoirithi; ni wao ambao watakumbwa na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Kongamano kabla ya Kongamano la Umoja wa Mataifa ni jukwaa la vijana viongozi na mashirika yanayoongozwa na vijana ili kuonyesha hatua ambazo wanachukua kwa ajili ya ya kupunguza kasi ya mabadiliko ya tabianchi kwa lengo la kuweka viwango vya joto katika selsiasi 1.5 juu ya viwango vya kabla ya viwanda. Mwezi Mei nilizindua changamoto yenye jina “msimu wa joto wa suluhu” kwa ajili ya vijana kubuni teknolojia za suluhu dhidi ya mabadiliko ya tabianchi. Hii inajumuisha kutengeneza jukwaa kwa ajili ya kuwezesha taarifa za soko na hali ya hewa mashinani, kubuni vifaa vya teknolojia kwa ajili ya kuimarisha “uchumi mzunguko”, mfumo wa kiuchumi unaolenga kutokomeza taka na kutumia tena rasilimali. Kuwapa fursa  vijana wachanganuzi kujadili na viongozi wa kisiasa, ikiwemo kwa kuuliza maswali mazito na ya kuzua mjadala, vile vile kutoa suluhu thabiti katika jukwaa la Umoja wa Mataifa itakuwa muhimu kwani sauti za vijana zitasikilizwa. Zaidi ya hapo, na la muhimu zaidi, kwamba wanapatiwa jawabu na wanachangia katika maamuzi katika ngazi ya juu. Kongamano la vijana ni mkakati wa Umoja wa Mataifa wa hatua ya vijana kuelekea 2030 ambapo, kipaumbele cha kwanza ni ujumuishaji, ushiriki na uchagizaji kwa ajili ya kupaza sauti za vijana na kuimarisha dunia yeney amani, haki na endelevu.

Kongamano la vijana kuhusu hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi zitatoa kipaumbele kwa ushirikiano na viongozi kutoka serikali za mataifa, sekta binafsi na mashirika ya kiraia. Inatarajiwa kwamba idadi kubwa ya nchi kote ulimwenguni zitadhamiria kupata mawazo ya vijana wakati wa kubuni na kutengeneza sera za hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, mipango na sheria. Inatarajiwa pia kwamba kwa kuwezesha mijadala hiyo, viongozi wa mashirika watadhamiria kufanya kazi na kuwapa mafunzo, pamoja na kujifunza kutoka kwa vijana wawekezaji na au makampuni yanayoongozwa na vijana, wengi wa wale ambao wako mstari wa mbele katika kubuni suluhu kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Moja ya sauti muhimu kwenye kongamano la vijana, ni Greta Thunberg na kwa maana hiyo Vijana wanafikiria, kuhisi na kufanya vitu tofauti ukilinganisha na watu wazima na hilo ni la thamani wakati tukikabiliwa na kile Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amekitaja kama janga la uhai la mabadiliko ya tabainchi. Greta Thunberg ni mfano anayetia matumaini kwa vijana kote ulimwenguni na ni ishara muhimu kwa ari yao kuchukua hatua kuzuia mabadiliko ya tabianchi. Sio jambo rahisi kusikilizwa na viongozi wa dunia kama alivyofanya, kwa hiyo kwa mantiki hiyo anabuni harakati muhimu hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi ikiongozwa na vijana na isiyoweza kupuuzwa. Ninafurahishwa sana na wanaharakati vijana kutoka mataifa ya kusini, ambao huenda hawaangaziwi na vyombo vya habari; kwa mfano Venessa kutoka Uganda na Timothy kutoka Fiji na maelfu ya wengine wengi ambao ni wanaharakati wanaochagiza kwa ajili ya mustakabali wa pamoja na wanaunga mkono Greta kote ulimwenguni.

Ikumbukwe kwamba  akizungumza na waandishi habari kunako mwezi Agosti, mwaka huu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bwana Antonio Guterres alikuwa amewaambia viongozi wa dunia wasije katika mkutano huo na hotuba za kupendeza, bali waje na mipango halisi ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi. Bwana Guterres alikutana pia na wanaharakati hao vijana na kukiri makosa ya kizazi cha umri wake kuwa “Kizazi cha umri wangu kimeshindwa hadi sasa kulinda haki za binadamu pamoja na kuuhifadhi ulimwengu. Nina wajukuu. Nataka wajukuu wangu waishi katika dunia inayoeleweka. Kizazi cha watu wa umri wangu kina jukumu kubwa. Na kizazi chenu lazima kituwajibishe kuhakikisha hatusaliti musatakbali wa wanadamu,”. Na wakati huo huo taarifa zinasema kuwa  Rais Trump hatohudhuria mkutano huo wa tarehe 23 Septemba 2019. Na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres leo Septemba 21 ameungana na vijana na kutoka ulimwenguni kote katika kongamano la aina yake la vijana na hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi. Kongamano hili la vijana limefanyika siku chache kabla ya kongamano la Katibu Mkuu la kuitisha viongozi wa dunia kuhusu hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi ambalo limeanza tarehe 23 Septemba 2019. Bwana Antonio Guterres akihutubia vijana hao amesema kuwa, “nimekuwa mzungumzaji mara nyingi kuliko msikilizaji. Na hiyo ni moja ya changamoto za viongozi duniani: wanazungumza sana na wanasikiliza kidogo. Na ni katika kusikiliza ndipo tunajifunza.”hata hivyo ameelezea kufurahishwa kwake na uongozi na utofauti wa harakati za vijana kwa ajili ya hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi duniani leo. Katibu Mkuu amesema alipoanza jukumu lake kama mkuu wa Umoja wa Mataifa alikatishwa tamaa na uwezekano wa hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, na kuongeza kwamba, “tayari tunakabiliwa na dharura ya mabadiliko ya tabicnhi tunashuhudia, bila kuingia kwa undani sana, lakini tunashuhudia ongezeko la majanga ya asili yakiendelea kuwa makubwa na yenye madhara zaidi.”

Bwana  Guterres aidha ameongeza kwamba athari hizo ni dhahiri huku akitolea mifano mingi ikiwemo, “tunashuhudia ukame barani Afrika, kwa mfano katika baadhi ya matukio, siyo tu inafanya jamii kutoweza kuishi lakini pia inaathiriwa na mzozo kwa mfano Sahel, ambako ukosefu wa raslimali maji inasababisha wakulima na wengine kupigana, na kwa sababu hiyo inachochea kuzuka kwa mizozo na kusambaa kwa ugaidi.” Bwana Gutterres amesisitiza umuhimu wa vijana katika kuchagiza taasisi kusukuma kufikia mchakato wa kufanya maamuzi. Akiongeza kwamba “Hatuishi katika utandawazi wenye haki, cha kushangaza ni kwamba sio bara Afrika au visiwa vidogo kwenye ukanda wa Pasifiki au Carribea, ndio wachangiaji wakubwa wa mabadiliko ya tabianchi lakini ndio waathirika wakubwa. Bwana Guterres amehitimisha kwa kusema ana wajukuu na kwamba anataka waweze kuishi katika sayari dunia bora na kwamba, “kizazi changu kina wajibu mkubwa. Ni kizazi chenu kitakochotuwajibisha kuhakisha kwamba hatusaliti mustakbali wa binadamu.” Baadhi ya vijana ambao waliungana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ni Wanjuhi Njoroge kutoka Kenya akiwakilisha vijana kutoka Afrika amesema, “katika juhudi zetu za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kama wachangiaji wadogo wa uchafuzi wa mazingira na waathirika wakubwa, lakini sasa sio wakati wakunyosheana kidole ni wakati wa kufanya kazi pamoja, sisi vijana takriban milioni 625 kutoka Afrika tunoamba uungwaji mikono katika ufundi, kifedha na kubadilishana ujuzi na stadi” Katika hatua dhidi ya kukabiliana na kuzuia mabadiliko ya tabianchi. Mapema wiki hii

23 September 2019, 16:19