Tafuta

Vatican News
Mbu anayesababisha ugonjwa wa malaria kwa binadamu ni aina ya Anopheles.Lakini iligundulika hata mbu wa aina ya Aedes na Culex,wana uwezo wa kueneza magonjwa mengine kwa wanadamu,kama vile Dengue,homa ya manjano West Nile,Chikungunya,Zika na Filariosi Mbu anayesababisha ugonjwa wa malaria kwa binadamu ni aina ya Anopheles.Lakini iligundulika hata mbu wa aina ya Aedes na Culex,wana uwezo wa kueneza magonjwa mengine kwa wanadamu,kama vile Dengue,homa ya manjano West Nile,Chikungunya,Zika na Filariosi 

Siku ya mbu duniani 2019:wadudu kama mbu wanasababisha vifo zaidi ya 700elfu kwa mwaka!

Shirika la Afya duniani (WHO) linakadiria kuwa magonjwa yanayosababishwa na wadudu kama vile mbu huwakilisha asilimia17% ya magonjwa yote ya kuambukiza na kusababisha vifo zaidi ya 700,000 kwa mwaka.Malaria pekee husababisha vifo 400elfu peke yake!Hii ni taarifa kufuatia na kilele cha Siku ya Mbu Duniani 2019,inayoadhimishwa kila ifikapo tarehe 20 Agosti ya kila mwaka!

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 20 Agosti ya kila mwaka ni Siku ya mbu Duniani (World Mosquito Day). Siku hii huadhimishwa ili kumkumbuka daktari wa Uingereza Sir Ronald Ross, ambaye mwaka 1897 aligundua uhusiano baina ya mbu na ugonjwa Malaria.  Shirika la Afya duniani (WHO) liliweka siku hii kuwa maalum katika kujenga ule uelewa kuhusu mbu kama chanzo cha Malaria na namna ya kuthibiti ugonjwa huo.  Shirika la Afya Dunia (WHO) kwa hakika, linakadiria kuwa magonjwa yanayo sababishwa na wadudu kama vile mbu huwakilisha asilimia17% ya magonjwa yote ya kuambukiza na kusababisha vifo zaidi ya 700,000 kwa mwaka. Malaria pekee husababisha vifo 400,000!

Historia kwa ufupi ya ugunduzi wa Malaria na magonjwa mengine ya binadamu

Kunako1897, afisa wa matibabu wa jeshi la Uingereza huko India, Sir Ronald Ross, aligundua kuhusika kwa mbu katika mzunguko wa maambukizi ya ugonjwa wa malaria. Hata hivyo ugunduzi huu uliweza kumpatia hata Tuzo la Nobel ya Tiba kunako 1902. Walakini, ilikuwa kazi ya mwanasayansi wa Italia, aliyekuwa anaitwa Giovanni Battista Grassi kwa kushirikiana na wenzake ambao walithibitisha kwamba mbu wenye kuhusika zaidi na ugonjwa kama huo wa binadamu ni wa aina ya Anopheles. Ni baadaye tu iligundulika kuwa hata mbu ambao ni wa aina ya Aedes na Culex walikuwa na uwezo wa  kueneza magonjwa mengine kwa wanadamu, kama vile Dengue, homa ya manjano (Yellow Fever), West Nile, Chikungunya, Zika na Filariosi.

Ripoti inayohusu Siku ya kupambana na Malaria 2019 ya MSF

Hata hivyo katika kilele cha Siku ya kupambana na ugonjwa wa Malaria duniani, tarehe 25 April, Ripoti ya Shirika la Madaktari wasio na Mipaka MSF , walisema kuwa, hali ya ugonjwa wa Malaria katika nchi ya Kidemokrasia ya Congo hasa katika jimbo la Kivu Kusini lilikuwa ni mbaya. Ugonjwa huo hadi wakati huo ulikuwa umeathiri watoto zaidi ya 1,600 hasa katika wilaya ya Fizi. Aidha, walikuwa wamsema kuwa kuna changamoto nyingi kuhusiana na matumizi ya vyandarua.

Chanjo mpya ya kinga ya malaria kwa watoto kutoka WHO

Na wakati huo huo Shirika la afya duniani, WHO kwa mara kwanza katika historia  kwa  kilele hicho iliweza kuzindua programu ya majaribio ya chanjo ya Malaria kwa watoto nchini Malawi. Chanjo hiyo ijulikanayo kama RTS,S ni ya kwanza duniani ambayo inataka kuleta kinga ya malaria kwa watoto.  Naye Mratibu wa WHO katika programu hiyo Mary Hamel wakati wa uzinduzi hu alikuwa amesema kuwa, “Malaria bado ni janga kubwa linalosababisha zaidi ya vifo vya watoto 250,000 barani Afrika kila mwaka”. Hata hivyo kufiatia na sula la kinga mpya, Malawi, Ghana na Kenya ziliteuliwa kufanyika majaribio ya chanjo hiyo mpya iliyochukua miaka 30 kutengenezwa!

21 August 2019, 15:00