Waziri Mkuu wa Mauritius azungumzia kuhusu umuhimu wa: Upatanisho, haki na amani; Majadiliano ya kidini na Kiekumene pamoja na uchumi fungamani. Waziri Mkuu wa Mauritius azungumzia kuhusu umuhimu wa: Upatanisho, haki na amani; Majadiliano ya kidini na Kiekumene pamoja na uchumi fungamani. 

Hija ya Kitume ya Papa Francisko Mauritius: Amani, Ustawi & Mafao

Waziri mkuu wa Mauritius wakati akitoa hotuba ya kumkaribisha Baba Mtakatifu Francisko nchini mwake, amekazia umuhimu wa mchakato wa upatanisho, haki na amani; Majadiliano ya kidini na kiekumene kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi. Mauritius inataka kujikita katika uchumi fungamani kama sehemu ya mapambano dhidi ya umaskini wa kipato.

Na Padre Angelo Shikombe, - Vatican.

Kauli mbiu iliyoongoza hija ya Baba Francisko nchini Mauritius kuanzia Jumatatu tarehe 9 hadi Jumanne 10 Septemba 2019 ni “Hujaji wa amani”. Waziri Mkuu wa Mauritius Bwana Pravind Kumar Jugnauth, tarehe 9 Septemba 2019 katika ziara ya Baba Mtakatifu Francisko nchini Mauritius iliyofanyika katika Ikulu, alitoa hotuba yake iliyosheheni furaha na shukrani kwa mwenyezi Mungu kwa baraka alizomjalia Baba Mtakatifu Francisko, Khalifa wa Mtakatifu Petro ambaye amefika Mauritius baada ya miaka 30 kutoka ujio wa Mtakatifu Yohane Paulo II uliofanyika nchini Mauritius mwaka 1989. Akiwa ameguswa sana na vipaji vya Baba Mtakatifu ikiwemo unyenyekevu na upole wake, ukaribu wake kwa wahitaji na wanaoteseka, hekima yake na uchaji wake, moyo wake wa kuwajali maskini na waliosetwa na jamii, ujasiri wake wa kutetea haki za wafanyakazi, vyote hivi vimehuisha maisha ya kiroho ya watu.

Aidha amekiri kuwepo kwa mahusiano ya karibu kati ya nchi ya Mauritius na Vatican katika kutafuta haki na amani ulimwenguni.  Akijivunia mwitiko mkubwa wa watu waliofika kumpokea na kumsikiliza kutoka visiwa vya jirani, Waziri mkuu Pravind Kumar Jugnauth alimpongeza kwa neno lake la upatanisho na amani. Aidha, amemwalifu kuwa ziara yake imepyaisha akili na mioyo ya watu, watu sasa wanaishi kwa pamoja, wanajadiliana kati yao kwa maana majadiliano katika cnhi ya Mauritius ni kiini kinachounganisha mila na desturi za watu wahamiaji kutoka sehemu mbali mbali. Akipembua zaidi mada hiyo Bwana Pravind Kumar Jugnauth, ametaja umuhimu wa majadiliano ya kidini kama sehemu ya utume wa Kanisa.  Bwana Pravind amesema baraza la ushauri wa kidini lililoundwa mwaka 2001 ambalo linashughulikia masuala ya majadiliano kati ya wakristo na wasio wakristo kwa ngazi ya Taifa ili kuwezesha kufanya kazi kwa pamoja kwa nji zote kwa lengo la kuleta amani.

Utamadunisho huo kwa nchi ya Mauritius uko damuni, wakijenga umoja na kulinda heshima yak ila mtu dhidi ya tofauti zao. Kisiwa hicho katika udogo wake lakini kimesheheni ushuhuda wa upendo wa kuishi pamoja wakichukuliana tofauti za ona kudumisha utamaduni fungamani. Pamoja na changamoto zinazokuwepo za kiuchumi, lakini bado taifa la Mauritius lina fursa za kujiendeleza kuwaunganisha watu wa rika mbalimbali wakiwemo wazee, walemavu na waliotelekezwa pembezoni mwa jamii. Serikali inawategemeza waliowanyonge na kusimamia maadili ya jamii. Hata hivyo bado changamoto ni kubwa kwa upande wa sekta ya elimu. Serikali imejiwekea mkakati wa miaka 15 wa maendeleo ya taifa katika sekta ya elimu kuanzia mwaka 2015 hadi 2030. Kanisa la Mauritius limetoa mchango mkubwa sana katika utoaji wa elimu ndani ya miaka 150 iliyopita.

Kwa upande wa kidiplomasia, Waziri mkuu amesema, tangu Januari 2019 Vatican imewaomba wanasiasa kusikiliza mahitaji ya wananchi na kutafuta suluhu halisi kwa ajili ya manufaa ya wote. Huko ni kuheshimu haki za kila mtu za kitaifa na za kimataifa. Serika ya mauritius inajitahidi kulitekeleza hilo kwa moyo wote. Aidha Waziri Mkuu Pravind Kumar Jugnauti amemshukuru Baba Mtakatifu Francisko, kwa kuwajali wananchi wa Mauritius wanaoteseka baada ya kufukuzwa huko uingereza na visiwa vya Chigago kutokana na kutenganisha shughuli zisizo halali na zilizohalali wakati Nchi ya Mauritius haijapata uhuru. Katika vuguvugu hilo la kupigania uhuru, Mahakama ya haki za kimataifa imehitimisha kesi hiyo kuwa visiwa vya Chigago ni sehemu ya himaya ya Mauritius na kuwa Uingereza anawajibika kusitisha shughuli zake visiwani mapema iwezekanavyo.  Tangu muda huo Serikali ya Mauritius inaendelea na bidii za kuwasaidia wanachikago ili warudi katika visiwa vyao na kuwarudishia tena heshima yao. 

Baada ya kueleza changamoto hiyo kubwa inayoikumba nchi ya Mauritius Bwana Pravind Kumar ameungana na Baba Mtakatifu katika jitihada ya utunzaji wa mazingira iliyo Nyumba ya wote, akibainisha kuwa mabadiliko ya hali ya hewa ni janga la kila mmoja wetu. Suala hilo linahitaji ushirikiano wa pamoja katiak nyanja zote za kijamii, kiuchumi na kisiasa. Mauritius katika udogo wake inayo shauku ya kulitekeleza kwa vitendo. Akiendelea kumshukuru Baba Mtakatifu kwa ujumbe wake anaoutoa ulimwenguni, ujumbe wenye kuonesha kuguswa kwake na mahangaiko ya maskini, ikiwemo kusitisha matumizi ya nguvu za kijeshi katika utatuaji wa migogoro na badala yake mataifa yatumie nguvu ya majadiliano. Akihitimisha hotuba yake, Bwana Pravind Kumar Jugnauth amemshukuru Baba Mtakatifu kwa kutembelea kaburi la Mwenyeheri Padre Laval aliyekuwa ame sahaulika, na kumwhidia ushirikiano wa karibu kati ya nchi ya mauritius na Vatican. Hakika ziara ya Baba Mtakatifu imeamsha moyo mpya wa utendaji kazi nchini Mauritius.

 

10 September 2019, 17:28