Ni zaidi ya watoto 500 wamekwisha fariki kati ya watoto 750 walioshambuliwa na Ebola huko DRC!
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican
Tamko la mwakilishi wa UNICEF huko DRC, Edouard Beigbeder anasema ni habari ya kusikitisha kwamba mtoto mwingine amefariki dunia na hiyo ikiwa ni kesi ya tatu kuthibitishwa uwepo bado wa Ebola jimbo la Kivu Kisini. Aidha amesema hii ni kuonesha hali halisi kwamba watoto ni waathirika sana kuhusiana na ugonjwa wa Ebola. Mtoto aliyefariki alikuwa na miezi 17 tu na wakati huo huo ni zaidi ya watoto 500 ambao tayari wamekufa kufuatia moto huo wa Ebola kati ya watoto 750 ambao wameshambuliwa tangu kuanza kwa mlipuko huo.
Ugunduzi wa hivi karibuni wa tiba mbili za kutibu Ebola ni muhimu
UNICEF inasema ugunduzi wa hivi karibuni wa tiba mbili yenye matokeo mazuri ni hatua nzuri na chanya dhidi ya mapambano ya Ebola, lakini hali halisi bado haitoshi kwa maana ya kuonesha uwazi na kasi ya hiyo ya maambuki na ndiyo maana suala la tiba ndiyo kiini kikubwa kutokana na kuendelea kuona vifo vikitokea. Na kutokana na hivyo ndiyo maana inakuwa muhimu kwa UNICEF kuendeleza jitihada zaidi za kufanya kazi ya kuhamasisha na kuhusisha jumuiya nzima kuhusu suala hili ambalo ni msingi kwa ajili ya kupata jibu linalostahili katika kesi hii ya Ebola.
Ghasia na ukosefu wa msimamo unawakilisha kizingiti kikubwa
Hata hivyo kuhusiana na hali halisi ya DRC, UNICEF pia inasema kuwa ghasia na ukosefu wa msimamo katika eneo kama vile la Walikale, linawakilisha changamoto kubwa la kuweza kuwafikia jumuiya iliyo shambuliwa. Ni muhimu kwamba, sehemu zote zenye kukumbwa na ghasia ziweze kudhibitiwa kwa uhakika na ili kwamba waokoaji waweze kuendelea na kazi yao kwa usalama na hata wale ambao wanatafuta msaada waweze kuwafikia bila wasiwasi wa kushambuliwa.