Tafuta

Shirika la Afya Duniani WHO katika ripoti yake ya utafiti inasema chembe chembe zaplastiki katika maji zipo, lakini siyo haratishi kwa maisha ya binadamu kama maji machafu! Shirika la Afya Duniani WHO katika ripoti yake ya utafiti inasema chembe chembe zaplastiki katika maji zipo, lakini siyo haratishi kwa maisha ya binadamu kama maji machafu! 

Chembechembe za plastiki kwenye maji si tishio kama kunywa maji machafu!

Tarehe 22 Agosti 2019 Ripoti ya Shirika la Afya duniani (WHO) imetolewa kuhusu tafiti za athari za uchafu wa Chembechembe za plastiki na kwamba ziko kila sehemu lakini hazihatarishi afya ya binadamu zaidi ya maji yasiyo safi na salama ambayo yanaathiri watu bilioni mbili duniani kote na kusababisha vifo vya watu milioni moja kila mwaka!

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Shirika la Afya Duniani (WHO) kupitia tafiti yake ya athari za uchafu wa chembechembe za plastiki kwa binadamu limetoa taarifa yake tarehe 22 Agoasti 2019 kuwa plastiki zimepatikana katika mazingira ya viumbe vya baharini, katika maji taka na maji safi, chakula na hewa na maji ya kunywa iwe ya chupa au bombani. Kwa kawaida chembechembe hizo za plastiki ni zile ambazo ni chini milimita  5 kwa urefu na idadi kubwa hupatikana katika maji ya kunywa vikitokana na vipande vidogo vya chupa za plastiki za maji.

Maji yasiyo safi na salama yanaua watu milioni moja kila mwaka

Katika Ripoti hiyo Shirika la Afya Duniani WHO imesema kwa kuzingatia taarifa za sasa, uwepo wa chembechembe za plastiki hauhatarishi afya kwa viwango vya sasa lakini utafiti zaidi unahitajika Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi huo, Bruce Gordon kutoka kitengo cha afya ya umma, WHO imesema kwa sasa hatari kubwa kuliko chembechembe hizo za plastiki ni maji yasiyo safi na salama huku yakiathiri watu bilioni mbili duniani kote na kusababisha vifo vya watu milioni moja kila mwaka. Ameongeza kuwa muorobaini ni kuweka mifumo bora ya kuchuja maji na hivyo kupunguza uchafuzi wa plastiki ndogondogo kwa asilimia 90. Bwana Gordon ameongeza kuwa watumiaji wa maji hawapaswi kuhofia sana lakini,“Tunachagiza kufanyike mengi zaidi kupunguza uchafuzi utokanao na chembechembe hizo za plastiki na hiyo ni kutokana na wasiwasi wa hali ya sasa tunayoshuhudia na inasikitisha na hiyo ni zaidi ya utafiti wowote wa kiafya wa binadamu”.

Licha ya ripoti kuhusu athari za maji ya kunywa,WHO imeanza kufuatilia athari nyingine

Na kwa upende wake Jenniffer de France kutoka kitengo cha afya ya umma cha Shirika la Afya Duniani (WHO) imesema kwa sasa utafiti umejikita katika maji ya kunywa na huku akikazia kusema kwamba maji ya chupa yana chembechembe nyingi za plastiki ikilinganishwa na maji ya bomba lakini ametoa angalizo dhidi ya kufikia uamuzi kwani chembechembe zinazopatikana kwenye maji ya chupa za plastiki ni aina ya plastiki inayotumika kutengeneza chupa za plastiki na aina nyingine inatumika kutengeneza vikombe kwa hiyo utafiti zaidi unahitajika kuelewa plastiki hizi zinatoka wapi.  Aidha Bi  Jenniffer de France ameongeza kuwa ,“Ripoti hii imejikita na maji ya kunywa, lakini ni muhimu kuzingatia maeneo mengine ya mazingira, kwa kutambua hilo, Shirika la Afya Duniani (WHO) tayari imeanzisha mchakato wa kufuatilia athari za kiafya kwa binadamu kwa kuwepo katika mazingira yenye plastiki.

23 August 2019, 14:50