Tafuta

Virus vya Ebola bado ni tishio kubwa kwa afya ya binadamu nchini DRC ambapo kesi tatu zimeweza kugunduliwa katika jimbo la Kivu kusini.Hadi sasa watoto 500 wamefariki dunia kati ya 750 walioambukizwa Virus vya Ebola bado ni tishio kubwa kwa afya ya binadamu nchini DRC ambapo kesi tatu zimeweza kugunduliwa katika jimbo la Kivu kusini.Hadi sasa watoto 500 wamefariki dunia kati ya 750 walioambukizwa 

Ni zaidi ya watoto 500 wamekwisha fariki kati ya watoto 750 walioshambuliwa na Ebola huko DRC!

Kesi tatu zimethibitishwa katika Jimbo la Kivu Kusini kufuatia na kifo cha mtoto wa miezi 17 na kesi mpya katika mji wa Walikale kwa mujibu wa tamko la mwakilishi wa UNICEF, Edouard Beigbeder huko DRC.Hata hivyo amesema kuwa ni muhimu sehemu zote zenye kukumbwa na ghasia ziweze kudhibitiwa ili waokoaji waweze kuendelea na kazi yao kwa usalama hata wale ambao wanatafuta msaada bila kushambuliwa!

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tamko la mwakilishi wa UNICEF huko DRC, Edouard Beigbeder anasema ni habari ya kusikitisha kwamba mtoto mwingine amefariki dunia na hiyo ikiwa ni kesi ya tatu kuthibitishwa uwepo bado wa  Ebola jimbo la  Kivu Kisini. Aidha amesema hii ni kuonesha hali halisi kwamba watoto ni waathirika sana kuhusiana na ugonjwa wa Ebola. Mtoto aliyefariki alikuwa na miezi 17 tu na wakati huo huo ni zaidi ya watoto 500 ambao tayari wamekufa kufuatia moto huo wa Ebola kati ya watoto 750 ambao wameshambuliwa tangu kuanza kwa mlipuko huo.

Ugunduzi wa hivi karibuni wa tiba mbili za kutibu Ebola ni muhimu

UNICEF inasema ugunduzi wa hivi karibuni wa tiba mbili yenye matokeo mazuri ni hatua nzuri na chanya dhidi ya mapambano ya Ebola, lakini hali halisi bado haitoshi kwa maana ya kuonesha uwazi na kasi ya hiyo ya maambuki na ndiyo maana suala la tiba ndiyo kiini kikubwa kutokana na kuendelea kuona vifo vikitokea. Na kutokana na hivyo ndiyo maana inakuwa muhimu kwa UNICEF kuendeleza jitihada zaidi za kufanya kazi ya kuhamasisha na kuhusisha jumuiya nzima kuhusu suala hili ambalo  ni msingi kwa ajili ya kupata jibu linalostahili katika kesi hii ya Ebola.

Ghasia na ukosefu wa msimamo unawakilisha kizingiti kikubwa

Hata hivyo kuhusiana na hali halisi ya DRC, UNICEF pia inasema kuwa ghasia na ukosefu wa msimamo katika eneo kama vile la Walikale, linawakilisha changamoto kubwa la kuweza kuwafikia jumuiya iliyo shambuliwa. Ni muhimu kwamba, sehemu zote zenye kukumbwa na ghasia ziweze kudhibitiwa kwa uhakika na ili kwamba waokoaji waweze kuendelea na kazi yao kwa usalama na hata  wale ambao wanatafuta msaada waweze kuwafikia bila wasiwasi wa kushambuliwa.

21 August 2019, 14:29