Mgogoro kati ya Mauritius na Uingereza ni kati ya mada zilizogusiwa na Rais Barlen Vyapoory wakati wa hotuba yake ya kumkaribisha Papa Francisko. Mgogoro kati ya Mauritius na Uingereza ni kati ya mada zilizogusiwa na Rais Barlen Vyapoory wakati wa hotuba yake ya kumkaribisha Papa Francisko. 

Hija ya Papa Francisko Mauritius: Mgogoro: Mauritius & Uingereza

Rais Barlen Vyapoory hakusita kumshirikisha Baba Mtakatifu Francisko changamoto waliyonayo juu ya visiwa vya Chigago na Diego Garcia ambavyo nchi ya Uingereza inaendelea kuving’anga’nia. Hatua iliyofikiwa hadi sasa ni kuwa Mahakama ya kimataifa imeshaivitambua visiwa hivyo kama sehemu ya Mauritius. Jitihada za makusudi zinaendelea kufanywa ili kukamilisha taratibu zote.

Na Padre Angelo Shikombe, - Vatican.

Bwana Barlen Vyapoory Rais wa kipindi cha mpito nchini Mauritius, Jumatatu, tarehe 9 Septemba 2019 amempongeza Baba Mtakatifu Francisko kwa kufanya ziara yake ya kitume nchini Mauritius. Katika kuelezea furaha yake ya kihistoria kwa kumpokea Baba Mtakatifu nchini Mauritius, Rais Barlen Vyapoory hakusita kuonesha furaha yake ya kipekee akikumbuka historia ya nchi ya Mauritius katika mahusiano bora na imara iliyonayo kati ya  nchi hiyo na  Vatican. Akiwa amejawa furaha amesema, miaka 30 iliyopita mwasisi wake Rais Uteem, alimpokea Baba Mtakatifu Yohane Paulo II alipotembelea Mauritius mwaka 1989, sasa imekuwa bahati yake ya pekee kumpokea Baba Mtakatifu Francisko katika hija yake akiwaimarisha ndugu zake. Rais Barlen Vyapoory ameyaeleza hayo katika hotuba yake aliyoitoa katika mkutano wa Baba Mtakatifu na viongozi wa Serikali na vyama vya kiraia na viongozi wa dini huko Ikulu. Akimshukuru sana Baba Mtakatifu Francisko kwa kuipa heshima kubwa nchi ya Mauritius amesema, Nchi ya Mauritius ni kati ya nchi ndogo katika bahari ya Hindi. 

Hata hivyo Baba Mtakatifu ameona umuhimu wa kuitembelea katika maadhimisho yake ya kumbukumbu ya miaka 155 ya Mwenye heri Padre Laval tangu afariki dunia na  ambaye alionekana kusahaulika, lakini ndani ya Nchi hiyo alikuwa ni chanzo cha kuimarisha umoja wa kitaifa. Ikumbukwe kuwa, Nchi ya Mauritius inayoundwa na waamini wa dini na madhehebu mabalimbali  ya kikristo yanayounda umoja wa kitaifa. Hivyo ndivyo Nchi ya Mauritius imegeuka kuwa nchi ya kiroho ambapo Kanisa Katoliki linamchango mkubwa katika kujenga moyo wa wanamauritius. Rais Barlen Vyapoory amempongeza Baba Mtakatifu kwa jitihada anazozifanya za kutetea haki za wanyonge ulimwenguni kote. Ili nchi ya Mauritius iweze kubaki na kumbukumbu yake, Rais Barlen Vyapoory alimwomba Baba Mtakatifu kubariki miche lakimoja ya miti itakayopandwa katika visiwa vya Rodriguez na Agaléga kwa kumbukumbu yake. Mradi huo wa jamii ustaendeshwa kwa ushirikiano wa Serikali na Kanisa Katoliki.

Aidha Rais Barlen amemshukuru pia Kardinali Maurice Piat, kwa jitihada zake alizozifanya kitaifa katika sekta ya elimu. Rais Barlen Vyapoory hakusita kumshirikisha Baba Mtakatifu changamoto waliyonayo juu ya visiwa vya Chigago na Diego Garcia ambavyo nchi ya Uingereza inaendelea kuving’anga’nia. Hatua iliyofikiwa hadi sasa ni kuwa Mahakama ya kimataifa imeshaivitambua visiwa hivyo kama sehemu ya Mauritius. Jitihada zimeanza kuchukuliwa za kuwarudisha watu waliokuwa wamevikimbia visiwa hivyo kutokana na machafuko na vurugu mbalimbali.   Akihitimisha hotuba yake, Rais wa kipindi cha mpito Bwana Barlen Vyapoory kwa amemshukuru na kumkaribisha tena Baba Mtakatifu katika nchi ya Mauritius. 

[ Audio Embed Siasa: Mauritius] 

 

10 September 2019, 16:22